Meli ya Vitabu Bandari ya Dar es Salaam "Mv Logos Hope" yaingia tena baada ya miaka 7

Nafikiri waandishi wetu wameshajua taarifa kama hizi za meli ya vitabu hazina amsha amsha kwa Wabongo wengi.
Vyombo vya habari havijatoa nafasi ya kutangaza sana ujio wa meli hii. Wamezoea kutangaza meli zile kubwa mfano meli ndefu au meli zenye gari nyingi ziingiapo Nchini.
 
Ni elfu 1 kaka, vitabu vipo vya kila aina, sehemu za kupiga picha za mandhari tofauti. Ice cream kuanzia elfu 1.

Walete watoto wacheze na wenzao wakina Patel na Charan maana leo ndio wamejaa
Akina Patel na Charan!

Kwa hiyo akina baba Masanaja na akina mama Bahati hawajui umuhimu wa kuwapeleka watoto wao "dukani?"
 
Ni duka la vitabu, sio maktaba. Kwa mujibu wa hilo tangazo hapo juu. Sasa sijui wewe ni mwandishi wa habari au raia tu wa kawaida unajiandikia tu kihole holela kama hukusoma
Punguza stress mazee...ukisoma ndio unaandika Hukusoma?
 
Kwanini wasiviupload kwenye mtandao halafu waipaki kwao tu
 
Sisi watu weusi kwenye vitabu hatuna muamko sana. Hata kujenga tamaduni kwa watoto wasome vitabu
Mkuu, nahisi ukisema mtu mweusi, unaweza ukawa unakosea. Pamoja na kuwa usomaji vitabu si tabia iliyozoeleka Tanzania, kuna baadhi ya Watanzania wanaopenda kusoma vitabu, mimi nikiwemo.

Nafikiri, ningelikuwepo Dar Es Salaam, nisingekosa kwenda na familia yangu.

Hivi lakini, hakuna kinachoweza kufanyika ili kuwaibua watu wengi zaidi Tanzania wanaopenda kusoma vitabu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…