Messi akishinda tena Ballon Dior itakuwa ni yale ya upendeleo, mapenzi na favouritism

Messi akishinda tena Ballon Dior itakuwa ni yale ya upendeleo, mapenzi na favouritism

Messi mwenyewe world cup kabebwa na akina mac Allister, Jullian Alvarez na enzo fenandez. Performance ya world cup mbappe alifanya vizuri kuliko huyo andunje.
Huyo messi tuzo moja kampora Iniesta, Nyingine kampora Lewandowski. Balon dor za halali alizonazo hazizidi 3
Maelezo yako yanatofautiana na numbers zao man , hizi stori mnaokotaga kijiweni sio ? Stats zao za world cup mbape kazidiwa sasa sijui mnataka nini wakuu
 
Vigezo huwa vinabadilika mara kwa mara, ili kum-favor jama fudenge au kumkomoa jamaa fulani.

2010, Xavi na Iniesta walibeba kombe la dunia, lakini alobeba Ballon d'Or ni mtu fudenge.

2014, jamaa fudenge angebeba UCL, hata kama basi angepewa yeye tena. Sema ndo hivyo ikampita kushoto.

2018, jamaa fudenge alipoteana. Ilikuwa sazi tuzo anapata jamaa fulani, basi vigezo vikabadikishwa tena akapewa LUKA MODRIC ili kumkomoa jamaa fulani.

2019 si unakumbuka mkuu? Mtu fudenge alibeba hiyo mambo kwa takwimu uchwara? Tukawekewa beki wa kati wa Liver yule, then zikafanishwa assist na magoli na mtu fudenge. BAasi mtu fudenge akapewa.

Matukio ni mengi sana mkuu. Nadhani unakumbuka mwkaa juzi juzi tuu hapo, mtu fudenge alikiri Lewandoski ana deserve Ballon d'Or kuliko yeye.

Ukiyajua haya mkuu, utaendelea kushughulika na mambo mengine.
 
UMEOMBA TAKWIMU MIMI NAKUPA ZANGU, NAOMBA NA WEWE UNIPINGE KWA TAKWIMU SIO MIHEMKO...

HIZI HAPA SABABU KWANINI MESSI ATAMSHINDA HAALAND...

1. Messi Kashinda Kombe La Dunia
- Messi alishinda kombe la dunia baada ya kulisotea zaidi ya mara nne, hili ndi kombe kubwa zaidi duniani, Lakini Haaland hata hakufuzu...

2. Kiwango Cha Messi Kwenye Kombe La Dunia
Pamoja na mwamba jamaa kua na zaidi ya miaka 35 lakini alipambana kufa na kupona kufunga magoli muhimu yaliyisaidia timu kushinda taji... Pia akawa Mchezaji Bora wa Michuano.

3. Msimu Bora Sana Kwenye Klabu yake ya PSG
Pamoja na kwamba PSG ilitolewa mapema kwenye UEFA lakini Messi aling'ara mbele ya lango. Alifunga Goli 38 kwenye michuano yote na assist 25 na kuisaidia PSG kua Mabingwa wa Ufaransa League 1.

4. Haaland alishindwa kung'aa kwenye mechi kubwa.
Kumbuka kuanzia nusu fainali Haaland alishindwa kufunga hata Goli moja hii ilipekea mchezaji mwenzake Rodri ambaye n kiungo kushinda tuzo ya mchezaji Bora wa UEFA mbele ya Haaland ni aibu.. [emoji28]

5. Manchester city walicheza kitimu zaidi.
Ingawa Haaland aliifungia Goli 58 lakini zilitoka na muundo wa uchezaji sio kupambana yeye kama yeye ndo maana baada ya KDB kuumia mwamba kapoteana.....
 
🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣
Man City walicheza kitimu, lakini timu PSG na Argentina zilicheza kutokana na uwezo binfasi wa Messi ama?

Mahaba ni kitu kibaya sana kwa kweli
 
Messi mwenyewe world cup kabebwa na akina mac Allister, Jullian Alvarez na enzo fenandez. Performance ya world cup mbappe alifanya vizuri kuliko huyo andunje.
Huyo messi tuzo moja kampora Iniesta, Nyingine kampora Lewandowski. Balon dor za halali alizonazo hazizidi 3
Jana kama sio juzi uliulizwa na hao kina enzo alvarez na mac allister fundi walisaidiwa na nani bado hujatoa majibu
 
Mtoa mada unasemaje ??
 
Attachments

  • A06FE9BF-08BF-45C0-A0D8-D054D192BB88.jpeg
    A06FE9BF-08BF-45C0-A0D8-D054D192BB88.jpeg
    125 KB · Views: 2
Huu ni unafiki tuu na wewe ni mshabiki wa Ronaldo.

Modric alichukua ballon d'or kwasababu alifika fainali ya kombe la dunia na kuchukua mchezaji bora wa kombe la dunia.

Ndio ule msimu Real Madrid walichukua Uefa lakini Madric hakuwa mchezaji bora kweny kikosi cha Real Madrid, kilichomfanya apewe hio tuzo ni performance yake kweny kombe la dunia.

Ukiachana na kushinda na kuwa best player kweny kombe la dunia, Msimu uliopita messi aliongoza kwa;
-Goal contributions(Goals+Assists)
-most assists
-most complete dribbles
-most playmaking (kampita hadi De Bruyne)

View attachment 2793244

Cha kushangaza Messi akishinda anaitwa Mwizi na anapendelewa lakini wengine wakishinda mnaona sawa, kwann?

Yaan hata Messi angekuwa ana magoli nusu ya aliyokuwa nayo bado Messi angekuwa The best player of time, huwez kupima anachofanya uwanjani, alaf unamfananisha na waviziaji kama hawa.

Angalia hii👇👇👇
View attachment 2793250

wew ni mshabiki lia lia wa kijana Its Penalty for Argentina. Unatia aibu kabisa
 
Maradona, Messi na Ronaldinho ndo wachezaji bora kuwahi kutokea duniani.

Messi ni complete player;
-Second best goal scorer of all time
-Most assists of all time
-greatest playmaker of all time
-Greatest dribbler of all time
- 5th best free kick specialist of all time.
-2 times world cup best player.
-Only football player to win The Laures awards, tena kashinda two times.

Ukiachana na statistics ballon d'or ntajie mchezaji mweny sifa kama hizi, penaldo robot hawez haya mambo.
 
Dogo kwanini unaropokwa tu? Ballon Dior ni individual award ambayo haihusiana na Fifa wala UEFA, ni gezeti la flani nchini France.
Sasa mimi na ww nani anaropoka? Manake nimekuuliza kupitia hoja ulizo unazo zianzisha ww ila hueleweki kama sigara kali, kwa hiyo gazeti hilo halinaga criteria za mshindi wa hiyo tuzo?
 
Toka lini Kombe la dunia likawa lina uzito kwenye Ballondor? Hili ndio swali langu.......
Mechi saba ndio mtu apewe Mchezaji bora wa mwaka? Kuweni serious basi.....

If Ingekuwa hivyo Iniesta Angechukua 2010.
Wewe huna unalojua mzee
 
Toka lini Kombe la dunia likawa lina uzito kwenye Ballondor? Hili ndio swali langu.......
Mechi saba ndio mtu apewe Mchezaji bora wa mwaka? Kuweni serious basi.....

If Ingekuwa hivyo Iniesta Angechukua 2010.
Zidane, De Lima, Canavaro na wengine wengi walipata Ballon d'or after winning world cup!
 
Ebu kabla haujaanza kubishana kwa sababu ushabiki wako kwa Messi, nipatie stats au details za kiwango bora(zaidi ya kushinda kombe la dunia ) ambazo zitamfanya Messi awe tena mshindi wa ballon dior.

Ni issue tu ya mapenzi tu kwa huyu jamaa ndio maana tena atabeba lakini kuna watu lukuki wamefanya vyema zaidi yake kwa kipindi hichi.
View attachment 2792549
Na hyo tuzo itapoteza hadhi yake Kwa kuendekeza upuuzi.
 
Ebu kabla haujaanza kubishana kwa sababu ushabiki wako kwa Messi, nipatie stats au details za kiwango bora(zaidi ya kushinda kombe la dunia ) ambazo zitamfanya Messi awe tena mshindi wa ballon dior.

Ni issue tu ya mapenzi tu kwa huyu jamaa ndio maana tena atabeba lakini kuna watu lukuki wamefanya vyema zaidi yake kwa kipindi hichi.

Wewe waona nani mwingine zaidi yake anastahili na kwa nini?

Mimi naona Messi na CR7 wamefanya standard za mchezaji bora kuwa juu sana, na katika kizazi hiki cha sasa hakuna mtu ambaye kaweza fikia nusu ya uwezo wa hao jamaa...
 
Back
Top Bottom