Kuna kitu hapa nimekichunguza nikahisi, naona Rais na serikali yake kwa namna fulani kama wanataka kuzima tetesi zizazozagaa kwenye mitandao halafu baadae huwa kweli, ni kama wanajaribu kurudisha imani ya wananchi kwa serikali yao (siri).
Sasa nahisi wameona wasome upepo kwenye mitandao wakiona watu wanaaminishwa jambo fulani (baada ya taarifa kuvuja) wao waje tofauti ili kuwapunguzia wenye ushawishi mitandaoni (twitter in particular) waonekane waropokaji na wazandiki.
Japo inawezekana kweli mpango ulikuwa ni kuongeza mishahara ndio maana mpaka kina Mhagama walikuwa wanajua hilo, inawezekana mchezo umebadilishwa ghafla hata hao kina Mhagama hawakuwa na habari.