Mdude Nyagali, siasa zako sio nzuri. Jirekebishe

Mdude Nyagali, siasa zako sio nzuri. Jirekebishe

Labda kam miss Nyapara huko selo
Anajitahidi kuleta vurugu akamatwe akakae na Nyapara wake..
Huwezi jua
 
Vyama pinzani ni vizuri sana kwa maslahi ya taifa lakini Tanzania bado sana kuwa na upinzani wenye tija

Watanzania kupitia vyama pinzani vya cuf, chadema na act tujue tuu tunapotezewa nguvu na muda wa kudhania kuna upinzani

Siasa za hawa watu ni siasa za nje kutamu ndani kuzuri
Daaah.

Mtihani.

Unanipa msamiati mpya hapa.

Sasa "siasa za nje kutamu ndani kuzuri" ndiyo zipoje hizo?
 
Serikali ina mkono mrefu,mikono mingine haipitii mahakamani na magereza, ni njia ya kizani
 
Alimnyoa lini jiwe wakati mpaka anakufa yeye yupo jela anakula ugali wa bure, ajifunze lugha ya stara siasa sio lugha mbovu kama aliyoitoa hapo.
Pia ye ni mtu mzima ajue tu kuwa mama ana mkono kwenye kuachiwa kwake so aache USENGE.
 
Ni ivi : Kama akiendeleza wembe wa mfu wenu meko basi hatoacha kuambiwa ukweli
Sasa hapo kosa liko wapi, nyinyi mataga hii nchi msiifanye ya kwenu pekee, msituletee upuuzi wenu
Aisee! Watu mnajiamini sana aiseee!! Uraiani kuzuri rafiki yangu, usiombee ufike kule aisee!!
 
Tumekuonea huruma sana uliyopitia na hata wengi nje ya nchi wanajua masahaibu yako ila una lugha zenye ukakasi sana sijui unataka kuwaiga kina Khery James au kina Kihongosi?

Ushasikia kina Mwaipaya au Pambalu wa BAVICHA wakitumia lugha yenye ukakasi kama yako? I think haiatakuchukua hata week utaanza kumtusi kama Rais Samia, jiheshimu bana.

Wengi tunataka Katiba mpya ndiyo lakini hii style yako inakera sana

View attachment 1837535
Kwa hiyo wewe mdude Nyangali ni muuaji na unatishia kuua wengine?
 
Ana haki ya kusema kikatiba na kama ingekuwa alichokuwa anakisema enzi za mwendazake ni kosa basi wangemshitaki kwa makosa hayo. Kwanini wakambambikia madawa kupitia yule msichana? Uhuru ukishatolewa hautakiwi tena kuwekewa mazonge kuwa nikosoe kwa staha na mtu akiona katika kutumia uhuru wa kujieleza amekashifiwa basi sheria iko wazi aende mahakamani kufungua madai. Kwanini hatuendi na katiba na sheria zetu badala ya kutumia hila kubambikia watu makosa ili kuwakomoa kwa kutumia haki yao waliyopewa na katiba.
Huo ukosoaji ulimuletea shida kwanini hajifunzi, this is Africa brother ona mateso aliyopata na isingekuwa huruma angepotea
 
Mimi nawalumu sana BAVICHA kuhusiana na Mdude Nyagali. Katoka jela badala wamfanyie vipimo kamilifu vya kiafya (ikiwezekana hata nje ya nchi) na kumtafutia mwanasaikolojia ili akae sawa kiakili na kimwili na apumzike walau miezi miwili/ mitatu hivi ili apate utulivu. Wao mbio wametoka nae Mbeya kuja naye Dar kwenye kongamano walichokumbuka ni kumnunulia nguo na viatu. Kwa hili hata wakina Mbowe wanapaswa kulaumiwa walipaswa kuwaelekeza BAVICHA nini cha kufanya kuhusiana na Mdude. Kwa watu makini waliomwona Mdude akihutubia jana watakiri kuwa jamaa bado hajakaa sawasawa. Mdude ni mzungumzaji mzuri lakini hachugui maneno ya staha matokeo yake watu wenye busara wanamuona kama mhuni tu. Ushauri wa bure kwa viongozi wa Chadema wamuweke kijana chini wamfundishe namna nzuri ya kuchagua maneno wakati anahutubia kwani katiba mpya inahitaji kila mtanzania ashiriki kuanzia wazee, vijana n.k. Iwapo ataendelea kutuma lugha za kukwaza kama jana alivyotumia juu ya raisi wa nchi kwa kweli nina uhakika kuna baadhi ya kundi la watu mtawakosa kwenye harakati zenu za kutafuta katiba mpya kwani wote mtaonekana wahuni tu. Tunahitaji sana katiba lakini tunahitaji sana tufike kwenye hiyo katiba kwa amani na tukiwa wamoja kama tulivyo sasa bila kujali rangi, dini wala kabila zetu kwani siku zote sisi watanzania ni watu wa amani sana.

Mungu iabariki Afrika. Mungu ibariki Tanzania.
 
Back
Top Bottom