Mercenaries kutoka Romania waomba njia Rwanda kurudi kwao

Marie Antoinette

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2019
Posts
426
Reaction score
412
Kundi la wazungu 288, waliokuwa wakioigana vita na M23 upande wa DRC, leo wametolewa kwenye kambi ya MONUSCO huko Goma, kuelekea mpakani mwa Rwanda na DRC. Wakisindikizwa na jeshi la M23, kundi hilo limekabidhiwa serikali ya Rwanda, ambayo itawasafirisha mpaka uwanja wa ndege Kigali, na wanatalajia kuondoka nchini humo leo jioni.

Afrika kusini pia, imeiomba M23 kutowadhulu wanajeshi wake, kwa ahadi ya wao kukusanyika sehemu moja na kutoendelea na vita, wakifanya utaratibu wa kuwarudhisha nchini kwao. Uwepo wao toka mwanzo, ulioingwa na chama cha upinzani, kilichosema hawana vifaa vya kutosha kukabiliana na kundi la M23, na kwamba walichoenda kukifanya ni kulinda mali za raisi tu.

Kwa sasa mipaka ya DRC mashariki mwa Kivu kasikazini inalindwa na M23. Raia waliokuwa wamekimbilia Rwanda, wameanza kurudi majumbani kwao huko Goma.


View: https://x.com/rbarwanda/status/1884556998353486105?s=46
 
Ndio maana Mimi binafsi nilisema kwamba DR Congo kuna Utawala dhaifu Sana ambao umekuwa ukiwabagua baadhi ya Raia wa nchi hiyo waishio maeneo ya pembezoni, hususani upande huo wa Mashariki mwa nchi hiyo ya DR Congo.

That's why Watu na Wakaazi wengi sana wanaoishi kwenye maeneo hayo ya Mashariki mwa nchi hiyo wanawaunga mkono Wapinzani wa Utawala wa nchi hiyo, wanawaunga mkono Waasi.

Ni hatari kubwa sana katika nchi kuwa na kundi kubwa la Watu/Wananchi wengi wa kawaida ambao wanajihisi kwamba wao siyo sehemu mojawapo ya Utawala/Serikali iliyopo madarakani katika nchi yao. Endapo likatokea jambo baya lolote lile kwa Watawala katika nchi, basi Wananchi hao wanakuwa wapo tayari kumuunga mkono adui wa Utawala uliopo madarakani, na mwisho wake matokeo yake yanakuwa kama haya yaliyotokea huko Goma nchini DR Congo
 
Mada nzuri ila inakera inakosa mvuto. Jifunze kuandika bana.... aaarrrrrghhhhh.. Content nzuri ila hujui wapi "l" wapi "r" mpaka mada inakosa ladha..
 
Anaripoti radio rwanda
 
Kongo ina Wapiganaji mahiri sana lakini haitaki kuwatumia, kama mimi nigekuwq ndio Raisi wa Kongo ningewaiingiza M23 wote kwenye jeshi halafu nikawatuma waende kuwaondoa FLDR na Interahamwe waliovamia Kongo baada ya mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 na kuwakabidhi Rwanda.
 
Kama hali ndiyo hiyo basi hata sisi wakwetu tuwaondoe ili wakongo wapambane na hali yao.

Otherwise tutaumia pasipo na sababu wakati wenye nchi yao hawako serious na nchi yao
Tawala za nchi na Serikali kwa ujumla zinapaswa ziepuke Sana kufanya Siasa za Kuwagawa Watu katika nchi. Watawala waache kueneza Propaganda za Siasa za Chuki na kuwagawa Watu kwa misingi ya Ukabila, Udini, Ukanda, Upendeleo, Itikadi za vyama vyao vya Siasa, n.k.
Hivi ndio vyanzo vikuu kabisa vinavyosababisha Vita, Vurugu, umwagaji wa damu na Uhasama usiokwisha katika nchi nyingi sana hapa barani Afrika.
 
Yaani Tshekedi aliingize jeshi la Rwanda kwenye jeshi la nchi yake?....
 
Kumbe ilikuwa kweli kuna mtu aliyeko huko aliniambia hao jamaa wazungu wanavaa full wasionekane kumbe hii vita in deep root
 
Tanzania soon
 
Wewe na imhotep ni wamoja!?..au ni mtu yuleyule?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…