Kwanza polen Sana kwa kuteseka na Uislamu, hakika Uislamu ni Vita kuu ya tatu ya dunia.
Je msingi wa kupinga kushiriki siku hii ni upi?
Ni itikadi kuwa Leo amezaliwa Mungu,tatizo liko hapo Lau ingekuwa Leo kazaliwa Nabii Yesu kusingekuwa na shida,kwasababu Yesu kwetu ni Mtume wa Allah na tunampenda Sana kwasababu itikadi ya kiislamu ni kumuamini Mungu Mmoja,kuamini Malaika wake,kuamini Vitabu vyake na kuamini Mitume wake akiwepo Yesu.
Nadhani mpaka hapo mmepata picha nazungumzia nini hapa.
Sasa baadhi ya waislamu huenda wanasahau juu ya Imani Yao na mafundisho Yao au huenda wanafanya ili kuwafurahisha watu fulani,lakini hatakiwi kuogopwa kiumbe chochote au kufurahishwa kiumbe chochote linapo kuja swala la Imani isipokuwa Mola WA Viumbe wote.
Kwahiyo naomba tuelewe hili,na tuvumiliane , mtuache na itikadi yetu na nyinyi sheherekeeni kuzaliwa kwa Yesu mwokozi wenu.
Kukua ni kukubaliana kutokukubaliana,Maisha ni rahisi Sana kama ukiwa open minded
Msiteseke hata kidogo.
Nawapenda Sana.