Mbowe hajaanza siasa wakati wa Magufuli.
Mbowe ni mtu aliyefanikiwa sana kisiasa na kiuchumi kwasababu anajua kuishi na mwenye nguvu.
..kwa hapa Tz wenye mamlaka au " nguvu " huwa hawa-deal na watu wasiokuwa na influence.
..wakati ambao Mbowe alikuwa hashughulikiwi, wenye mamlaka walikuwa wakishughulikia viongozi wengine wa upinzani kama Mrema, Maalim Seif, Lipumba, Juma Duni, Dr.Wilbrod Slaa, etc.
..kabla Chadema haijaanza kushughulikiwa, wenye mamlaka walikuwa wanashughulika na vyama vilivyokuwa na nguvu wakati huo kama NCCR, CUF, na UDP.
..Kabla ya Chadema kuwa wanapigiwa miruzi kuwa ni chama cha kikabila cha Wachagga, wenye mamlaka walikuwa wanakituhumu chama cha UDP kuwa cha kikabila cha Wasukuma.
..Ukiona mpinzani haandamwi na hapatwi na mabalaa hapa Tz ujue kwamba wenye mamlaka wanaamini mpinzani huyo hana madhara.