Meli 13 zinahudumiwa muda huu bandari ya DSM Januari 28/2024

Meli 13 zinahudumiwa muda huu bandari ya DSM Januari 28/2024

Hizi hapa dondoo 15 muhimu za kuzingatia dhidi ya propaganda hasi kwa bandari ya DSMView attachment 2886233

1. Magati yote 12 pamoja na maeneo ya kuhudumia shehena za mafuta yanahudumia meli hadi kufikia muda huu wa leo tarehe 28 Januari 2024, tofauti na wapotoshaji wanaoposha kwa makusudi kuwa ni magati mawili (2) tu ndio yanayofanya kazi kati ya magati 12 yaliyopo.

2. Taarifa zinaonesha ukweli halisi watu wakichapa kazi katika magati yote 12 na kuongeza ufanisi. Kwa mfano, Gati namba Sifuri (0) ambalo ni mahsusi kwa kushusha shehena ya magari nalo linahudumia meli MV Yangze 32 ya mizigo mchanganyiko.

3. Idadi na wingi wa meli bandarini unabadilika ukiona leo foleni meli 20 na keshokutwa ukaona meli 20 haina maana ni zilezile maana yake kuna meli zimehudumiwa na nyingine zimekuja kutaka kuhudumiwa.

4. Ni sawa na shuleni mtu anaweza kuhoji mbona kila mwaka shule zinakuwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne. Maana yake ni kuwa kadri wengine wanavyomaliza shule ndivyo wengine wanaanza shule, wa kidato cha nne akimaliza wa kidato cha tatu anapanda cha nne, wa cha pili anapanda cha tatu, wa cha kwanza anapanda cha pili na aliyemaliza shule ya msingi anapanda cha kwanza ni mzunguko. Ndivyo mzunguko wa meli unavyokuwa

5. Mara kadhaa TPA wametufafanulia kuwa meli kuongezeka ni neema sio laana. Tumshukuru Mungu kila meli zinapoongezeka maana yake ajira zinaongezeka, mapato yanaongezeka, makusanyo yanaongezeka na mzunguko unaongezeka.

6. Ni rahisi kusema kuwa meli zinakimbia bandari ya Dar zinakimbilia Mombasa lakini kiuhalisia huu ni uongo na hautekelezeki.View attachment 2886235

7. Tabia za kibiashara za bandari ya Dar zinaifanya iwe ya kipekee kwa wenye meli kwa kuwa wana uhakika wa kupata mzigo wa kurudi unaotokana na exportation ya nchi jirani hasa madini tofauti na Mombasa ambayo haina mzigo wa kurudi.

8. Haiingii akilini pia kusema mteja wa mzigo kutoka Lusaka Zambia akashushe mzigo wake Mombasa kisha autembeze kutoka Kenya-Tanzania-Zambia wakati anao uwezo wa kutumia Bandari ya Dar moja kwa moja.

9. Kuna tofauti kubwa sana kati ya ongezeko la meli bandarini na ufanisi kupungua (Ongezeko la meli ni kielelezo cha kukua kwa biashara, hata wenye mashule wanapenda wanafunzi waongezeke). Ni muhimu kufahamu kuwa, ufanisi wa Bandari ya Dar ni moja kati ya vivutio vya ujio wa meli nyingi. Kupungua kwa ufanisi kungepimwa na kushuka kwa mapato, kuongezeka kwa muda wa kupakua na kupakia meli. Lakini badala yake mapato yamepanda na muda wa kupakua na kupakia meli umezidi kupungua-Wanastahili pongezi kwenye hili.

10. Ni makosa makubwa sana kuilinginanisha bandari ya Dar na ya Mombasa kiufanisi, uwekezaji na kimuundo

11. Kimuundo Bandari ya Dar ina jumla ya magati 12 na maeneo makuu mawili ya kuhudumia shehena ya mafuta. Bandari ya Mombasa ina magati 22 tofauti yake bandari ya Dar ni nusu ya Bandari ya Mombasa kiukubwa.

12. Kiufanisi bandari ya Dar inapaswa kuhudumia mzigo nusu ya bandari ya Mombasa lakini mwaka Jana Mombasa yenye magati 22 wamehudumia tani takribani milioni 28 huku Bandari ya DSM yenye magati 12 ikahudumia tani milioni 22. Kihesabu ilipaswa kuzidiwa tani milioni 12.

13. Kiutendaji bandari ya DSM inaikimbiza sana bandari ya Mombasa ukilinganisha miondombinu na vifaa walivyonavyo.

14. Sio kweli kwamba Bandari ya Mombasa haijazidiwa na meli, pamoja na kuwa na magati mara mbili ya bandari ya DSM lakini nayo imekiri kuongezeka kwa meli na kwamba wateja wake wawe na subira katika upakuaji mizigo.

15. Kila tunaposikia matangazo ya mapato ya makusanyo kutoka .mamlaka ya Mapato nchini TRA tufahamu kwamba wastani wa asilimia 40 ya makusanyo hayo yanatokana na ushuru wa forodha unaotokana na bandari ya DSM.
Hongereni bandari ya Dar
 
Jifunze kwanza kuandika alafu acha matumizi ya bhangi
Wazazi wangu walinifunza kuheshimu kila mtu na nashukuru kwa lugha uliyoitumia maana hunijui lakini umenihukumu na hicho ulichokisema Mungu akubariki sana
 
Nina mizigo yangu imekwama hapo tokea tarehe 11 ndo melinilifika jana ndo nmepata taarifa kua leo ndo wanaanza kushusha nahisi kuna tatizo bandarin haikua ivo kipindi cha nyuma
Ni jambo la kweli kuna sehemeu wanapashwa kuparekebisha ili twende sawa kunabaadhi ya vitu lazima tukubali vikiwa havipo sawa vifanyiwe marekebisho na mambo yakawa sawa kwa kila upande.
 
Wazazi wangu walinifunza kuheshimu kila mtu na nashukuru kwa lugha uliyoitumia maana hunijui lakini umenihukumu na hicho ulichokisema Mungu akubariki sana
Sasa kama siyo bhangi nini? Wewe upo Kiteto sijui Nyakabazu huko alafu unasema mzigo wako umechelewa bandarini, kweli?
 
Ni jambo la kweli kuna sehemeu wanapashwa kuparekebisha ili twende sawa kunabaadhi ya vitu lazima tukubali vikiwa havipo sawa vifanyiwe marekebisho na mambo yakawa sawa kwa kila upande.
Kitu gani unataka kirekebishwe kama kweli wewe ni mtumiajia wa bandari ya Dar? Acha kuandika porojo ushashiba viazi na katecno kako basi unaporojoka tu
 
Nimesoma kipeperushi chako cha kufungia vitumbua, kwanza kimepitwa na wakati, ndio maana nasisitiza wewe ni kanjanja
Wewe hata elimu huna. Full MEMKWA eti na wewe unachangia mada za kisomi. Toa counter argument na siyo blank statements za kuita vipeperushi
 
Kitu gani unataka kirekebishwe kama kweli wewe ni mtumiajia wa bandari ya Dar? Acha kuandika porojo ushashiba viazi na katecno kako basi unaporojoka tu
Wewe ndiye mvuta bangi na unavuta bangi chooni baada ya kula makande. Kwanini watu wenye heshima zao ambao wanatoa argument yenye kuleta tija kwa bandari yetu halafu wewe unakuja hapa unaandika hovyo kama bata anaye hara
 
Wewe hata elimu huna. Full MEMKWA eti na wewe unachangia mada za kisomi. Toa counter argument na siyo blank statements za kuita vipeperushi
Sikia wewe kanjanja, acha kutuwekea toilet paper zilizopitwa na wakati, weka vitu kama wenzako taarifa za kisasa na za uhakika kutoka gazeti lenye sifa zake mjini. Umeelewa we kanjanja
 
Wewe ndiye mvuta bangi na unavuta bangi chooni baada ya kula makande. Kwanini watu wenye heshima zao ambao wanatoa argument yenye kuleta tija kwa bandari yetu halafu wewe unakuja hapa unaandika hovyo kama bata anaye hara

Wewe ndiye mvuta bangi na unavuta bangi chooni baada ya kula makande. Kwanini watu wenye heshima zao ambao wanatoa argument yenye kuleta tija kwa bandari yetu halafu wewe unakuja hapa unaandika hovyo kama bata anaye hara
Nakuheshimu acha kabisa kuingilia yasiyokuhusu
 
Hatuwezi kuacha ujinga ukapita bila kuwa checked, irrespective the fact that siyo mimi uliiye ni address
Atakuwa anasubiri ubuyu kutoka Zanzibar siyo mizigo ya bandari ya Dar, wanaosubiri mizigo hawaendi bandarini kusubiria wapo kwenye maofisi yao huko
 
Nasasa navyo andika hivi nipo hapa hap Bandarini tuseme ukweli kuna vitu haviko sawa tusifiche na wakubali ushauri wawateja ndugu yangu tukipende hichi chetu na tukitetee kiwe bora zaidi ili tuwarithishe vizazi vijavyo kilicho bora.
Utakuwa unasubiri ubuyu kutoka Zanzibar
 
Wewe ndiye mvuta bangi na unavuta bangi chooni baada ya kula makande. Kwanini watu wenye heshima zao ambao wanatoa argument yenye kuleta tija kwa bandari yetu halafu wewe unakuja hapa unaandika hovyo kama bata anaye hara
argument yenye kuleta tija ni kusema kuwa yupo bandarini anasubiri mzigo wake?? Imekuwa stendi ya Shabiby??? Acha ukanjanja
 
DP world at work! Hapo wanaofaidika ni waarabu, kwann unaleta taarifa hii kwa watanzania? Watumie waarabu wafurahie?1
Taarifa yenyewe uongo mtupu,kuna meli zimefika toka tarehe 11/01 mpaka leo mizigo haijatoka bandarini, bidhaa madukani inazidi kupanda.Ukiuliza unaambiwa kuna mabadiriko ya uongozi.
 
Nasasa navyo andika hivi nipo hapa hap Bandarini tuseme ukweli kuna vitu haviko sawa tusifiche na wakubali ushauri wawateja ndugu yangu tukipende hichi chetu na tukitetee kiwe bora zaidi ili tuwarithishe vizazi vijavyo kilicho bora.
Kila kitu kipo sawa, labda upande wako wewe ndio hauko sawa kwanza mizigo hatusubiri bandarini ndio maana kuna makampuni ya Clearing & Forwarding.
 
Taarifa yenyewe uongo mtupu,kuna meli zimefika toka tarehe 11/01 mpaka leo mizigo haijatoka bandarini, bidhaa madukani inazidi kupanda.Ukiuliza unaambiwa kuna mabadiriko ya uongozi.

Back
Top Bottom