Yawezekana nisieleweke vyema katika hili ila wale mnao mweleza Gwajima kuwa atachaguliwa na waumini wake kwa hivyo atashinda mnamdanganya.
HAKUNA muumini anae ishi maeneo Mikocheni Masaki Mikocheni anasali kanisa la la Gwajima, waumini wa makanisa haya ni wakazi wa Mbagala rangi TATU,Chalambe na Majimatitu na wote ni wakazi wa WILAYA moja anayoongoza Godwini Gondwe.
Kwa maana hiyo Gwajima angeshinda kama angepitishwa Temeke
Hata kama hao waumini wote ni wa wakazi wa KAWE...
Lililo la kweli ni hili;
Kwamba, waumini hao watakuwa wanaugua "UGONJWA WA UKOSEFU WA MAARIFA YA KIROHO" kama baba yao aliyepewa jukumu la kuwalea KIROHO watampa jukumu la KISIASA badala ya "KUKAA NYUMBANI MWA BWANA (BABA MUNGU) SIKU ZOTE"....
Kwa maoni yangu, nina hakika uamuzi huu wa Mch. Gwajima utakuwa umewachanganya sana waumini wake.....
Lazima wamegawanyika Makundi mawili...
Hata Yesu Kristo jaribu hili la kutaka kufanywa mfalme (mwanasiasa) lilimkuta lakini alilishinda vyema...
(SOMA INJILI YA YOHANA SURA YA 6 YOTE)
Ilitokea kuwa, walipoona anatenda miujiza sana, walimfuata na kutaka kumfanya "mfalme wao"...
(Mstari wa 14, 15)
".... 14. Basi watu wale walipoiona ishara (muujiza) ile, walisema, hakika huyu ni nabii yule ajaye ulimwenguni. 15. Hali Yesu akitambua walitaka kuja kumshika (kumchagua kwa kura) ili wamfanye Mfalme, akajitenga (akawakatalia), akaenda tena mlimani peke yake......"
Watu hao walitaka awe mfalme wao siyo kwa sababu kweli walikuwa na dhamira safi mioyoni mwao, bali ilikuwa ni kwa sababu ya miujiza aliyoitenda...
Katika mawazo yao, walidhani kuwa, kwa kuwa mfalme wao basi wapambe wangeweza kunufaika na faida ya miujiza hiyo....
Kwa ufupi ni kuwa kusudi lao la kutaka kumfanya mfalme lilikuwa motivated na tamaa za kimwili zaidi na siyo KIROHO au UPENDO WA KIMUNGU...
Kwa kutambua hilo, YESU KRISTO aliwakwepa....
Sijui motives za Mch. Josephat Gwajima ni nini kwa kweli. Je, ni msukumo wa Roho Mtakatifu au ni tamaa yake mwenyewe tu?
Kanuni iko hivi;
Kama ni Mungu mwenyewe kamtuma na kumwagiza aache kujikita kwenye kazi ya wito wake wa UINJILISTI na UCHUNGAJI na UALIMU na UTUME na UNABII badala yake agombee Ubunge (nafasi ya kisiasa) ili aliyemtuma (MUNGU YEHOVA) atimize kusudi lake, basi itakuwa vile bila kujali ana waumini Kawe au Charambe au popote pale kwa sababu KUSUDI LA MUNGU HALISHINDWI na HALINA MAJUTO....
Lakini, upande wa pili kama Mch. Josephat Gwajima kwa sababu ya tamaa zake tu kaamua kujituma kwenye jukumu jingine bila uongozi wa Mungu, HAKIKA huu ndiyo utakuwa mwanzo na mwisho wa wito wake....
Mungu atamnyang'anya huduma yake na kumpa mtu mwingine. Kwa kimombo tunasema, IT'S THE BEGINNING AND THE FALL OF GWAJIMA....!!