Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Wanabodi,

Benard Membe amesema bado anajishauri kama agombee kumpinga Magufuli sio ili ashinde uchaguzi bali kuunogesha tuu uchaguzi.

Trend hii imepatikana kwa kumsikiliza Membe kwa kutumia analytical listening in between the words, na kubaini kitu kilicho moyoni kwa msemaji japo hajakizungumza expressly but impliedly kupitia matamshi yake.

Time will tell.

Nawatakia Jumapili Njema.

P


Kaka Pascal, ebu pitia ujumbe wangu hapa nimeuliza matumizi ya sisi, tumehuru, kuwauliza viongozi na etc, the political pig with vuvuzela has unfolded a number of issues.
 
Membe anasema:

Nimetafakari wito wa Watanzania. Mchakato wa Uchaguzi ulipoanza sikuamini tungefanya uchaguzi kutokana na hali ya Corona. Nilitarajia ungefanywa uchambuzi mkubwa sana kabla ya kuamua kuingia kwenye uchaguzi katika mazingira haya.

Nilihoji, tunaweza kwenda kwenye Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi? Jibu likawa – tuwe na Tume Huru. Lakini, safari hii Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa hawatakuwepo. Je, tuko tayari kuwa na Uchaguzi usio na waangalizi wa Kimataifa?

Kuhusu kugombea ndani ya CCM:

Tumefikia uamuzi kuwa sisi hatujamkosea mtu, hatujawa wahalifu, na hatuna uoga na tunajiamini. Tunayo haki kabisa ya kugombea Urais kwakuwa tunalindwa na Katiba na si utamaduni. Tunamheshimu Mwenyekiti na tunaiheshimu Kamati Kuu. Walichokisema kilikuwa ni mapendekezo na yatafanyiwa kazi na Halmashauri Kuu ya Taifa ambayo itafanyika mwezi Julai. Chombo kinachotoa adhabu ndani ya CCM ni Halmashauri Kuu ya Taifa; bahati mbaya Kamati Kuu wao walitamka kuwa “Membe tumemfukuza” na hawana mamlaka hayo.

Kamati Kuu ya CCM inaweza ikakataa, ikasema tulichoamua – tumeamua… Inaweza kabisa ikakataa! Ikikataa, sitoweza kwenda Dodoma kuchukua fomu. Kunikataa mimi kugombea ndani ya CCM, Uchaguzi haunogi. Mimi sitakwenda Dodoma mpaka Kamati Kuu itakaponiambia kuwa nipo huru kufanya hivyo, siko tayari kuingia kwenye mtego. Lazima tupate ridhaa!

Nisipopata ridhaa, tunakitakia chama chetu kila la heri. Uchaguzi ni Oktoba, sasa ni Juni… Chochote kinaweza kutokea hapa katikati. Nawaomba vijana tulieni, msilete ghasia zozote. Hatujui Mungu alichotupangia, tusitoe hukumu mapema! Tuwe na imani, yote tumwachie Mwenyezi Mungu.

Video hii hapa:


View attachment 1484912
Mpo na dikteta mnaona mambo yalivyo mabaya na huyo mtu mkimwachia awamu ya pili mtateseka zaidi.
 
Labda kama kuna video nyingine,ila kwa hii uliyoisikiliza wewe mhh.

Anaiheshimu kamati kuu,anaisubiri itoe tamko ama hata kiongozi mmoja wa hiyo kamati kuu..akisema yupo huru basi ataenda kuchukua fomu.

Vinginevyo kamati kuu/kiongozi wake wakikaa kimya Membe hachukui fomu. Huo ni mtego.

Uchaguzi unanoga panapokuwa na ushindani,uwepo wake utafanya unoge zaidi..si unakumbuka ulipoweka kambi kwa Lowassa. Zile raha za mshikemshike..ndo kunogesha kwenyewe.

Ila huyu jamaa pengine anavitu ambavyo wengi hatuvijui.

Hotuba yake hii inahitaji kufanyiwa critical analysis hasa na vyombo vya usalama.

Inanikumbusha hotuba za Osama Bin Laden,ikulu ya marekani haikuwahi kuzipuuza. Zilichambuliwa in detailed.

Membe sio wa kumpuuza hata kidogo.

June-Oct lolote lile litatokea,tuwe wapole.

Kazungumza kwa namna yenye harufu ya uhaini na uasi, inahitaji akili za kawaida tu kuliona hili.
 
Kama ni kweli basi Membe atakuwa amejipanga kisawasawa.
Kama form inatolewa na mtu mmoja Bashiru, basi itakuwa ngumu.
Na akikataliwa ATAKINUKISHA.Hoja yake ikipata mtu wa kuipigia upatu katika NEC ni wazi kutatokea mtafaruko heavy.Na kama hawatamtuliza Membe basi CCM inaweza ikagawanyika vipande vitatu.
 
Huo urais aende akagombee chadema au ACT lakini sio CCM na haita kuja itokee membe awe rais wa tanzania ,hana vigezo wala hata nusu ya kumfikia Dr. Magufuli hakuna wa kumpinga magufuli ndani ya CCM. Over.
Yaani mwenye uwezo wa kuongoza CCM ni Magufuli tu?
 
Ofisi gani intampa hizo fomu, Kama anatumwa na K. Kikwete na wanamtandao aende chama chochote maana jumatatu fomu hapewi ofisi yoyote ya CCM, na ajiandae kweli kweli anaemtuma kachelewa angempa urais 2015, watu wa pwani walijiaminisha ccm washaimiliki sasa ndio basi na ccm hamtaikamata tena. Aanzishe vita bwege huyu tutamfuata huko aliko na AK47 tumevumilia sasa basi, ruhusa inachelewa sana, moto auwashe hio wiki ijayo. Hio corona ya Bibi zake.
Huko CCM hakuna demokrasia tena?
 
huyu ndiye mwanaume sasa!!!! ccm wakijiloga kumpitisha tu.... meko bye bye na hata akigombea chama kingine membe anashinda uchaguzi
 
Ni mfumo bibie, CCM ina mizizi, Membe mwenyewe kanywa maji ya chama anajua nguvu zake
Basi mruhusu demokrasia achukue fomu ili akajipime na Mtukufu na KUNOGESHA uchaguzi, shida ni nini wana CCM wenzangu?
 
Membe ametoa dira,ni wazi kuwa kamati kuu wanamuogopa membe maana hawajui aki na nani wapo nyuma ya Membe,hivyo kwa kugombea ndani ya CCM akitegemea kuwa CC ya CCM itatengua ni ndoto.
Membe katoa option,kuwa chochote kinaweza kutokea kati ya juni na Oktoba.

Lkn jambo la msingi na muhimu kabla ya yote ni tume huru ya uchaguzi na waangalizi wa uchaguzi wa kimataifa.

Hapo ndio kuna point,Membe anaungana na Askofu Bagonza kudai tume huru ya uchaguzi.

Tume huru itaweka usawa kwa vyama vyote na kwakuwa CCM wamefanya makubwa chini ya Rais Magufuli ni wazi kuwa hawataogopa uwepo wa Tume huru ya uchaguzi.

Sitegemei mpaka maandamano ndio tume huru iwekwe,CCM ni chama kikubwa naamini kitaviongoza vyama vingine kudai tume huru
 
Membe anafaa.

2020 Twende na Membe.

Kitendo cha kutetea tume huru ya uchaguzi iliyofair kwa wote ameonyesha leadership kubwa sana, yaani amejipambanua kama kiongozi makini!
 
Back
Top Bottom