Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Uchaguzi 2020 Membe: Kamati Kuu haina mamlaka ya kunifukuza Uanachama wa CCM bali Halmashauri Kuu ya Taifa. Asema kati ya Juni na Oktoba chochote kinaweza tokea

Membe anasema:

Kuhusu kugombea ndani ya CCM:

Kuhusu kugombea ndani ya CCM, tukafikia mwafaka na Washauri, Tukafikia uwamuzi kwamba, sisi hatujamkosea mtu, sisi hatujawa waharifu, sisi hatuna uoga na tunaniamini, sisi tuna haki kabisa kabisa ya kugombea urais huu kwa sababu tunalindwa na Katiba sio Utamaduni. Tunalindwa na Katiba ya Nchi.

Lakini tukasema, kwakuwa Kamati Kuu tunaiheshimu, tunamheshimu Mwenyekiti na tunaiheshimu Kamati Kuu. Tungependa basi, kamati Kuu itamke iseme kwamba, kile tulichokisema sisi Wakati ule ni Mapendekezo ni Bahati mbaya yalitoka nje. Ni mapendekezo ambayo yatafanyiwa Uamuzi na Halmashauri kuu ya taifa mwezi ujao wa Saba.

Na mpaka hapo Halmashauri kuu ya Taifa itakapo kaa, Mheshimiwa hana hatia. Wakitamka hivyo leo, au wakitamka hivyo Kesho, tutajaza kugombea urais Jumatatu asubuhi. Naomba nirudie, kwakuwa chombo kinachotoa adhabu ni Halmashauri kuu ya Taifa, na kwakuwa kamati ya Maadili tayari imeandaa taarifa yake na wameipitisha kwenye Kamati Kuu na kwa bahati Mbaya Kamati kuu ikatamka kwamba "Membe tumemfukiza" kinyume cha Utaratibu. Kamati kuu au Msemaji yeyote au Katibu Mkuu au Katibu Mwenezi, akieleza leo kwamba alichokisema Mheshimwa Membe ni sahihi, sisi tunayo repoti iliyotoka kwenye Kamati ya Maadili na Sisi Kamati kuu tumeshaweka mapendekezo yetu, tunayapeleka kwenye NEC.

NEC inakutana mwezi ujao lakini Shughuli za Urais zipo sasa, mpaka hapo NEC itakapo kaa na kuamua iwapo Mheshimiwa Membe afukizwe au la!, Sasa hivi Mheshimiwa Membe yupo huru Kujaza Fomu, Kugombea, Kupata Wadhamini, na kujipima na Rais. Wakitamka hivyo leo au Kesho, Jumatatu nitajaza Fomu ya kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano CCM Oyeee..!!

Lakini Kamati Kuu inaweza kukataa, ikasema hapana, sisi tulichoamua tumeamua, Mheshimiwa Membe tumemfukuza, sasa yeye akitaka aende Upande mwingine tukutane mwaka 2020. Kamati kuu ni kubwa, inaweza kabisanikakataa. Ikikataa, huwezi mimi kunituma niende Dodoma. Niende kule nikikataliwa kuchukua Fomu? Je, nikipewa ile Fomu nikaenda kwenye Mkoa au Kwenye Wilaya nisimkute anayekusika, anasema ameitwa Dodoma kwenye Ushauri au unauguliwa na Mkwe wake nimsubiri baada ya Siku Mbili? Haitawezekana.

Kwahiyo kugombea kwetu kwenye Chama cha Mapinduzi, ambapo kungewasha hisia kubwa na Msisimko Mkubwa wa Watu kwenda kupiga kura. Na watu wote wangesema Uchaguzi huu unanoga kama mnavyo sikia Uchaguzi wa Zanzibar unavyo Noga, you Mnogeshaji ni Mimi. Ukinikataa mimi nisiende kugombea, Uchaguzi huu hauonogi!.

Na niwaambie Siri.. Naiambia Tanzania na Dunia na nyie watu wangu wa Rondo. Na nimalizie tu kwa kusema hivi, Mimi sitakwenda Dodoma Mpaka Kamati Kuu, au Mjumbe yoyote wa Kamati Kuu atakapo nieleza Mheshimiwa Membe upo Huru fanya hivyo. Kwa sababu tusipofanya hivyo, tutaingia kwenye Mitego. Tutaingia kwenye nini?.. (Mitego)... Tena inaitwa Shilibata.. Utanasa.

Ni lazima tupewe ridhaa, kama hatutapata ridhaa, tunakitakia chama chetu kila la heri kwenye Uchaguzi huu. Hilo la Kwanza.

La pili;

Uchaguzi ni Mwezi wa ngapi? (Wananchi wanaitikia... Wa kumiii...)

Huu ni mwezi wa ngapi? ( Wananchi wanaitikia wa Sitaaa)

Chochote kinaweza kutokea hapa katikati.(Wananchi wanapiga Makofi na Kelele)

Mumenielewa? Nmeeleweka?. Sasa naomba Vijana wote kwa jina la Mwenyezi Mungu, Mtulie, Msilete ghasia zozote, tulieni hatujui Mungu alichotupangia, tusitoe hukumu Mapema. Naelewa jinsi Mioyo yemu inavyowaka Moto. Lakini muwe na imani kwa sababu leo nmepigiwa simu nyingi sana kutoka Dar Es Salaam na kutoka Mikoa mingine ya Kusini wote wakiwa na Mioyo hii.

Lakini naomba tutulie, tusilete fujo, tusilete gasia yoyote Vyote tumuachie Mwenyezi Mungu. Lengo letu sisi tuwe na Uchaguzi wenye amani lakini wengine sisi hatutoacha kueleza Ukweli kwa sababu ukweli ndio hazina ha Siasa.

Nitasema kweli? (Wananchi wanaitikia.. Daima)

Fitina kwangu? (Wananchi wanaitikia.. Mwiko)

Asanteni na salaam Aleikum.

Pia Soma:

Elections 2020 - Bernard Membe: Tunafanyaje Uchaguzi bila Tume Huru ya Uchaguzi na Waangalizi wa Uchaguzi wa Kimataifa?

CCM yamfukuza uanachama Bernard Membe, Kinana apewa karipio kali huku Makamba akitoka salama

Membe asitafute kiki eti vijana watulie wasilete ghasia, wajaribu waone watakavyochakazwa kwa kipigo cha mbwa koko. Membe atulie tu keshafukuzwa atafute chaka lingine mbona machaka ya matapeli wa kisiasa yapo mengi tu?
 
mkuu vipi unahasira na membe?
 
Simtishi Membe bali ni kumjulisha kuwa baada ya zoezi la uchaguzi mkuu hapo Oktoba mwaka huu kwa hakika satoshi magumu mno!

Kama wasemavyo wao kwamba MWENYE KULITAFUTA NA HULIPATA.

Ni hayo tu.
 
Yule ni bilionea alikwiba mabilion ya Watanzania kule libya

Ndio maana
 
Huyo ana pesa za kuishi nje ya nchi maisha yake yote yaliyobaki duniani kwa starehe na chenji ikabaki, hao walishapiga pesa kipindi cha Mkwere halafu pia ni mtu wa idarani huyo anajua kila kitu kinachopangwa na kinachoendelea kila siku Magogoni na chamwino anajua hadi sasa hivi baba jeska anapiga mvinyo au kapiga chafya ndio maana akaitwa mbobezi system yote anaijua....NB: Usimuamini sana mwanasiasa hizi zote ni kutaka kuichanganya upinzani na kuwaondoa kwenye tension ya uchaguzi ili magu apate mserereko na wenyewe wakiicheza hii singeli ya membe wameenda na maji.
 
Kwan yeye halijui hilo???

Nakwann umpe maisha mgumu mtu aliyesahihi katika kile kinachofahamika na wengi???

Nadhan mwenye maisha magumu niyule atakayeamua kumuumiza mwenzake,, Usoni mwake atafurahi lkn moyon ataumia sana.

Alafu mwisho wa siku, Anakufa mapema, Membe bado anadunda.
 
Simtishi Membe bali ni kumjulisha kuwa baada ya zoezi la uchaguzi mkuu hapo Oktoba mwaka huu kwa hakika satoshi magumu mno!

Kama wasemavyo wao kwamba MWENYE KULITAFUTA NA HULIPATA.

Ni hayo tu.
hakuna kama kuna mtu atakuja kuishi vibaya (kama ataishi that is) kama Bashite beyond October 2020 / October 2025.
 
Simtishi Membe bali ni kumjulisha kuwa baada ya zoezi la uchaguzi mkuu hapo Oktoba mwaka huu kwa hakika satoshi magumu mno!

Kama wasemavyo wao kwamba MWENYE KULITAFUTA NA HULIPATA.

Ni hayo tu.
Hivi kosa lake Membe ni nini haswa? Maana mko kama kasuku mnaimbishwa tu.
 
Huyo ana pesa za kuishi nje ya nchi maisha yake yote yaliyobaki duniani kwa starehe na chenji ikabaki, hao walishapiga pesa kipindi cha Mkwere halafu pia ni mtu wa idarani huyo anajua kila kitu kinachopangwa na kinachoendelea kila siku Magogoni na chamwino anajua hadi sasa hivi baba jeska anapiga mvinyo au kapiga chafya ndio maana akaitwa mbobezi system yote anaijua....NB: Usimuamini sana mwanasiasa hizi zote ni kutaka kuichanganya upinzani na kuwaondoa kwenye tension ya uchaguzi ili magu apate mserereko na wenyewe wakiicheza hii singeli ya membe wameenda na maji.
Sisi tunachojua Membe ndiye mgombea wa kiti cha Urais kupitia CCM mwaka huu ni suala la muda tu.
 
Back
Top Bottom