Mimi ninaamini kwa desturi, maadili, mitizamo na mazingira ya kitanzania iwapo CDM na wadau wengine watadai katiba kwa hoja, hekima, busara,diplomasia, majadiliano na kimkakati wanaweza kufanikiwa lakini kama watatanguliza vitisho, nguvu, matusi na mashinikizo kwa mihemko kwa mamlaka zilizopo wajue hawatafanikiwa hili ni jambo kubwa linapaswa lipelekwe kwa umakini na siasa za ustaarabu.Hawana adabu hawa watu wanaoittwa cdm, jpm aje kuwanyosha tena, hawajui hata wanataka nini. Kwao kila kitu ni ni matusi.
Kitendo cha kutolea mfano na kigezo cha utawala wa awamu ya 5 pekee km hoja ya kuleta mabadiliko ya katiba haitoshi inaakisi nia ya kulipiza kisasi na chuki dhidi ya utawala wa awamu hiyo ambapo kimsingi tulitarajia takwa la katiba litokane na hoja za mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitekinolojia yalyotokea kuanzian1977.
Hiyo ndiyo hoja ya msingi na siyo kujikita kulalamikia utawala wa Magufuli tu kana kwamba kwa katiba hiyo hiyo awamu nyinginevhazikuwa ns tatizo kikatiba. Basi iwapo mwelekeo wa dhana ndiyo hiyo tatizo litakuwa mtu- uongozi na siyo mifumo.