Uchaguzi 2020 Membe: Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala, nitajitosa na nitashinda

Miundombinu inajengwa kwa kodi za wananchi na sio hisani au mshahara wa rais. Hivyo miundombinu itajengwa na yoyote hata kama nchi itakuwa haina rais kwani mipango ya nchi ipo tayari.
Duh mkuu, uko sawasawa kweli. Huo ndo upeo wako wa kufikiria au kuna kitu kime hack ubongo wako
 
CCM kuna demokrasia ambapo wanachama wanajadili mambo yao kwa uwazi kwenye vikao halali vya Chama. Hiyo demokrasia ya kujificha na kuanza kufanya mipango ya uhaini si demokrasia bali domogasia
Makatibu wamekuja na waraka kwa nia njema tu, tumeona walivyoshambuliwa kwa matusi sijui ndiyo demokrasia unayoisema.
 
Umetoa mchango wa mawazo mzuri sana. Wewe ni great thinker
 
Kwani katiba ya CCM inasemaje kuhusu hilo?
 
Ukweli ni kwamba JPM ni kiongozi mzuri sana,kama angeheahimu katiba na chama chake pia,angeshughulika na matatizo ya nchi pasipo kiburi na jeuri,angeacha kufanya upendeleo wa wazi wazi kama afanyavyo sasa,angeimarisha taasisi zaidi na sio kwa kiburi cha kujiona yeye ni booora kuliko wengine wote!

Amekuta nchi hii inaendelea kujengwa,(barabara,viwanja vya ndege,madaraja,na miradi mingine mingi) ila ajabu sasa akisimama yeye anazungumza kana kwamba nchi ameikuta ikiwa jangwa na ameanza yeye kuijenga (hii si sawa hata kidogo)

Tazama mfano mdogo tu huu,alipokuwa anazindua terminal 3 ya uwanja wa mwl.Nyerere,amesahau kuwa terminal 1 na two tayari zilikuwa zimejengwa na watangulizi wake,na yeye kwa sehemu yake amesimamia ujenzi wa hiyo terminal 3,lakini namna anavyozungumza utadhani yeye ndo wa kwanza kuijenga hiyo airport!

Ameenda mbali zaidi kwa kiburi na jeuri kwamba "ikitokea siku Mungu amenichukua sina hakika kama anayekuja ataweza kazi hii..." Khaaa! Yaani amefika mahali anaona hakuna mtu mwingine anayeweza kufanya kazi ya urais isipokuwa yeye? Na anadiriki kusema hadharani eti Mungu akimchukua, kwani watanzania wamesema wanataka awe rais mpaka Mungu amchukue?

Katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea inamwambia kuwa atakuwa hapo mpaka Mungu atakapomchukua? Au ni jeuri na kiburi cha madaraka? Ni kiongozi wa kawaida sana tu,na kama ingekuwa mtu wa kukaa madarakani mpaka kufa alikuwa baba wa taifa hili,kwa sababu watu walimpenda pamoja na mapungufu machache aliyokuwa nayo!

Hawa wengine ni wadanganyifu tu,wanaitumia Ikulu yetu kujinufaisha,tena huyu anafanya wazi wazi,tazama CHATO inavyofanywa bila aibu tunahamisha mpaka hifadhi!

Kama kila mtu angetaka kufanya kama afanyavyo huyu,basi kuna maeneo yangekuwa masikini kabisaaa kwa sababu tu,hayakutoa mtu mwenye wadhifa wa rais!

TUJIREKEBISHE,TUHESHIMU KATIBA YETU ,TUJENGE NCHI KWA ZAMU!
 
Kwa wanasiasa ni jambo la kawaida
Hata wewe zipo nyuzi zako humu unawsshabikia slaa,zitto na kitila,nina uhakika ukikutana nao leo unaweza hata kuwatemea mate
Labda Slaa, lkn Zitto na Kitila tangu mwanzo nilikuwa na wasiwasi wao.
 
Akili za wana CCM wasio kuwa na maono ndio hutoa michango kama yako. Mbona hamja mshughulikia au mnasubiri wakati wa kura za maoni? Shame!!!
 
Miundombinu inajengwa kwa kodi za wananchi na sio hisani au mshahara wa rais. Hivyo miundombinu itajengwa na yoyote hata kama nchi itakuwa haina rais kwani mipango ya nchi ipo tayari.
Tatizo hapq siyo kujenga swala kubwa hapa ni usimamizi na nidhamu kwa pesa zetu wananchi.
 
Labda Slaa, lkn Zitto na Kitila tangu mwanzo nilikuwa na wasiwasi wao.
Nassary kauza mechi upo kimyaa,Mbowe kapitiliza muda madarakani hataki uchaguzi upo bize na ccm na membe
Akili yako inakuambia kabisa,membe atachukua fomu,atarudisha,atapitishwa na sekretarieti,atapitishwa na kamati kuu,ataputishwa na NEC,halafu atapita kwa kishindo kwenye mkutano mkuu?lazima ukapimwe
Membe na January wameshakosa sifa za kugombea urais,kwa sababu walishafunguliwa ma file na mangula ya kucheza rafu 2015 kwa kuanza mapema kampeni
Zama hizi ni za magufuli ni bora tu wakae nyumbani
 
Huyu Mzee anaota ndoto za mchana. Hivi kwani lazima kila mtu afanye siasa?.
 
Wakati mwingine unaweza usielewe watanzania wanataka nn. Hata kama ni kuchanganyikiwa sio kwa kiwango hicho. Hatujafikia hatua ya kuona membe anaweza kuwa rais mzuri kuliko magufuli.

Mi naona ni mbinu tu za kisiasa baada ya kuona hana mwelekeo yeye na kundi lake so wanajaribu kutafuta umaarufu. Lakin kwa akili y kawaida hawana tena future kwenye siasa za nchi hii. Wamepoteza wakubali either kustaafu au kushirikiana na serikali iliyopo otherwise wanajitengenezea future mbaya tu bila sababu za msingi.

Hakuna mtu alikuwa na nguvu ndan ya CCM kuliko Lowasa. Lakin unavotangaza kupambana na mtu alie madarakan hadharan sidhan kama unaelewa maana yake. Marekan tu wameshindwa kumchomoa Trump sembuse nchi zetu hizi changa kidemocrasia. Wanaomshauri wanamdanganya.

Membe habari yake ishaisha kwenye siasa za Tanzania. Ni kama Lowasa habari yake ilivoisha baada ya kuondolewa kwenye uwaziri mkuu. Its over. Kwanza mtu mwenyewe hana mvuto kama aliokuwa nao Lowasa. Lakin pia hana ubavu wa kupambana na kundi jipya la akina Magufuli ambao ni majasiri kuliko ujasiri wenyewe. Subirin mtaona.

Kama obama alivopambana kumuondoa Trump akashindwa ndivo wanaomshauri Membe wanavojiharibia.

Kama kuna kosa walifanya ni pale walipompa Nchi magu. Hawawezi kumnyang'anya tena. Wasubiri tu muda wake uishe. Lakin as i know story ya Membe kuwa Rais ishafungwa. Asahau kabisa
 
Kati ya wanasiasa Nassary naye unamhesabu, kuhusu Mbowe kasome katiba ya Chadema. Kama matokeo ya vikao vyote vya CCM unayajua yanajulikana kwa wanachama kama wewe kuna haja tena ya CCM kufanya vikao.

Ni kweli kwa sasa Magufuli ni kila kitu, amekuwa mkubwa kuliko chama, yeye ndio katiba, neno lake halipingwi wala kukosolewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…