1: Mwita Waitara vs John Heche
2: Tulia Acskon vs Sugu
3: Askofu Gwajima vs Halima Mdee
4: Mrisho Gambo vs Godbless Lema
Hizi ni mechi kali sana za kukata na shoka .
Nategemea wote wafanye kampeni za kistarabu, wakinadi sera zao ili tuamue nani wawe wawakilishi,
Hakuna sehemu yeyote CCM itashinda hapo
1.Kwa Sugu, kumbuka kwa sasa ngome ya Chadema ni nyanda za juu kusini!! Hakuna Jimbo CCM watashinda nyanda za juu kusini hasa Mbeya!!
2. Heche lazima atamshinda Mwita. Watu wa Tarime nao wanajitambua sana. Hawawezi kuhamishia matatizo ya wana ukonga Tarime. Mwita ni mbunge aliyefeli vibaya sana Ukonga. There is no way akaenda kushinda Tarime.
3. Kuhusu Mdee- Mdee anaenda kumpiga vibaya sana Gwajima. Gwajima kwa jimbo la Kawe hawezi kupita kwa sababu Kawe ni Jimbo la wasomi sana na watu wanaojiweza kifedha sana. Sio watu wa mihemko na ujinga.
Pia Gwajima ana scandals chafu sana ikiwemo ya ukabila baada ya clip zake kusambaaa mitandaoni akihamasisha wasukuma kuunda vikundi vya kikabila ili kum support magufuli. Project ya wapwa tuinuane ni ya Gwajima na hata polisi walimuita kuongea nae.
Mwisho gwajima ana uchafu mwingi wenye ushahidi wa wazi, kujirekodi akifanya mapenzi na wanawake ni moja ya machafu yake na piani mpotishaji mkubwa. Rejea mphiphilo kwenye korona. Kwa iyo sioni akipewa ushindi kwenye jimbo la wasomi na wenye fedha kama Kawe!!!
4. Mrisho Gambo na Godbless Lema.Hapa Gambo ana kazi kubwa kwa sababu alitumbuliwa vibaya kwa kashfa nyingi na Magufuli mwenyewe. Sioni ni kwa namna gani anaweza kujisafisha hapa kwa watu wa Arusha. Pili Gambo ana majivuno sana na ubabe wa kijinga mambo yaliyompelekea watu wengi sana kumchukia. Kwa hapa Naona Lema akimshinda Arusha
Mwisho ni nguvu ya Ushawishi ya Lissu. Hapa Nina uhakika wa asilimia 100. Nguvu ya Lissu itawabeba wana Chadema wengi sana mwaka huu maana Magufuli nae ana hali mbaya kwa Lissu