Mechi kati ya Al ahly Vs Raja na CR Beouilzdad Vs Mamelody

Mechi kati ya Al ahly Vs Raja na CR Beouilzdad Vs Mamelody

Hakuna timu ya kucheza na mamelod hata mashibdano yangeanza upya
Al Ahly ni kama Real madrid kadri anavyozidi kusonga mbele ndivyo anavyozidi kuwa mgumu zaidi kufungika. Mpira alionesha Raja kwenye group stage, tulitegemea angetoa ushindani mkubwa kwenye mechi ya robo fainali ila ndio hivyo kala chuma mbili. Ana kazi kubwa sana ya kupindua matokeo
 
Raja ni timu ya kawaida inayobebwa na ubora wa wachezaji wawili watatu pale mbele so binafsi sijashangaa.
Magoli Yao mengi yamefungwa jumlisha na uwezo binafsi wa mfungaji.
 
Timu yetu ya Simba sc inatakiwa itumie sana full backs katika mashambulizi...nimecheki hizi timu za robo fainali ...huwa zinapopanda kushambulia basi fullbacks huwa ni sehemu ya mashambulizi tofauti na sisi...timu inashambulia ila utaluta kina kapombe na shabalala wapo nyuma..au full back anapewa pasi hajui wapi apige cross au v-pass...na akipiga cross utakuta amebutua tu bila kuwafikia walengwa
Mkuu tactics na Technic za mechi zinatokana na resource ulizona ambao ni wachezaji,huwez kua unacheza na mualabu ana winga zinakimbia kuliko beki zako alafu uruhusu mabeki zako wawe juu mda mwingi mtaumia,..na hii ndo kazi ya kocha kumsoma mpinzani kujua strength zake na weekness alaf unachambua na zako llili ujue utamkabili vipi
 
Hili goli la 2 la Al Ahly mfungaji ali unawa mkono na refa hakuona lkn kaita kati ..

Ingetokea bongo hii wale wachambuzi hasa hasa wa wachafu fm hasa hasa yule george lazi + edo wange shikia bango.mnooo
La kwanza pia.ni offside kabisa
 
Ingekua taifa jana lingekataliwa
VAR kwa Africa bado bado sana, msimu uliopita Simba walilalamika sana kule Africa kusini kwa kitotendewa haki na maamuzi. Jana pia uwanja wa Mkapa ilitokea tukio lililolazimika kuangaliwa kwenye VAR. Kwa mechi za ulaya tunaona wanaangalia kwanza tukio la kwanza kisha wanakuja kwenye tukio la mwisho. Kabla ya faulo ambayo ilikuwa inapelekea kuwepo au kusiwepo kwa penati, kulipaswa kuangaliwa kwenye hiyo hiyo move kama aliye receive mpira kama yupo onside position au offside position. Lakini VAR imeenda kuhukumu tukio la mwisho kabisa la faulo
 
Mbona unatumia nguvu kutuaminisha ujinga
Kama mimi ni mjinga, wewe unaetumia nguvu kutuaminisha yale ambayo bado hayajatokea uitwe nani?

Yani unataka kulazimisha kila mtu amuone Mamelod ni bingwa?

Hili kombe ni la mwarabu.
 
Back
Top Bottom