Mdude Nyagali, siasa zako sio nzuri. Jirekebishe

Mdude Nyagali, siasa zako sio nzuri. Jirekebishe

Hawana adabu hawa watu wanaoittwa cdm, jpm aje kuwanyosha tena, hawajui hata wanataka nini. Kwao kila kitu ni ni matusi.
Mimi ninaamini kwa desturi, maadili, mitizamo na mazingira ya kitanzania iwapo CDM na wadau wengine watadai katiba kwa hoja, hekima, busara,diplomasia, majadiliano na kimkakati wanaweza kufanikiwa lakini kama watatanguliza vitisho, nguvu, matusi na mashinikizo kwa mihemko kwa mamlaka zilizopo wajue hawatafanikiwa hili ni jambo kubwa linapaswa lipelekwe kwa umakini na siasa za ustaarabu.

Kitendo cha kutolea mfano na kigezo cha utawala wa awamu ya 5 pekee km hoja ya kuleta mabadiliko ya katiba haitoshi inaakisi nia ya kulipiza kisasi na chuki dhidi ya utawala wa awamu hiyo ambapo kimsingi tulitarajia takwa la katiba litokane na hoja za mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi, kijamii na kitekinolojia yalyotokea kuanzian1977.

Hiyo ndiyo hoja ya msingi na siyo kujikita kulalamikia utawala wa Magufuli tu kana kwamba kwa katiba hiyo hiyo awamu nyinginevhazikuwa ns tatizo kikatiba. Basi iwapo mwelekeo wa dhana ndiyo hiyo tatizo litakuwa mtu- uongozi na siyo mifumo.
 
Zipo kauli kadhaa za dhihaka na vitisho kutoka kwa Mwenyekiti na makamu mwenyekiti wa Chadema zilizofuatiwa na matusi na dhihaka kwa Rais Samia zilizotolewa na Mdude...
Wewe umeleta uzi juu ya kuipongeza Yanga au juu ya matusi ya mdude??---- siye wa Simba wala hatukuelewi.🤔
 
Kabisa unadiliki kusema Mama Samia ndio alimwachia jamaa maana yake ni kuwa Mahakama IPO chini ya Mama Samia au sio??.
Ndio maana tunahitaji Katiba mpya!
Mama Samia hakumuachia bali ni Mahakama. Je unadhani kama Mwendazake angekuwa hai Mahakama ingeweza kumuachia Mdude?

Mara moja moja muwe mnatumia critical thinking Econometrician
 
Mimi ninaamini kwa desturi, maadili, mitizamo na mazingira ya kitanzania iwapo CDM na wadau wengine watadai katiba kwa hoja, hekima, busara,diplomasia...
JK aliwahonga, wakakimbia bunge la katiba, leo wanapiga kelele hapa! Ok nyinyi mashabiki wa CHADEMA mjue mkiti wenu alikuwa anaongwa na Kikwete kumchafua Lowasa
 
Adabu gani uliokua ukitaka awe nayo
Acha kutetea upumbavu mkuu,,
Sisi wengine tuko neutral na tulichukia sana utawala wa jiwe na tukamtetea sana huyu mt alivyobambikiwa kesi,,
Ila hizi kauli zake sio za staha kbsa hata kama katiba mpya inahitajika,
Ukifikiria sana unaweza kuconclude jamaa ana matatzo ya akili au kaathirika kisaikolojia.
 
Tumekuonea huruma sana uliyopitia na hata wengi nje ya nchi wanajua masahaibu yako ila una lugha zenye ukakasi sana sijui unataka kuwaiga kina Khery James au kina Kihongosi?...
Huyo hana cha kujirejebisha. Huyo ni chizi tu. Kama CHADEMA ikimsaidiabsawa, ila kwa sasa inatosha, wanapaswa wajitenge naye. Ni mropokoja mwenye kauli za kiwehu.

Yaani like seriius wanampa mtu kama Nyangali platform ya kuongea? Hakuna mtu mwenye akiki timamu anayeweza ki side na kundi linalomkumbatia mtu wa aina hiyo.

Pia, kwa wale tunaokemea na kulaani tabia za Mdude tujiulize je, huwa tunakemea watawala wakipotoka? Juzi rais ameongea kuhusu kuyapuuza madai ya Katiba kwa sasa, je tuliweza kukemea hilo?
 
Mama Samia hakumuachia bali ni Mahakama. Je unadhani kama Mwendazake angekuwa hai Mahakama ingeweza kumuachia Mdude?

Mara moja moja muwe mnatumia critical thinking Econometrician

Unathibitisha mwendazake na sasa mama ndiyo wanaozielekeza mahakama ya nini cha kufanya!

Jambo la hatari kabisa lenye kuhitaji kuwekwa sawa mapema iwezekanavyo.
 
Kiukweli napenda Siasa za mageuzi lakini jamaa hapana anatumia lugha Kali Sana ambayo inaweza Fanya kiongozi aka react.
Rais alishasema kosoeni na mtoe na mbadala lakini huyu jamaa Yuko radical Sana aisee.Mbowe unahitaji ku mentor vijana wafanye constructive criticism na Soo hizi provocation
 
Kuna watu bila kick hawafiki mbali na wengine kushikwa, kufungwa, kwenda mahakamani ndio ina mboost bila hayo anapotea wanajijuwa sasa itokee apuuzwe atarusha na ngumi ili akamatwe kusudi tu.

Fanya siasa ila mtu yoyote anayetaka kuleta vurugu asivumiliwe na ajuwe siku akiingia kwenye 18 atakuja kufungwa na watu wengine wanaomtumia pia kugain katika siasa wakiona hana mvuto wanamtupa huko.

Enzi za siasa za kina Mandela zimeisha asitake kujifanya mpiganaji. Haijalishi hukubali siasa lakini kumtishia kiongozi wa nchi hapana hili likemewe kwa nguvu.
 
Kusema wembe uliotumika kunyoleo utakua huo huo

Sasa hapo amekosaje adabu?

Ukiona hivyo basi ni wale waliokua wamempa jiwe uungu!

Sioni kosa lolote hapo la mdude kusema hivyo!
Hata Raisi Mama Samia anawashangaa wanaomshangaa Mdude.
Bado watu wanaishi enzi za Jiwe.
 
Naona amekumbuka mabwana zake wa jela anataka kurudi tena
 
Tumekuonea huruma sana uliyopitia na hata wengi nje ya nchi wanajua masahaibu yako ila una lugha zenye ukakasi sana sijui unataka kuwaiga kina Khery James au kina Kihongosi?

Ushasikia kina Mwaipaya au Pambalu wa BAVICHA wakitumia lugha yenye ukakasi kama yako? I think haiatakuchukua hata week utaanza kumtusi kama Rais Samia, jiheshimu bana.

Wengi tunataka Katiba mpya ndiyo lakini hii style yako inakera sana

View attachment 1837535
View attachment 1839252
Huu sio uana harakati bali ni upumbavu na ujinga huyu alistahili abaki ndani kwanza.
 
Niwaombe tu Chadema kama hawana ya kuzungumza basi kukaa kimya nako ni uungwana.

Katikati ya utulivu tulionao siyo haki kuwaweka mstari wa mbele wanasiasa roporopo kwani wataligharimu taifa pamoja na Chadema kama chama kinachoendeshwa kwa kodi za wananchi maskini.

Nawatakia Dominica yenye baraka!
 
Back
Top Bottom