Uchaguzi 2020 Membe: Mimi nilitafuta wadhamini kimya kimya kukwepa mtego wa kuvunja kanuni na kuanza kampeni mapema

Uchaguzi 2020 Membe: Mimi nilitafuta wadhamini kimya kimya kukwepa mtego wa kuvunja kanuni na kuanza kampeni mapema

Wasalaam wana jamvi!

Mgombea wa ACT Wazalendo jana alikwenda mahakama kuuu kula kiapo kwa judge ... alipoulizwa na waandishi kuhusu njia yake ya kutafuta wadhamini aliweka wazi kabisa yeye alikuwa mtulivu kusoma kanuni na sheria hivyo ndio maana alitumia njia ya kutafuta wadhamini kimya kimya ili asivunje kanuni alizo zisoma na kuzielewa!

Alisema wazi kabisa hakutaka kuingia kwenye mtego wa kuanza kampeni kabla ya muda maana muda ya kujinadi bado haujafika mpaka hapo watakapo vuka kiunzi cha kuteuliwa na tume!

Ni wazi kuna mtu hapa alikuwa ana kumbushwa na kutumiwa salamu!

Wape salaaam....

Mswahilikavaasuti

Mswahili amevua koti la suti
 
Hamjui, anakaa porini huko atamjuaje. Huyu ndio yule ambaye wanaCCM walienda kwenye kibanda chake wakiomba kura maana wamenunua ndege
Tajeni hiyo sheria basi mbona mnazunguka tu sijui kanuni sijui nini, iko hivi kwenye vyama ndiko kwenye hayo makatazo ya kuanza kampeni mapema sasa watu kama Membe ameshazoea hizo kanuni za chama chake anadhani kuna sheria ya uchaguzi inayokataza kuanza kampeni mapema. Kwanza haiwezekani sababu wagombea wakishaidhinishwa huwa wanaruhusiwa kuanza kampeni sasa watawezaje kuanza kampeni kabla ya kuidhinishwa na tume ni mambo ya kuchekesha sana watu wenye akili wanahangaika kiasi hicho. Nakumbuka Membe mwaka 2015 kidogo aenguliwe na chama chake kwa kosa hilo ndiyo maana sasa hivi hata akiguswa na jani anafikiri ni nyoka.
Wenzako wanajua kusoma na kuandika.sheria unawauliza wataitoa wapi? Wahurumie bwashee
 
Ukiwa hujuwi sheria lazima utakuwa muoga muoga na mwisho we hata nchi hutaweza kuiongoza kwa kufuata sheria maana huzifahamu. Lissu alishasema kisheria huwezi kuanza kampeni mapema wakati hujateuliwa hiyo haiwi kampeni kwakuwa hujaidhinishwa kuwa mgombea hivyo zinakuwa ni ziara za kutafuta tu wadhamini au kuimarisha chama kampeni wanafanya wagombea na sasa bado tume haijateua wagombea. Aelewe sheria vizuri siyo anakuwa muoga muoga. Anaonekana kama anatumiwa ukimsikiliza kwa makini anaombea Lissu akatwe akidhania kuna kosa lolote limekiukwa kumbe hakuna. Kama ni kuenguliwa Magufuli pia itabidi aenguliwe basi maana yeye hakuwa anatafuta wadhamini ila kuhamasisha watu wachague chama chake pia.
Mijitu ina vichwa vikubwa lakini akili matakoni. Logic ndogo tu kampeni inawashinda. Hata baada ya kuwapa ufafanuzi bado hawataki kumuelewa.
 
Huku Lisu naye anaendelea na kampeni zake tu kabla ya muda uliowekwa na tume.

Tume imkate.
 
Subiri mpaka Lisu akatwe ndio utajua kama kuna sheria
Nami ninakumbia TL akikatwa ndipo utakifahamu Chama tawala chenye wasomi walioko mitaani bila kazi ni kipi na chenye watumishi miska 5 hawajapandishwa Mishahara, wafanyabiashara wanaoteseka,wafugaji na wakulima walinaoteseka,watumishi wanaotumbuliwa kila siku na wengine kibao.
 
Mgombea Urais wa chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe amesema wao wamepata wadhamini katika mikoa kumi

Amesema ACT-Wazalenda waliamua kutafuta wadhamini kimyakimya ili kuepuka kuteleza

Majina wa wateule wa kugombea Urais yanatarajia kutolewa na Tume ya Uchaguzi, NEC Agosti 25, na kampeni zitaanza Agosti 26

Source ITV
Hii ni kauli ya maajabu sana aseme ndo utartibu alioona unamfaa basi , kuwepa mtego ina maana gani kwani kutafuta wadhamini openly kuna kosa gani , hata hivyo amekua kwenye serikali ya kikwete ,je kikwete alitafuta wadhamini kwa kificho , na je kuna kanunu yoyote tume inayokataza mtu kutafuta wadhamin openly na kama ametafuta wadhamini kwa kificho vipi tukisema hata hao wadhamin kafoji , angalizo vyama muwe makini na watu kama hawa,kanialibia siku, yani mtu analazimisha mazoea kua sheria very sad
 
Upuuzi mtupu nani aliongea Zanzibar na kusema atawatoa mashehe wa uhamsho akichaguliwa kuwa Rais?

Wanatufanya watanzania wote wapumpavu kama wao.
Kuna kichaa wenu ameshaanza kampeni kabla ya muda, kila siku ,"Risasi, risasi, risasi, sasa sijui ndio maumivu yake yataleta maendeleo!! asubiri kukatwa tu na huyo bwanaake kutoka US anayejifanya anajua kuvuruga amani ya nchi za kiafrika ashafahamika.
 
Mgombea Urais wa chama cha ACT-Wazalendo Bernard Membe amesema wao wamepata wadhamini katika mikoa kumi

Amesema ACT-Wazalenda waliamua kutafuta wadhamini kimyakimya ili kuepuka kuteleza

Majina wa wateule wa kugombea Urais yanatarajia kutolewa na Tume ya Uchaguzi, NEC Agosti 25, na kampeni zitaanza Agosti 26

Source ITV

Ameanza unafiki na kujishuku🤨😏
 
Nayo atuondolee ujinga hapa, mbona Zanzibar walipokelewa kwa maandamano? Kiufupi hatoshei kwa Lissu hata kidogo, ampishe Lissu apeperushe bendera ya wapinzani!
Kaboa zaidi yaani kujinafikisha kujiona yeye mwema anajua Sheria...
 
Back
Top Bottom