Mimi nimekemea MATAGA wanapotumia lugha kali na za uongo au zilizo vague.
Nimekemea kauli za Magufuli na za Samia. Nimekemea kauli za Kikwete na Mkapa. Nimekemea kauli za Makonda ma makada wengi wa CCM.
Na nilitegemea upinzani uondokane na siasa hizo za kauli za uongo na propaganda mbuzi, utuoneshe siasa tofauti, tuone hawa watu ni tofauti na CCM. Watatufaa.
Mdude kamnyoa nani jamani? Lini? Wapi? Kivipi?
Sasa kama upinzani unaendeleza siasa zile zile za propaganda, mtu kanyolewa, halafu anasema yeye ndiye kanyoa wengine, kwa nini nione huyu atanifaa zaidi ya CCM?
Mtu aliyenyolewa, halafu anasema yeye ndiye kanyoa wengine, siku akisema kaibiwa kura nitaamini vipi kaibiwa kura kweli, na hasemi hivyo kwa sababu ni tabia yake tu kupindua maneno?