Mdude Nyagali, siasa zako sio nzuri. Jirekebishe

Mdude Nyagali, siasa zako sio nzuri. Jirekebishe

Tujadili hoja yake kwa utulivu kama imebeba ukweli au ni bangi fulani tu inasumbua.

Wembe anaojinasibu kumnyolea bwana yule ni upi na athari zake kwa bwana yule ni zipi hadi amtishe mrithi wa mikoba?
Walio karibu na Nyagali watoe majibu
Jamaa anamaanisha yeye bado yu hai lakini alienyolewa tayari hayupo duniani hivyo wa sasa ahiangalie asitende kama mtangulizi wake aje anyolewe.
 
eti wembe uliotumika kwa mtangulizi, hahahahahahahaha, kuna watu wanaaminishana ujinga sana aisee...wakati umekaa jela zaidi ya miaka 2 leo umetoka kwa huruma ( wanasema eti umeshinda kesi kwenye katiba hii hii wanayosema ni mbovu)...juzi hapa akina Malisa kule JF walipitisha mchango kumsaidia maisha halafu eti leo anajiona kashinda booonge la vita...
 
Wewe lini ulimuonea huruma? Nyinyi ndio mliokua mkipiga kelele asitoke, lugha za ukakasi ndio zinakunyima usingizi? Kama kavunja sheria peleka mashtaka mahakamani sio kutupigia kelele humu
mkishitakiwa kelele mkiachiwa kelele ni bora mfungwe tu.

Mnashauriwa mnaleta usera mavi
 
eti wembe uliotumika kwa mtangulizi, hahahahahahahaha, kuna watu wanaaminishana ujinga sana aisee...wakati umekaa jela zaidi ya miaka 2 leo umetoka kwa huruma ( wanasema eti umeshinda kesi kwenye katiba hii hii wanayosema ni mbovu)...juzi hapa akina Malisa kule JF walipitisha mchango kumsaidia maisha halafu eti leo anajiona kashinda booonge la vita...
Unakosea sana; wapi imetamkwa kua ametolewa kwa huruma? sema kilichotamkwa na majaji huko mahakamani siyo kupotosha jamii.
 
Jamaa anamaanisha yeye bado yu hai lakini alienyolewa tayari hayupo duniani hivyo wa sasa ahiangalie asitende kama mtangulizi wake aje anyolewe.
Hahahaaa basi jamaa ni noma na kweli mrithi amsikilize vyena bwana Nyagali
 
Respect kwako Kiranga[emoji123]
Mimi si mshabiki wa Magufuli, na wengi wanajua hili.

Ila ni mshabiki wa ukweli.

Mdude kamnyoa nani, lini, wapi, kivipi?

Tusije kulishwa matango pori kwa propaganda mbuzi za ushairi na ngonjera potofu ikawa tunakataa uzandiki wa CCM kwa kufuata uongo wa CHADEMA.

Maneno kama haya ndiyo yananifanya niseme matatizo yetu yamezidi vyama vya siasa.

Tuna matatizo ya utamaduni na elimu ambayo yanavuka mipaka ya vyama vya siasa. Yapo kotekote. CCM na upinzani.

Yani unapofikiri upinzani unaweza kubadilisha mambo, unakutana na vijana kama hawa wanaofikiri kupindapinda maneno tu ndiyo kitu kinachohitajika.

Mdude kababimbikiwa kesi ya madawa na mwanamke malaya, kijinga. Kakamatwa kama kuku wa mdondo.

Katuaibisha kiumeni.

Hana vetting mechanism. Yani hajui kuchuja kuona huu mtego. Akili yake ndogo, angalau kwenye hilo.

Kifupi, yeye ndiye kanyolewa. Kavuliwa nguo, both literally and metaphorically.

Sasa basi, watu wamemfanyia wepesi wamemsimamia kupiga kelele kwamba kesi kabambikiwa kwa sababu za kisiasa. Mpaka katoka.

Tunaambiwa mtu mzima ukivuliwa nguo, chutama ujisitiri dhakari na utupu wako. Watu wakufunike wakusitiri zaidi usiaibike.

Mdude kavuliwa nguo.

Badala ya kuchutama ajisitiri, anakimbia uchi kijiji kizima akipiga kelele kamnyoa mtu aliyemchezea shere.

Wakati watu na akili zetu tunaona sio tu Mdude ndiye aliyenyolewa, bali pia, hata akipewa wembe amnyoe mtu atajikata mwenyewe kwa papara zake.

Wazaramo wamejisemea.

"Zilongwa mbali, zitendwa mbali. Sakala Kandumbwa."

Najua unasema "Translation pleasee!".

Maanqnyqke, kinachosemwa na kinachofanyika ni vitu viwili tofauti. Mjinga kadanganywa.

Yani mtu kanyolewa, halafu yeye ndiye anasema kanyoa watu.

Sasa huyu akisema kaibiwa kura tutajuaje kaibiwa kura kweli, na haendelezi tabia yake ya kupindua maneno tu?

CHADEMA inatakiwa kufundisha vijana cha kusema.

Mimi sina tatizo CHADEMA wakiisema CCM.

Lakini, waiseme kwa ukweli na kauli zisizo na ambiguity. Haya mambo ndiyo tunayakataa CCM.

Sasa chama mbadala nacho kikiturudisha kulekule, kutakuwa na haja gani ya kuitoa CCM?
 
Pumbavu kabisa mkishitakiwa kelele mkiachiwa kelele ni bora mfungwe tu.

Mnashauriwa mnaleta usera mavi
Alaf yakikamatwa mabox ya kura fake day za uchaguzi , mkiuwa na kutia watu kwenye viroba ,mkifilisi watu na kuwaweka ndani mnahisi kuwa uchafu mnaoufanya hautokua na effect ? Msifanye watu ni wapumbavu siku hizi, ukifanya kosa lazima uambiwe ukweli
 
Mimi si mshabiki wa Magufuli, na wengi wanajua hili.

Ila ni mshabiki wa ukweli.

Mdude kamnyoa nani, lini, wapi, kivipi?

Tusije kulishwa matango pori kwa propaganda mbuzi za ushairi na ngonjera potofu ikawa tunakataa uzandiki wa CCM kwa kufuata uongo wa CHADEMA.

Maneno kama haya ndiyo yananifanya niseme matatizo yetu yamezidi vyama vya siasa.

Tuna matatizo ya utamaduni na elimu ambayo yanavuka mipaka ya vyama vya siasa. Yapo kotekote. CCM na upinzani.

Yani unapofikiri upinzani unaweza kubadilisha mambo, unakutana na vijana kama hawa wanaofikiri kupindapinda maneno tu ndiyo kitu kinachohitajika.

Mdude kababimbikiwa kesi ya madawa na mwanamke malaya, kijinga. Kakamatwa kama kuku wa mdondo.

Hana vetting mechanism. Yani hajui kuchuja kuona huu mtego. Akili yake ndogo, angalau kwenye hilo.

Kifupi, yeye ndiye kanyolewa. Kavuliwa nguo, both literally and metaphorically.

Sasa basi, watu wamemfanyia wepesi wamemsimamia kupiga kelele kwamba kesi kabambikiwa kwa sababu za kisiasa. Mpaka katoka.

Tunaambiwa mtu mzima ukivuliwa nguo, chutama ujisitiri dhakari na utupu wako. Watu wakufunuke wakusitiri zaidi usiaibike.

Mdude kavuliwa nguo.

Badala ya kuchutama ajisitiri, anakimbia uchi kijiji kizima akipiga kelele kamnyoa mtu aliyemchezea shere.

Wakati watu na akili zetu tunaona sio tu Mdude ndiye aliyenyolewa, bali pia, hata akipewa wembe amnyoe mtu atajikata mwenyewe kwa papara zake.

Wazaramo wamejisemea.

"Zilongwa mbali, zitendwa mbali. Sakala Kandumbwa."

Najua unasema "Translation pleasee!".

Maanqnyqke, kinachosemwa na kinachofanyika ni vitu viwili tofauti. Mjinga kadanganywa.

Yani mtu kanyolewa, halafu yeye ndiye anasema kanyoa watu.

Sasa huyu akisema kaibiwa kura tutajuaje kaibiwa kura kweli, na haendelezi tabia yake ya kupindua maneno tu?

CHADEMA inatakiwa kufundisha vijana cha kusema.

Mimi sina tatizo CHADEMA wakiisema CCM.

Lakini, waiseme kwa ukweli na kauli zisizo na ambiguity. Haya mambo ndiyo tunayakataa CCM.

Sasa chama mbadala nacho kikiturudisha kulekule, kutakuwa na haja gani ya kuitoa CCM?

Sio issue ya ushabiki ila ni issue ya ukweli na uwezo wa kujua kipi cha kuongea in public
Mdude anachuma janga upya hapa
 
Mwendazake alipokua anazungumzia mambo ya kupanua uku anakula mahindi alikua anamaanisha nini vile?
 
Mwendazake alipokua anazungumzia mambo ya kupanua uku anakula mahindi alikua anamaanisha nini vile?

Alikua anamaanisha kupanua eneo la biashara ila waliozoea kupanuliwa vinginevyo waliwaza vinginevyo pia

Na waliomuomba awapanulie eneo la biashara ndio waliompa mahindi ya kuchoma... kwani kuna ubaya!!?
 
Sio issue ya ushabiki ila ni issue ya ukweli na uwezo wa kujua kipi cha kuongea in public
Mdude anachuma janga upya hapa
Yani mimi naanza kuelewa kabisa kwa nini amekuwa catfished na huyo mwanamke na kubambikiwa madawa.

Inaonekana uwezo wake wa kuchambua aseme nini, afanye nini, wapi, kwa wakati gani, uwezo mzima wa kuchambua mambo, wafaransa wanaita "savoir faire", ni mdogo.

Na CHADEMA wanavyoshindwa kumpanga, hilo linaonekana kuwa si tatizo la Mdude tu.

Linaonekana ni tatizo la chama.

Sasa haya ndiyo matatizo tunayakimbia CCM. Tunataka upinzani utaotuvusha hapo.

Sasa chama mbadala nacho kinaturudisha kulekule jamani?

Whats the point of chama mbadala kama nacho kinarudi kwenye propaganda mbuzi?
 
Mwendazake alipokua anazungumzia mambo ya kupanua uku anakula mahindi alikua anamaanisha nini vile?
Na baadae alivyokua kilaza akawambia wabaki na mavi yao, hapo mataga walikaa kimya kwa sababu wanamuogopa alaf leo wanakuja kutupigia kelele kuhusu kunyolewa humu jf, hawa jamaa ni waajabu sana
 
Habari za leo wakubwa na Vijana wenzangu

Niende kwenye maada moja kwa moja. Mimi ni Shabiki wa siasa za kistarabu na Kujengeana uwezo kupitia kukosoana kwa lugha nzuri na zenye staha ili kulindiana heshima.
Sasa ndugu zetu wa Chadema, Mna huyu kijana ambaye ametoka rumande juzi juzi baada ya kukalishwa mahabusu kwa siku takribani 357 ni kijana anayeonekana kuwa kama Akili yake haijakaa sawa sawa.
Leo nikiwa naperuzi kwenye mtandao wa Kijamii Twitter, nikakutana na hii kauli ya Jamaa huyu mdude imenukuliwa

“WEMBE niliotumia kumnyolea mtangulizi wake nitautumia kumnyolea yeye akiendelea kuleta Jeuri”

Mimi niwaombe viongozi wa CHADEMA Mmwambie huyu kijana alinde sana maneno yake asijekurudi alikotoka.

NI HAYO TU
 
Dogo akiendelea asijekulialia tena atapotezwa vilevile na hakuna kitu Chadema watafanya.
Watakachoweza kufanya ni kuongea tu na kuongea hakubadilishi kitu.

Alafu sasa hivi anatakiwa ajue kuwa watz wengi wanamheshimu huyu mama.

Sasa yeye akianza maneno ya kukosa heshima kisha akapotezwa hakuna mtanzania atamuelewa.

Mama ana iile heshima mbali na kuwa raisi anaheshimiwa na wengi.
 
Back
Top Bottom