Wyatt Mathewson
JF-Expert Member
- Dec 22, 2017
- 10,432
- 25,124
Tusiandikie mate na wino ungalipo, tusubiri tuone
Tusubiri!
Hao hao anaowategemea kua ni watu wake hawawezi gusa jina lake ndio hao hao watalikata ndio atajua maharage ni mboga!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tusiandikie mate na wino ungalipo, tusubiri tuone
Nyie si mnasema kila siku kuwa Jiwe anakubalika ,sasa atajuaje kuwa anakubalika sasa si ashindane na membe aonekane anavyokubalika ,mbona anaogopa hivyo ushindani .Halafu upinzani ndani ya chama sio uhaini ,tatizo la Jiwe wenu hajui siasa yeye ni ubabe ,matokea yake hana sapoti kabisa ndani ya chama labda wachumia tumbo kina Bashiru ,polepole ,musukuma ,lusinde ambao ni empty head ,membe akigombea Jiwe byebye .
kama ubunge watu watajitosa kugombea sioni tatzo yeye akifanya hivyo kwenye uraisBernard Kamillius Membe waziri wa zamani wa Mambo ya nchi za Nje na uhusiano wa kimataifa, anazidi kukoleza mbio za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Yusufu Katimba.
Taarifa za hivi karibuni zinasema Membe ambaye alikuwa waziri kwa miaka minane ya utawala wa Jakaya Kikwete, ameapa kujitosa katika kinyang'anyiro cha kumpinga rais wa sasa John Pombe Magufuli.
"Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala tuombe Mungu niwe mzima. Nitajitosa na nitashinda." Amenukuliwa mwanasiasa huyo akiwaeleza baadhi ya wafuasi wake wa karibu ndani ya chama hicho.
Amesema, "Katika hili siwezi kurudi nyuma na hayupo anayeweza kunishawishi kurudi nyuma. Nitagombea, nitajitosa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa nina kila sababu ya kufanya hivyo."
Kupatikana kwa taarifa kuwa Membe amepanga kujitosa katika mbio za urais 2020, kutaweza kumaliza mining'ono kuwa kwa muda mrefu kiongozi huyo amekuwa akiendesha mikakati yake kimya kimya ya kumkabili Magufuli ifikapo 2020.
![]()
Miundombinu inajengwa kwa kodi za wananchi na sio hisani au mshahara wa rais. Hivyo miundombinu itajengwa na yoyote hata kama nchi itakuwa haina rais kwani mipango ya nchi ipo tayari.
Kwa kumsengenya mwenyekiti wa ChamaAtafukuzwa kwa kosa gani.
Muulize huyo jiwe wako alipokuwa waziri alikuwa anasimamia nini? Acha uzwazwa.Aliyekuwepo huko nyuma alijenga miundo mbinu IPI?? Huyo hawezi kuwa rais hata kwa mtutu was bunduki!!
Wakimfukuza ndio itakuwa vizuri ili mkose pa kujifichia pale mnaposema ccm kuna demokrasia, na mkimuacha mmemuogopa.
Jane msalimie babaAmesema wapi
Mipango ilikuwepo tangu awamu ya kwanza. Tatizo unampigia chapuo mtu dhaifu kwa nafasi ya uraisi ili muendelee kutafuna nchi kirahisi zaidi.
JPM anatekeleza majukumu yaliyowashinda wengi hivyo ukiwa muathirika wa kukatiwa mrija lazima umpinge na hilo hatushangai.
Tukutane 2020
CCM kuna demokrasia ambapo wanachama wanajadili mambo yao kwa uwazi kwenye vikao halali vya Chama. Hiyo demokrasia ya kujificha na kuanza kufanya mipango ya uhaini si demokrasia bali domogasia
Leo Membe kawa kikaragosi wakati juzi nyie hao hao mlikuwa mnasema ni jembe bobezi la chama, kwa tabia hizi za wanaCCM si ajabu huko mbeleni Magufuli mkamuita kikaragosi.Labda urais wa YANGA
Kams alishindwa lowassa,alikua na NEC yote,na asilimia 90 ya wajumbe wa mkutano mkuu itakua kikaragosi membe?
Membe ni sawa na joka la mdimuni
Huwa wanasema "Ameenda kinyume na utamaduni wa chama"Kwa kumsengenya mwenyekiti wa Chama
Mkakati wake wa kipuuzi sana huo.Usiwe mjinga, kinachojadiliwa kwenye vikao rasmi na halali ni matokeo ya mikakati. Lakini mikakati inafanyika nje ya vyumba vya mikutano. Toka nje ya box usigeuzwe zoba na wadhaifu wa ushindani.
Kwa wanasiasa ni jambo la kawaidaLeo Membe kawa kikaragosi wakati juzi nyie hao hao mlikuwa mnasema ni jembe bobezi la chama, kwa tabia hizi za wanaCCM si ajabu huko mbeleni Magufuli mkamuita kikaragosi.
Usiwe mjinga, kinachojadiliwa kwenye vikao rasmi na halali ni matokeo ya mikakati. Lakini mikakati inafanyika nje ya vyumba vya mikutano. Toka nje ya box usigeuzwe zoba na wadhaifu wa ushindani.
Mkakati wake wa kipuuzi sana huo.
Alishashindwa 2015,huyu atakuja Chadema kuwazungusha vichwa badala ya mikonoBernard Kamillius Membe waziri wa zamani wa Mambo ya nchi za Nje na uhusiano wa kimataifa, anazidi kukoleza mbio za kuwania urais katika uchaguzi mkuu wa 2020 ndani ya chama cha Mapinduzi CCM. Anaripoti Yusufu Katimba.
Taarifa za hivi karibuni zinasema Membe ambaye alikuwa waziri kwa miaka minane ya utawala wa Jakaya Kikwete, ameapa kujitosa katika kinyang'anyiro cha kumpinga rais wa sasa John Pombe Magufuli.
"Kuhusu suala la urais hilo halina mjadala tuombe Mungu niwe mzima. Nitajitosa na nitashinda." Amenukuliwa mwanasiasa huyo akiwaeleza baadhi ya wafuasi wake wa karibu ndani ya chama hicho.
Amesema, "Katika hili siwezi kurudi nyuma na hayupo anayeweza kunishawishi kurudi nyuma. Nitagombea, nitajitosa katika kinyang'anyiro hicho kwa kuwa nina kila sababu ya kufanya hivyo."
Kupatikana kwa taarifa kuwa Membe amepanga kujitosa katika mbio za urais 2020, kutaweza kumaliza mining'ono kuwa kwa muda mrefu kiongozi huyo amekuwa akiendesha mikakati yake kimya kimya ya kumkabili Magufuli ifikapo 2020.
![]()
Wenzie wanafanya makakati wa kumfuta uanachama ajipange tu kwenda kwa akina Zitto