Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea



Kaka Pascal, ebu pitia ujumbe wangu hapa nimeuliza matumizi ya sisi, tumehuru, kuwauliza viongozi na etc, the political pig with vuvuzela has unfolded a number of issues.
 
Mpo na dikteta mnaona mambo yalivyo mabaya na huyo mtu mkimwachia awamu ya pili mtateseka zaidi.
 

Kazungumza kwa namna yenye harufu ya uhaini na uasi, inahitaji akili za kawaida tu kuliona hili.
 
Kama ni kweli basi Membe atakuwa amejipanga kisawasawa.
Kama form inatolewa na mtu mmoja Bashiru, basi itakuwa ngumu.
Na akikataliwa ATAKINUKISHA.Hoja yake ikipata mtu wa kuipigia upatu katika NEC ni wazi kutatokea mtafaruko heavy.Na kama hawatamtuliza Membe basi CCM inaweza ikagawanyika vipande vitatu.
 
Huo urais aende akagombee chadema au ACT lakini sio CCM na haita kuja itokee membe awe rais wa tanzania ,hana vigezo wala hata nusu ya kumfikia Dr. Magufuli hakuna wa kumpinga magufuli ndani ya CCM. Over.
Yaani mwenye uwezo wa kuongoza CCM ni Magufuli tu?
 
Huko CCM hakuna demokrasia tena?
 
huyu ndiye mwanaume sasa!!!! ccm wakijiloga kumpitisha tu.... meko bye bye na hata akigombea chama kingine membe anashinda uchaguzi
 
Ni mfumo bibie, CCM ina mizizi, Membe mwenyewe kanywa maji ya chama anajua nguvu zake
Basi mruhusu demokrasia achukue fomu ili akajipime na Mtukufu na KUNOGESHA uchaguzi, shida ni nini wana CCM wenzangu?
 
Membe ametoa dira,ni wazi kuwa kamati kuu wanamuogopa membe maana hawajui aki na nani wapo nyuma ya Membe,hivyo kwa kugombea ndani ya CCM akitegemea kuwa CC ya CCM itatengua ni ndoto.
Membe katoa option,kuwa chochote kinaweza kutokea kati ya juni na Oktoba.

Lkn jambo la msingi na muhimu kabla ya yote ni tume huru ya uchaguzi na waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa.

Hapo ndio kuna point,Membe anaungana na Askofu Bagonza kudai tume huru ya uchaguzi.

Tume huru itaweka usawa kwa vyama vyote na kwakuwa CCM wamefanya makubwa chini ya Rais Magufuli ni wazi kuwa hawataogopa uwepo wa Tume huru ya uchaguzi.

Sitegemei mpaka maandamano ndio tume huru iwekwe,CCM ni chama kikubwa naamini kitaviongoza vyama vingine kudai tume huru
 
Membe anafaa.

2020 Twende na Membe.

Kitendo cha kutetea tume huru ya uchaguzi iliyofair kwa wote ameonyesha leadership kubwa sana, yaani amejipambanua kama kiongozi makini!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…