Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Sekta ya utalii Tanzania tumepata bahati ya meli hii lakini nafasi hatutumii vizuri.Kwa namna hiyo meli inavyo zunguka nchi nyingi duniani ni nafasi nzuri kwa sekta ya utalii nchini kufanya jambo kuhakikisha kila sehemu hiyo meli inako nanga wanajua kuhusu utalii wa Tanzania
Bei zipo tofauti kwa kila kitabu mkuu
WamelalaKwa namna hiyo meli inavyo zunguka nchi nyingi duniani ni nafasi nzuri kwa sekta ya utalii nchini kufanya jambo kuhakikisha kila sehemu hiyo meli inako nanga wanajua kuhusu utalii wa Tanzania
Tupe ratiba mkuu ni kuanzia saa ngapi hadi saa ngapi!?
Iliwahi kuja enzi za magu?Mv Logos Hope ni meli ya vitabu yenye library kubwa yenye vitabu mbalimbali inayozunguka kwenye mataifa na bandari mbalimbali duniani.
View attachment 2774301
Meli hii ya kihistoria ilijengwa mwaka 1973 huko Randsburg, kaskazini mwa Ujerumani kisha ikapita mikononi mwa kampuni tofauti mpaka 2004 ilipochukuliwa na GBA Ship na kufanyiwa marekebisho na kuwekewa library ya vitabu, mwaka 2005 ikaanza kuzunguka bandari tofauti Duniani.
View attachment 2774298View attachment 2774299
Meli hii ina urefu wa mita 132.50,upana 21.06 wafanyakazi 442 na imesajiliwa Nchini Malta. Wastani hutembelea nchi 70 na bandari zipatazo 140 duniani kote.
Mara ya mwisho meli hii ilikuja Tanzania 25/01/2016 na kuondoka tarehe 18/02/2016. Mwaka huu tena Tanzania imepata Bahati ya kutembelewa na meli hii imeingia tarehe 05/10/2023 na itakuwa Nchini kwa wiki 2, mpaka tarehe 22/10/2023.
Hii ni fursa kwa sekta ya utalii,elimu na wadau mbalimbali kwenda kutembelea na kujifunza kiingilio ni Shilingi 1000 ya Kitanzania.Tiketi za kuingilia melini zinapatikana geti namba 2 la Bandari ya Dar es Saalam njia ya Kituo kikuu cha Central Police au Stesheni kwa wageni.
View attachment 2774293
Picha baadhi za sehemu za ndani za meli ya Logos Hope.Wenye familia,watoto,mashule kuna vitabu sehemu za kupiga picha,ice cream,kahawa na kumbi za kuonyesha matamasha ya watu mataifa mbalimbali.
View attachment 2774296
Ratiba ya kutembelea siku ya Jumatatu kuna mapumziko. Hivyo ni kuanzia Jumanne mpaka Jumapili.
Nataka nikumbukie enzi zangu ndugu yangu 🤣 nishamisi madude magumu magumu kichwani mwangu.Mzee baba unataka urushe chombo sayari ya Mars
Nipo hapa melini kweli watanzania tumelala kila Sekta, wanakuja watu wa nchi mbalimbali, kutoka ubalozini na watanzania wengine wanakosa Cash kulipa vitu.Wamelala
Bongo tupo nyuma saana kaka.Nipo hapa melini kweli watanzania tumelala kila Sekta, wanakuja watu wa nchi mbalimbali, kutoka ubalozini na watanzania wengine wanakosa Cash kulipa vitu.
Vodacom ndio wapo nao wameweka huduma ya kulipa. Kuna watu wanataka Cash wanakosa mpaka watoke nje. Meli wana kubali Credit Card. Hakuna taasisi ya kifedha ilikuja kuweka hata tent kutoa huduma na meli itakuwa nchini week 2.