Mdude Nyagali, siasa zako sio nzuri. Jirekebishe

Labda kam miss Nyapara huko selo
Anajitahidi kuleta vurugu akamatwe akakae na Nyapara wake..
Huwezi jua
 
Daaah.

Mtihani.

Unanipa msamiati mpya hapa.

Sasa "siasa za nje kutamu ndani kuzuri" ndiyo zipoje hizo?
 
Serikali ina mkono mrefu,mikono mingine haipitii mahakamani na magereza, ni njia ya kizani
 
Alimnyoa lini jiwe wakati mpaka anakufa yeye yupo jela anakula ugali wa bure, ajifunze lugha ya stara siasa sio lugha mbovu kama aliyoitoa hapo.
Pia ye ni mtu mzima ajue tu kuwa mama ana mkono kwenye kuachiwa kwake so aache USENGE.
 
Ni ivi : Kama akiendeleza wembe wa mfu wenu meko basi hatoacha kuambiwa ukweli
Sasa hapo kosa liko wapi, nyinyi mataga hii nchi msiifanye ya kwenu pekee, msituletee upuuzi wenu
Aisee! Watu mnajiamini sana aiseee!! Uraiani kuzuri rafiki yangu, usiombee ufike kule aisee!!
 
Kwa hiyo wewe mdude Nyangali ni muuaji na unatishia kuua wengine?
 
Huo ukosoaji ulimuletea shida kwanini hajifunzi, this is Africa brother ona mateso aliyopata na isingekuwa huruma angepotea
 
Mimi nawalumu sana BAVICHA kuhusiana na Mdude Nyagali. Katoka jela badala wamfanyie vipimo kamilifu vya kiafya (ikiwezekana hata nje ya nchi) na kumtafutia mwanasaikolojia ili akae sawa kiakili na kimwili na apumzike walau miezi miwili/ mitatu hivi ili apate utulivu. Wao mbio wametoka nae Mbeya kuja naye Dar kwenye kongamano walichokumbuka ni kumnunulia nguo na viatu. Kwa hili hata wakina Mbowe wanapaswa kulaumiwa walipaswa kuwaelekeza BAVICHA nini cha kufanya kuhusiana na Mdude. Kwa watu makini waliomwona Mdude akihutubia jana watakiri kuwa jamaa bado hajakaa sawasawa. Mdude ni mzungumzaji mzuri lakini hachugui maneno ya staha matokeo yake watu wenye busara wanamuona kama mhuni tu. Ushauri wa bure kwa viongozi wa Chadema wamuweke kijana chini wamfundishe namna nzuri ya kuchagua maneno wakati anahutubia kwani katiba mpya inahitaji kila mtanzania ashiriki kuanzia wazee, vijana n.k. Iwapo ataendelea kutuma lugha za kukwaza kama jana alivyotumia juu ya raisi wa nchi kwa kweli nina uhakika kuna baadhi ya kundi la watu mtawakosa kwenye harakati zenu za kutafuta katiba mpya kwani wote mtaonekana wahuni tu. Tunahitaji sana katiba lakini tunahitaji sana tufike kwenye hiyo katiba kwa amani na tukiwa wamoja kama tulivyo sasa bila kujali rangi, dini wala kabila zetu kwani siku zote sisi watanzania ni watu wa amani sana.

Mungu iabariki Afrika. Mungu ibariki Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…