Ifuatayo ni miradi mikubwa iliyojengwa na wakoloni:-
1. Ujenzi wa Bandari ya DSM
2. Ujenzi wa Bandari ya Tanga
3. Ujenzi wa Bandari ya Mtwara
4. Ujenzi wa uwanja wa ndege wa DSM
5. Ujenzi wa uwanja wa Bandari ya Pemba
6. Ujenzi wa Ikulu ya DSM
7. Ujenzi wa Dsm College (Baadae ikaboreshwa na kuwa UDSM baada ya uhuru)
8. Ujenzi wa Bandari ya Zanzibar
9. Ujenzi wa reli ya kati, Dar-Tabora-Mwanza, Tabora -Kigoma
10. Ujenzi wa mji wa Tanga + Master Plan
11. Ujenzi wa Jiji la DSM + master plan yake
12. Ujenzi wa Bandari ya Mwanza
13. Ujenzi wa bandari ya Bukoba na Musoma
14. Ujenzi wa Bandari ya Mbamba Bay
15. Ujenzi wa Bandari ya Ujiji Kigoma
16. Uundaji wa meli ya MV. Liemba (Ziwa Tanganyika)
17. Uunzi wa meli ya MV. Victoria (Ziwa Victoria)
18. Ujenzi wa shule za Sekondari za kale, mfano Mzumbe, Ilboru, Tanga Tech, Moshi Tech, Mazengo, Mtwara Tech, Tabora Boys+Girls, Pugu, Kibaha, Minaki, Bwiru boys & Girls, Msalato, Ifunda, Iyunga, Mkwawa, Nganza, Tosamaganga, Kilakara, nk
19. Ujenzi wa Ikulu ya Z'bar
20. Ujenzi wa majengo mengi ya Wizara za serikali, vituo vya polisi, magereza na Mahakama.
21. Ujenzi wa shule za msingi za serikali na za Seminari
22. Ujenzi wa makanisa, mf. St. Joseph na Azania Front (Posta Dar) na Misikiti kwa upande wa Z'bar
23. Ujenzi wa hospitali kubwa, mf. Muhimbili
24. Ujenzi wa mabwawa ya kuzalisha umeme mf. Hale + Nyumba ya Mungu.
25. Ujenzi wa vyuo vikuu vya kati, mfano Dar Tech, Arusha Tech, vyuo vya Ualimu, Kilimo, nk
26. Ujenzi wa reli ya Tanga
27. Ujenzi wa gridi ya kwanza ya Taifa ya umeme
28. Uanzishaji wa mashirika ya umma mfano Posta na simu pamoja na Benki yake
29. Ujenzi wa Uwanja wa Taifa, jijini Dar (Leo Shamba la Bibi)
30. Ujenzi wa vivuko, mfano Kigamboni na Posta jijini Dar
31. Na kadhalika na kadhalika.
Lakini pamoja na yoooote hayo, miradi hiyo yooote, Bado wazee wetu wakiongozwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, walisimama mbele ya kadamnasi na kuwaambia wananchi kuwa hao watu (wakoloni) hawafai, waondoke watupishe. Na kweli wakapisha rasmi Desemba mwaka 1961.
Sasa mwaka huu 2020, mimi ni nani hata nisimpinge ccm kwenye uchaguzi huu, pale anapotumia miradi ya maendeleo kadhaa iliyojengwa na serikali anayoiongoza, kama kigezo cha yeye kutaka kuchaguliwa tena na kubakia madarakani?
Tafakari...!!!.