Meja Jenerali Charles Mbuge astaafu utumishi wake jeshini

Sasa hapo Tanzania mtu akitaka kukutwanga mvua ya mabomu hao wanajeshi wasio hata na air force ya kueleweka wanazuiaje?
Umeanza kwa kudhihaki mstaafu kutumia miaka 35 jeshini bila kwenda vitani. Nimekujibu kazi kubwa ya jeshi ni kuepusha vita through deterrence. Hauamui tu upigane vita ili uonekane una Airforce au Navy au Army nzuri, unapigana ukilazimika tu.

Kama deterrence haifanyi kazi vita ungeona haijalishi kuna Airforce ya maana au hakuna. Israel ina Airforce kubwa yet inakuwa vitani mara kwa mara. China ina Airforce kubwa na haijaenda vitani miaka zaidi ya 50.
Usichanganye Africa kutokuwa na vita kwa sababu kila mtu anapambana na umasikini wake na ufanisi wa wanajeshi wetu.
Afrika ndio bara lenye vita zaidi sasa sijui idea ya kusema hakuna vita kisa umaskini unaitoa wapi.

Sudan, Ethiopia, Somalia, Libya, DRC zina vita ya miaka. Uko Western Africa kuna vita active dhidi ya ugaidi kwa Chad, Niger, na Mali.
Vita ni biashara yenye gharama kubwa ambayo nchi nyingi masikini za Africa haziwezi ku afford.
China ni nchi ya pili kiuchumi duniani na haina vita wala haijashiriki kwa miaka zaidi ya 50.
Switzerland mara ya mwisho kushiriki vita ni 1847 hadi leo wakati silaha za kisasa wanazo na wanatengeneza na kuuza.

Nchi maskini kama Myanmar na Congo DR zimepigana miaka nenda rudi na zina njaa.
 
Rest in peace Mbuge Mwendo umeumaliza utakumbukwa kwa mema uliyotrnda enzi za uhai wako
 

Ma Jenerali wengi bila vita ni u jenerali wa mchezo tu. Nchi yenyewe uchumi mdogo, ma jenerali wengi wa nini?

Unatetea vipi wingi wa Ma Jenerali katika nchi masikini ambayo hata haiweki wazi military spending yake?

Deterrence una m deter nani (nation state) anataka kupigana vita na Tanzania sasa?

Mkuu wa majeshi kalalamika watu wasio Watanzania wameshika nafasi nyeti serikalini, maana yake wanausalama na wanajeshi wameshindwa kulinda nafasi za serikalini zisishikwe na watu wasioeleweka, let alone ku deter vita.


Unahakikishaje hatupigani vuta kwa sababu ya deterence na si kwa sababu hakuna anayetaka kupigana vita na sisi tu?
 
Watu hawafahamu kazi za Jeshi.
 
Shortly, kama unataka kujua kazi za hao Ma Gen, na kama unataka kuona Vita, watoe kwenye nafasi zao! lakin zaidi! freez Jeshi lisifanye kazi.

Asante.
 
Kiranga, naamini katika dialogue na mantiki, lakini kwenye hili la Jeshi
,naona liko juu sana ya uwezo au mawanda yako. (Your Play ground).

Unaonekana huna ufaham sahihi kuhusu masuala mbali mbali ya kijeshi

Ni busara kukaa kimya pia.
 
Shortly, kama unataka kujua kazi za hao Ma Gen, na kama unataka kuona Vita, watoe kwenye nafasi zao! lakin zaidi! freez Jeshi lisifanye kazi.

Asante.
Hakuna kazi jeshi inafanya zaidi ya kushiriki missions za kimataifa na ku deal na vi Al-Shabab vya hapa na pale.

Kitu ambacho hakihitaji gunia la ma Jemerali.

Kama mnabisha, nyie ndiyo mnatakiwa kuwa transparent kuonesha ma Jenerali wengi hivyo wanafanya kazi gani.

Ama sivyo unaweza kuwa unatetea jeshi kubwa lisilo na kazi yoyote ya maana.
 
Kiranga, naamini katika dialogue na mantiki, lakini kwenye hili la Jeshi
,naoba liko juu sana ya uwezo au mawanda yako. (Your Play ground).

Unaonekana huna ufaham sahihi kuhusu masuala mbali mbali ya kijeshi

Ni busara kukaa kimya pia.
Wewe una ufahamu gani kuhusu mambo ya jeshi katika nchi ambayo kila kitu kuhusu jeshi ni siri?
 
Huna uelewa na kazii za Jeshi!
 
Halafa machawa wa UVCCM walimkula huyu mzee milioni kama 500 hivi ili mtoto wake ashinde kura za maini kupitia UVCCM matokeo bint yake akaambulia kupata kura moja, mzee alipoata matokeo aliwatolea bastora wale vijana, almanusura awamwage ubongo
 
Halafa machawa wa UVCCM walimkula huyu mzee milioni kama 500 hivi ili mtoto wake ashinde kura za maini kupitia UVCCM matokeo bint yake akaambulia kupata kura moja, mzee alipoata matokeo aliwatolea bastora wale vijana, almanusura awamwage ubongo
Za kustaafu au alipiga na yeye?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…