Mv Logos Hope ni meli ya vitabu yenye library kubwa yenye vitabu mbalimbali inayozunguka kwenye mataifa na bandari mbalimbali duniani.
View attachment 2774301
Meli hii ya kihistoria ilijengwa mwaka 1973 huko Randsburg, kaskazini mwa Ujerumani kisha ikapita mikononi mwa kampuni tofauti mpaka 2004 ilipochukuliwa na GBA Ship na kufanyiwa marekebisho na kuwekewa library ya vitabu, mwaka 2005 ikaanza kuzunguka bandari tofauti Duniani.
View attachment 2774298View attachment 2774299
Meli hii ina urefu wa mita 132.50,upana 21.06 wafanyakazi 442 na imesajiliwa Nchini Malta. Wastani hutembelea nchi 70 na bandari zipatazo 140 duniani kote.
Mara ya mwisho meli hii ilikuja Tanzania 25/01/2016 na kuondoka tarehe 18/02/2016. Mwaka huu tena Tanzania imepata Bahati ya kutembelewa na meli hii imeingia tarehe 05/10/2023 na itakuwa Nchini kwa wiki 2, mpaka tarehe 22/10/2023.
Hii ni fursa kwa sekta ya utalii,elimu na wadau mbalimbali kwenda kutembelea na kujifunza kiingilio ni Shilingi 1000 ya Kitanzania.Tiketi za kuingilia melini zinapatikana geti namba 2 la Bandari ya Dar es Saalam njia ya Kituo kikuu cha Central Police au Stesheni kwa wageni.
View attachment 2774293
Picha baadhi za sehemu za ndani za meli ya Logos Hope.Wenye familia,watoto,mashule kuna vitabu sehemu za kupiga picha,ice cream,kahawa na kumbi za kuonyesha matamasha ya watu mataifa mbalimbali.
View attachment 2774296
Ratiba ya kutembelea siku ya Jumatatu kuna mapumziko. Hivyo ni kuanzia Jumanne mpaka Jumapili.