Mechi ya Yanga dhidi ya Simba, June 25 kuchezeshwa na Waamuzi kutoka Misri

Mechi ya Yanga dhidi ya Simba, June 25 kuchezeshwa na Waamuzi kutoka Misri

Bado watakosolewa kuwa wanatoka Misri,
ingefaa watoke nchi tofauti ikiwa Mmoja anaongea Kiarabu, Kireno, Kizulu na Kifaransa yaaani iwe ngumu kuwasiliana na kupewa bahasha na wenyeji...
Derby ya Misri wanawakataa waamuzi wenzao wa Misri, sisi derby yetu tunawakataa wa kwetu tunaenda kuwachukua wa Misri wanaokataliwa na wenzao.
Mechi hii ndio ina mvuto zaidi kwakua atakayeshinda bingwa, wakitoka droo mmojawapo bingwa ,kwahiyo mvuto wa mechi hii ni mkubwa zaidi kuliko kama ingechezwa tarehe 08/03 au tarehe 15/05
Mpira una kanuni zake na hauwezi kuendeshwa na maamuzi ya kisiasa yanayofanywa na watu wenye malengo ya kisiasa. Leo wamevuruga ratiba wakaamua tarehe ya mechi, kesho wakiamka wakasema timu fulani ikishinda ndiyo itakuwa na mvuto itakuwaje?
 
Derby ya Misri wanawakataa waamuzi wenzao wa Misri, sisi derby yetu tunawakataa wa kwetu tunaenda kuwachukua wa Misri wanaokataliwa na wenzao.

Mpira una kanuni zake na hauwezi kuendeshwa na maamuzi ya kisiasa yanayofanywa na watu wenye malengo ya kisiasa. Leo wamevuruga ratiba wakaamua tarehe ya mechi, kesho wakiamka wakasema timu fulani ikishinda ndiyo itakuwa na mvuto itakuwaje?
Mleteni huyo Mpanzu wenu
 
Kwa pressure iliyopo hamna namna, kuepusha mlolongo mbeleni inabidi , timu zote zina mvutano mkubwa mno

Kupata marefu neutral ambao hawana mfungamano ni moja ya suluhisho. Ikiwezekana

Kwa pressure iliyopo hamna namna, kuepusha mlolongo mbeleni inabidi , timu zote zina mvutano mkubwa mno

Kupata marefu neutral ambao hawana mfungamano ni moja ya suluhisho. Ikiwezekana mechi ichezewe hata nchi nyingine kabisa
Hii ni nzuri, pia kama itawezekana ikifika octoba kwenye uchaguzi tuazime tume ya uchaguzi ya kenya waje wasimamie uchaguzi ili kuondoa sintofaham.
 
Waamuzi wa mchezo wa dabi itayofanyika tarehe 25 watangazwa na wote wametokea nje ya nchi uku muamuzi wa kati akiwa kutokea nchini Misri. Orodha yao iyo chini.
Nafikiri hii itakuwa mwanzo mzuri wa kupata fair match isiyokuwa na makosa
Atakaefungwa atalalamikia marefa tu.
 
Hii ni aibu kwa taifa, Mechi ya ndani kuchezeshwa na marefa wa nje, inapeleka ujumbe gani kwa marefa wa Kitanzania?
Haiwezi kuwa aibu. Tena TFF msimu ujao watoe ajira kwa waamuzi kutoka mataifa mengine waje wachezesha hata nusu ya me za ligi.

Hii itasaidia sana kukuza ligi yetu na waamuzi wa ndani.

Kama tuna makocha na wachezani wa kigeni, haina shida pia kuwapa nafasi waamuzi wa nje.

Hii italazimisha watu wenye weledi kuingia kwenye uamuzi na kujifunza lugha pia ili iwe rahisi kupata hata international games.

Hongereni TFF lwa hili, liongezeni ktk msimu ujao wa ligi.
 
Ni Derby hii tu itachezeshwa na marefa kutoka nje ama hata zijazo? Na hizo zijazo hawa marefa wa ndani wakiwagomea mtawalaumu? Kwasababu mmesha set precedence.
Sasa unagomea kazi. Si unasugua benchi tu.
 
Sie kila kitu hatuwezi hata kuchezeshe mechi kwa haki kweli?
Tupo tunawatambia mabeberu kuwa sisi ni nchi huru hatutaki kuingiliwa mambo yetu halafu tunashindwa kuendesha wenyewe kampuni ya daladala au kuchezesha kwa haki kamchezo ka mpira wa miguu tunaishia kuwapa wageni watuendeshee.
 
Hivi kwani si tulikubaliana refa atakuwa arajiga ambaye hana upendeleo kwa timu yoyote
Sasa nyinyi si hamumtaki! Na badala yake mnamtaka Tatu Malogo au Kepha Kayombo! Sasa safari hii ni ubaya ubwela.
 
Sasa nyinyi si hamumtaki! Na badala yake mnamtaka Tatu Malogo au Kepha Kayombo! Sasa safari hii ni ubaya ubwela.
Wapi simba wamesema hawamtaki kwani simba ndio wanajipangia marefa, kama alichezesha mechi dhidi ya singida na wakakubaliana na matokeo, ndio ashindwe kuchezesha mechi dhidi ya yanga au ninyi mlitaka refa awe nani
 
Mchezo wa Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga SC na Simba SC utachezeshwa na waamuzi kutoka nchini Misri.

Mwamuzi wa kati atakuwa Amin Mohamed Amin Omar, msaidizi namba moja ni Mahmoud Ahmed Abo El Regal, huku msaidizi namba mbili akiwa Samir Gamal Saad Mohamed.

Dabi ya Kariakoo kati ya Yanga SC na Simba SC imeahirishwa mara mbili, kwani mchezo huo uliopangwa kufanyika Machi 8, 2025 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, na kuahirishwa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB).

Soma: POSTPONED (PP): Yanga SC VS Simba SC | Ligi Kuu NBC | Benjamin Mkapa Stadium | 08.03.2025

Mechi hiyo ikapangiwa tena kuchezwa tarehe Juni 15, 2025, ikiwa ni mabadiliko ya kwanza ya tarehe tangu kupangwa kwake awali.

Taarifa ya Bodi ya Ligi kuu yaahirisha Mechi ya Derby kati ya Yanga dhidi ya Simba

Baada ya mvutano kuendelea kuhusu Dabi ya Kariakoo, Rais Samia, alikutana na viongozi wa timu ya Simba na Yanga kwa mazungumzo maalum yaliyofanyika Ikulu Chamwino, mkoani Dodoma.

Soma: Rais Samia akutana na Viongozi wa Simba na Yanga Ikulu, leo Juni 13, 2025

Mara baada ya kikao hicho, ratiba mpya ya mchezo huo ilipangwa rasmi, ambapo Dabi hiyo inayosubiriwa kwa hamu imepangiwa kuchezwa Jumatano, tarehe 25 Juni 2025.

Kina Arajiga na Kayoko mnawakwepa.
 
Derby ya Misri wanawakataa waamuzi wenzao wa Misri, sisi derby yetu tunawakataa wa kwetu tunaenda kuwachukua wa Misri wanaokataliwa na wenzao.

Mpira una kanuni zake na hauwezi kuendeshwa na maamuzi ya kisiasa yanayofanywa na watu wenye malengo ya kisiasa. Leo wamevuruga ratiba wakaamua tarehe ya mechi, kesho wakiamka wakasema timu fulani ikishinda ndiyo itakuwa na mvuto itakuwaje?
Mimi sijajua mnaolalamikia huu uamuzi wa marefa kutoka nje ni mashabiki wa timu gani na mnataka refa awe nani, wamisri kuwakataa marefa wao si kwamba hawajui kuchezesha ila ni ile kufungamana na timu moja kwahiyo wanataka marefa neutral, sisi kuwaita marefa kutoka misri maana yake na sisi tunategemea watakuwa neutral hawatafungamana na timu yoyote huku, hata sisi marefa wetu si kwamba hawajui kuchezesha ila shida ndio hiyo ya kupendelea timu moja hasa timu kubwa ila mechi zingine mbona wanachezesha vizuri tu, halafu hao wamisri si mechi zote wanaita marefa toka nje maana wanadai ni gharama mara nyingi ni mechi za derby ya al ahly na zamalek na timu nyingine kubwa kama pyramids
 
Wapi simba wamesema hawamtaki kwani simba ndio wanajipangia marefa, kama alichezesha mechi dhidi ya singida na wakakubaliana na matokeo, ndio ashindwe kuchezesha mechi dhidi ya yanga au ninyi mlitaka refa awe nani
Sisi hata Kepha Kayombo akichezesha sawa tu. Ila akizingua, tutamdunda kama yule mwenzake Israel Nkongo.
 
Back
Top Bottom