Hata Sheikh wetu nchini Tanzania, mwanazuoni Sheikh Abuu Iddi ambaye ni Msaidizi wa Mufti wa Tanzania aliwahi kuonya juu ya dhehebu moja kuanza fitna, misuguano, kutishiana n.k dhidi la dhehebu jingine, wakati wote ni dini moja ya ki-Islamu..
19 January 2023
Dar es Salaam, Tanzania
SHEIKH ABUU - HATARI INAKUJA TUSIPOTOA TAHADHARI KWA HAYA YANAYOENDELEA
Sheikh Abuu Iddi ambaye ni Msaidizi wa Mufti wa Tanzania ametoa tahadhari hiyo kwa kuwa inaweza kupelekea amani kuvunjika nchini Tanzania.
Sheikh Abuu Iddi CV (wasifu) yake imesheheni nyadhifa kadha wa kadha sawia na maktaba yake binafsi iliyosheni mabuku juu ya mabuku ya elimu duniya na ilm ya dini pia ktk utumishi ulitukuka kwa dini na jamii.
Pia sheikh Abuu Iddi ni imamu mkuu msikiti wa Masjid Mnyamani Buguruni jijini Dar es Salaam. Pia kwa miaka 16 amekuwa akiendesha kipindi ktk kituo cha televisheni cha Channel Ten kutoa daawa na darsa, mratibu Al Risala Foundation, Mratibu wa Kudumisha Amani katika mkoa wa Dar es Salaam, Mwandishi wa kitabu kinachokwenda kwa jina Misingi 15 ya amani, mwandishi wa makala katika gazeti kubwa la Mwananchi pia ni Mshauri wa dini na jamii wa Mufti Mkuu wa Tanzania.
Sheikh Abuu Iddi ameelekeza tahadhari hii hususan kwa madhehebu ya Sunni Saudia na Shia linaloegamia Iran yanayo shambuliana kupitia propaganda kutoka maeneo mbalimbali ya dunia ya mitandao ya kijamii wakiongozwa na viongozi wao wa ndani na nje ya nchi kuchochea misuguano