Mechi ya Simba na Yanga yasogezwa mbele. Kuchezwa 25 June, 2025

Scars
unaitwa huku mbona jana ulikuwa unarindima na hukuacha hata akiba ya maneno baada jana Ahmed Ali kupiga mikwara yote

Nikikuambia wewe bado mtoto unakasirika
Wewe raisi unafanya nini kwenye nyuzi za kijinga jinga namna hii? Huku ulipaswa kuingia na ile I'd ya 2017 na sio hii ya raisi wetu kipenzi cha watanzania 🤔
 
Iwe funzo kwa bodi ya ligi na huyo kiongozi wao aliyepiga simu ambaye tunajua atakuwa yule waziri shabiki wa kolo, wanataka kuuwa ligi kisa mapenzi ya timu yao ,wanapokuwa viongozi waweke unazi pembeni wafanye kazi waliyotumwa na raisi, ni aibu kwa ratiba za ligi hadi raisi aingilie
Karia kazi imemshinda atoke tu
 
Mkuu, bado hatujajua wamekubaliana nini huko, ni vema kusubiri matokeo.
Kama nikusubiri matokeo yatakuja yale yale viongozi wa bodi kutafutiwa sababu wajiuzulu kwa ridhaa zao bila kulazimishwa. Na kwakuwa serikali imeingilia hilo ni jambo la kawaida kabisa kutokea.
Najiuliza je, wakifanya hivyo na FIFA wakaja kugundua hayo nini kitafuata?
 
Hivi bodi na viongozi wa TFF wamejiuzulu au yanga wamelipwa pesa zao.
Hizi zote ni mchezo wa kufifisha no reform no electionI
Nadhani lazima watakua wameweka sawa hayo mambo hasa kuhusu malipo yao, na kwa maoni yangu mimi, wale viongozi hata kama hawataondolewa basi watakua wamejifunza kitu kupitia moto walipata safari hii.
 
Busara za tarehe 8 ndio hizi za tarehe 13. Tukihitaji kanuni na taratibu tunaanzia tarehe 8 kisha mechi inapangwa upya
 
🥱🥱 Rais mama yenu ameamua kuwaokoa Tff vinginevyo wangeita maji mma!!.
Hajaokoa chochote bali anajaribu kuingilia masuala ambayo hayamuhusu kama serikali.
 
haikutakiwa kuwa hivi, na hii inaonesha Shirikisho limeshindwa kutimiza wajibu wake,
 
Yanga imebarikiwa kuwa na viongozi na mashabiki wajinga sana
Kuna mashabiki na viongozi wajinga kama wa umbumbuni? Watu wazima mnakaa ukumbuni mnaletewa manzoki mnapiga makofi,,mnaambiwa kateni tiketi mechi inachezwa kwa mkapa na nyie mnaliunga tu kama mmekatika vichwa kisha mnaibiwa mchana peupe,,Sasa nyie akili zimo kweli?
 
Nadhani lazima watakua wameweka sawa hayo mambo hasa kuhusu malipo yao, na kwa maoni yangu mimi, wale viongozi hata kama hawataondolewa basi watakua wamejifunza kitu kupitia moto walipata safari hii.
Kuna watu hawatabaki salama. Tusubiri
 
Hajaokoa chochote bali anajaribu kuingilia masuala ambayo hayamuhusu kama serikali.
Kaingia kutuliza gasia tu, maana Tff walishafeli njia pekee ya kuokoa mpira uchezwe ilikuwa hii!.
 
Shida si mchezo kusogezwa mbele. Yanga walikuwa wanataka bodi ya ligi ijiuzulu lakini inavyoonekana wametepeta na wala malalamiko yao yametupiliwa mbali.

Ameenda mmiliki wa 🐸🐸 mwenyewe, hersi kachochora.
Point za mezani hazipo Tena ndugu,,kuhusu kujiuzulu kwa viongozi wa bodi ambalo ndio lilikuwa sharti la yanga subilia kuanzia wiki ijayo utapata majibu ya swali lako
 
Hili suala lazima litamchomoa tu karia kwenye uchaguzi wa August
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…