Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Membe anasema:

Nimetafakari wito wa Watanzania. Mchakato wa Uchaguzi ulipoanza sikuamini tungefanya uchaguzi kutokana na hali ya Corona. Nilitarajia ungefanywa uchambuzi mkubwa sana kabla ya kuamua kuingia kwenye uchaguzi katika mazingira haya.

Nilihoji, tunaweza kwenda kwenye Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi? Jibu likawa – tuwe na Tume Huru. Lakini, safari hii Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa hawatakuwepo. Je, tuko tayari kuwa na Uchaguzi usio na waangalizi wa Kimataifa?

Kuhusu kugombea ndani ya CCM:

Tumefikia uamuzi kuwa sisi hatujamkosea mtu, hatujawa wahalifu, na hatuna uoga na tunajiamini. Tunayo haki kabisa ya kugombea Urais kwakuwa tunalindwa na Katiba na si utamaduni. Tunamheshimu Mwenyekiti na tunaiheshimu Kamati Kuu. Walichokisema kilikuwa ni mapendekezo na yatafanyiwa kazi na Halmashauri Kuu ya Taifa ambayo itafanyika mwezi Julai. Chombo kinachotoa adhabu ndani ya CCM ni Halmashauri Kuu ya Taifa; bahati mbaya Kamati Kuu wao walitamka kuwa “Membe tumemfukuza” na hawana mamlaka hayo.

Kamati Kuu ya CCM inaweza ikakataa, ikasema tulichoamua – tumeamua… Inaweza kabisa ikakataa! Ikikataa, sitoweza kwenda Dodoma kuchukua fomu. Kunikataa mimi kugombea ndani ya CCM, Uchaguzi haunogi. Mimi sitakwenda Dodoma mpaka Kamati Kuu itakaponiambia kuwa nipo huru kufanya hivyo, siko tayari kuingia kwenye mtego. Lazima tupate ridhaa!

Nisipopata ridhaa, tunakitakia chama chetu kila la heri. Uchaguzi ni Oktoba, sasa ni Juni… Chochote kinaweza kutokea hapa katikati. Nawaomba vijana tulieni, msilete ghasia zozote. Hatujui Mungu alichotupangia, tusitoe hukumu mapema! Tuwe na imani, yote tumwachie Mwenyezi Mungu.

Video hii hapa:

View attachment 1484912
Anaposema lolote laweza kutokea kati ya sasa hadi October, ni wazi Mr Membe ni zaidi ya mtia nia.
Huwezi kumpuuza kwa sababu hatujui ana silaha zipi.Kilichomsukuma akahitisha mkutano bila kukatishwa na vyombo vya Dola,ujue ameishajizatiti.
 
Membe anasema:

Nimetafakari wito wa Watanzania. Mchakato wa Uchaguzi ulipoanza sikuamini tungefanya uchaguzi kutokana na hali ya Corona. Nilitarajia ungefanywa uchambuzi mkubwa sana kabla ya kuamua kuingia kwenye uchaguzi katika mazingira haya.

Nilihoji, tunaweza kwenda kwenye Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi? Jibu likawa – tuwe na Tume Huru. Lakini, safari hii Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa hawatakuwepo. Je, tuko tayari kuwa na Uchaguzi usio na waangalizi wa Kimataifa?

Kuhusu kugombea ndani ya CCM:

Tumefikia uamuzi kuwa sisi hatujamkosea mtu, hatujawa wahalifu, na hatuna uoga na tunajiamini. Tunayo haki kabisa ya kugombea Urais kwakuwa tunalindwa na Katiba na si utamaduni. Tunamheshimu Mwenyekiti na tunaiheshimu Kamati Kuu. Walichokisema kilikuwa ni mapendekezo na yatafanyiwa kazi na Halmashauri Kuu ya Taifa ambayo itafanyika mwezi Julai. Chombo kinachotoa adhabu ndani ya CCM ni Halmashauri Kuu ya Taifa; bahati mbaya Kamati Kuu wao walitamka kuwa “Membe tumemfukuza” na hawana mamlaka hayo.

Kamati Kuu ya CCM inaweza ikakataa, ikasema tulichoamua – tumeamua… Inaweza kabisa ikakataa! Ikikataa, sitoweza kwenda Dodoma kuchukua fomu. Kunikataa mimi kugombea ndani ya CCM, Uchaguzi haunogi. Mimi sitakwenda Dodoma mpaka Kamati Kuu itakaponiambia kuwa nipo huru kufanya hivyo, siko tayari kuingia kwenye mtego. Lazima tupate ridhaa!

Nisipopata ridhaa, tunakitakia chama chetu kila la heri. Uchaguzi ni Oktoba, sasa ni Juni… Chochote kinaweza kutokea hapa katikati. Nawaomba vijana tulieni, msilete ghasia zozote. Hatujui Mungu alichotupangia, tusitoe hukumu mapema! Tuwe na imani, yote tumwachie Mwenyezi Mungu.

Video hii hapa:

View attachment 1484912
Kwa kukosekana kwa Tume huru ya uchaguzi basi serikali ya awamu ya tatu na nne zilikuwa batili, hivyo waliongoza serikali hizo warudishe mishahara Yote
 
Kasema kati ya juni na oktoba chochocte chaweza tokea, namuona ACT....changamoto inakuja act wamesema wanaungana na chadema, je chadema watakubali membe awe mpeperusha bendera? Jibu: hii ni karata ya chadema kumsimamisha membe kwa kivuli cha act, waonekane sio wao waliomchukua membe na kuonekana wamerudia kosa lile lile la lowasa....chadema hawasimamishi mtu uchaguzi huu bali watamuunga mkono membe wa act...
Angalizo kwa sisiemu: huyu jamaa akiingia kugombea urais, kuna manouvre makali atafanya na kina januari kwenye votes...
Ifanyike juhudi zozote asichukue form ktk chama chochote, kwa kifupi asigombee! Sio kwamba ana nguvu ya kupendwa, la hasha, JPM anakubalika zaidi kwa wananchi, uwanja ukiwa fair, jpm anashinda dhidi ya membe saa tatu asubuhi, ila link kali aliyonayo membe ya kucheza na votes ndio threat, ana link na vijana wa it mpaka wa nje na bado ana vijana kawaacha tiss...

Acha uoga huyu kopo tu kama makopo mengine, tunamsubiria kwa hamu aje ulingoni, kapauka hata shanti inaweza mkataa
 
[QUO"Apolinary, post: 35773311, member: 53034"]
Anachukua kwa chama kipi?
Kwa chama hiko hiko cha CCM..,..

Kwani nyinyi maccm kwa akili zenu mnadhani mmemfukuza Membe kwa Katiba ya CCM kweli?

Sasa ndiyo mtakapoijua mbivu na mbichi
[/QUOTE]
Bashiru na wahuni wenzake ndio atajua hajui
 
Ccm mna mtu makini sana na mwenye uzoefu mkubwa wa uongozi ndani na nje ya nchi huyu ni Bernard Kamilius Membe. Huyu ni mdemokrasia na anaziweza siasa za kidiplomasia na ujengaji hoja.

Membe atasaidia ccm kuondokana na udikteta unaokichafua chama na nchi nzima. Kumekuwa na malamiko ya chini chini ya ukabila nadhani Membe ana nafasi nzuri zaidi ya kuirejesha nchi kwenye mstari mnyoofu, mwacheni agombee urais.
 
Kweli watoto wa mjini ni balaa....Kwaiyo wamemuingiza chaka mwenzao kumpa fomu ya uongozi wa vyombo vya dola, alafu ya urais anapewa Membe..... Duuh kweli kuzaliwa mjini raha sana
Naona raia wengi mnasema alipewa fomu ya kugombea uongozi wa vyombo vya dola. Ni wapi mliyajua hayo, wengine sisi wageni hapa
 
Yani ni afadhali apewe form CCM na kushindanishwa na Anko Magu ambako Magu anaweza kushinda kuliko mkimnyima akaenda upinzani ataenda kuboost upinzani kwa kiasi kikubwa sana na kusababisha wanachama wa upinzani kuongezeka na idadi ya wabunge na madiwani kuongezeka kama ilivyokuwa uchaguzi ulipita wakati wa mamvi.
 
Akipewa form CCM itasaidia CCM zaidi kuliko wakimnyima na kwenda upinzani.

Akipewa form CCM faida itakuwa ya chama maradufu kuliko akienda upinzani.

Haya mambo yanahitaji kumtanguliza Mungu mbele na kukubali mapenzi ya Mungu kutimia.

Na haki itendeke sababu Mungu ni mwenyehaki siku zote!
 
Kwani akichukua 2020 kuna ubaya ?Hii ndo demokrasia. Ndo tupime kweli Magu anakubalika au unafki wa watu tu ?
Why now? Kwa nini disturbing the piece now? Utaratibu wa zamani wa chama ulikuwaje? Mkapa walichukua form? Kikwete walichukua form? Membe nae anajua utaratibu wa sisiemu hii, na kubadilihwa kwa huo utaratibu sio muda huu....
 
Membe anasema:

Nimetafakari wito wa Watanzania. Mchakato wa Uchaguzi ulipoanza sikuamini tungefanya uchaguzi kutokana na hali ya Corona. Nilitarajia ungefanywa uchambuzi mkubwa sana kabla ya kuamua kuingia kwenye uchaguzi katika mazingira haya.

Nilihoji, tunaweza kwenda kwenye Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi? Jibu likawa – tuwe na Tume Huru. Lakini, safari hii Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa hawatakuwepo. Je, tuko tayari kuwa na Uchaguzi usio na waangalizi wa Kimataifa?

Kuhusu kugombea ndani ya CCM:

Tumefikia uamuzi kuwa sisi hatujamkosea mtu, hatujawa wahalifu, na hatuna uoga na tunajiamini. Tunayo haki kabisa ya kugombea Urais kwakuwa tunalindwa na Katiba na si utamaduni. Tunamheshimu Mwenyekiti na tunaiheshimu Kamati Kuu. Walichokisema kilikuwa ni mapendekezo na yatafanyiwa kazi na Halmashauri Kuu ya Taifa ambayo itafanyika mwezi Julai. Chombo kinachotoa adhabu ndani ya CCM ni Halmashauri Kuu ya Taifa; bahati mbaya Kamati Kuu wao walitamka kuwa “Membe tumemfukuza” na hawana mamlaka hayo.

Kamati Kuu ya CCM inaweza ikakataa, ikasema tulichoamua – tumeamua… Inaweza kabisa ikakataa! Ikikataa, sitoweza kwenda Dodoma kuchukua fomu. Kunikataa mimi kugombea ndani ya CCM, Uchaguzi haunogi. Mimi sitakwenda Dodoma mpaka Kamati Kuu itakaponiambia kuwa nipo huru kufanya hivyo, siko tayari kuingia kwenye mtego. Lazima tupate ridhaa!

Nisipopata ridhaa, tunakitakia chama chetu kila la heri. Uchaguzi ni Oktoba, sasa ni Juni… Chochote kinaweza kutokea hapa katikati. Nawaomba vijana tulieni, msilete ghasia zozote. Hatujui Mungu alichotupangia, tusitoe hukumu mapema! Tuwe na imani, yote tumwachie Mwenyezi Mungu.

Video hii hapa:

View attachment 1484912
Kauli kama hizi ndizo haswa zinahitajika kukisika kutoka kinywani mwa mtu makini kabisa, mwenye uelewa mpana wa masuala ya kimataifa na tena mwenye kumaanisha kuwa Rais wa Tanzania.
 
Ni kweli, ila aliposema lolote laweza tokea kati ya juni na oktoba, anaweza akavuka boda....
Huyu jamaa ni mbishi Sana labda mumiminie risasi kama 40 Kama mlivyofanya kwa lissu,vingi evyo mnautema uraisi mapemaa.

Tuliwaonya sana huyu jamaa yenu atakuwa raisi wa kipindi kimoja tu hamkuelewa ona sasa mmeanza kupoteana
 
Back
Top Bottom