Meya wa Jiji la Arusha, Kalisti Lazaro ahamia CCM. Awashutumu CHADEMA kumkataza kutoa ushirikiano kwa viongozi wa Serikali

Meya wa Jiji la Arusha, Kalisti Lazaro ahamia CCM. Awashutumu CHADEMA kumkataza kutoa ushirikiano kwa viongozi wa Serikali

Wanaume sasa hivi wamebaki wachache sana sijui kwa nini jamani, yaani hawa kina Kalist wameamua kuwa VI ben ten wa ccm njaa ya madaraka ni mbaya kuliko utapiamlo, fika salama mkia wako utaokotwa na mbwa..
 
Meya wa Jiji la Arusha (Chadema), kalisti lazaro leo Novemba 19, 2019 amekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi

Amesema amefikia uamuzi huo baada ya kupitia wakati mgumu kutoka kwa uongozi wa chama chake ikiwamo kupokea barua za onyo mara kwa mara ambazo zilimtaka kutokutoa ushirikiano kwa viongozi wa Serikali ambao anatakiwa kufanya nao kazi ngazi ya Mkoa na Wilaya na kutompongeza hadharani Rais Dk. John Magufuli.


Kalisti Lazaro amenena kwamba,
"Nimekuwa nikifanya kazi katika mazingira magumu nakutana na changamoto, nimeshletewa barua nyingi za onyo kwa sababu ya kumsifia Rais, lakini pia siwezi kukaa chama ambacho kimejitoa kwenye Uchaguzi, leo Arusha inaenda kuwa ya CCM sababu wenzetu wamejitoa."

"Nitaendelea kuwa Mwanasiasa kwa sababu niwaombe wananchi wa Kata yangu, nitaendelea kuwatumikia kwa nafasi nyingine ambayo chama changu itaamua mimi nirudi"

Pia soma


Welcome son, come back home a "prodigal son".
 
Duh.. Kumbe ni wajinga hivyo?
Nilifikiri wakitishiwa wanatoka hadharani ili dunia na watz wajue mbivu na mbichi.
. Kwahiyo kumbe hata wakipewa nchi wakitishiwa tu wanatuuza hata sisi watz tukiwa ndani na hai kabisa?
hahaa kwamba wakitishwa na RC na polepole wanaogopa wanasarender
wakipewa waongoze nchi halaf watishwe na Trump, Xi jiping au Putin itakuwaje [emoji23][emoji23][emoji23]
 
CCM impe ugombea ubunge Arusha mjini Ni meya pekee wa upinzani aliyekuwa akitoa ushirikiano kwa serikali kwa Maendeleo ya jiji lake.

Kama sivyo agombee udiwani awe meya Tena ubunge apewe Profesa Ole Gabriel
Wanapewa au wanashiriki kwenye mchakato mzima wa uchaguzi!!!!!!!
 
Wanaume sasa hivi wamebaki wachache sana sijui kwa nini jamani, yaani hawa kina Kalist wameamua kuwa VI ben ten wa ccm njaa ya madaraka ni mbaya kuliko utapiamlo, fika salama mkia wako utaokotwa na mbwa..
Ila wakihamia chadema mnawapa majina matamu ,wakihama mnawawapa majina mabaya

Achen ujinga
 
Ila wakihamia chadema mnawapa majina matamu ,wakihama mnawawapa majina mabaya

Achen ujinga
Sio ujinga ila ndio ukweli, na kuhama ni haki ya kila mtu aende salama, ila historia ndio haifutiki na kuhama hama ni tabia yake..anatafuta maslahi una fikiri kwa nini hakwenda ACT, TLP kama kahama kwa kuwa kachoshwa na CHADEMA? pesa ndio msingi wa maendeleo inategemea unaitafuta vipi.,
 
SABABU ZA KUHAMA HAWA CHADEMA KUJA CCM ZINATOSHELEZA?

Na Thadei Ole Mushi

Nimesikiliza clip ya Mh Lazaro kuhamia CCM, ametoa sababu kuwa anahamia CCM kwa sababu akiwa Chadema alikuwa akisifia serikali anaandikiwa barua na kuonywa. Hii ndio sababu kuu ya kuhamia CCM.

Sijui ni Lini hawa watu wataona Vision aliyonayo Mh Rais, Rais hahitaji wasifiaji zaidi ya waliopo sasa, Rais anahitaji watu watakaowaza na kuleta Solutions za matatizo yanayomfanya asilale usiku. Yaani mtu anahamia CCM ili apate nafasi ya kuja kusifia, kwa kuwa huko aliko alinyimwa kusifia, what a shame!!!!
Kila siku nalia hapa wanaotaka kukaa karibu na viongozi wetu hasa Rais lazima wawe na akili Daraja la kwanza kabisa. Ni Mali ya Rais, hizi akili za kusifia tu Mimi bado sijaona kama zitatusaidia sana.
Leo Lazaro angetulaza na viatu kama angelionyesha ni changmoto gani zipo Arusha na anatoa na "HOW" katika kuzitatua. Angetuambia masuala ya Utalii tunafeli wapi, ajira kwa vijana anawagusaje, Kupangika kwa jiji la Arusha atafanyaje, na ataongezaje Pato la Jiji la Arusha kwa mtu mmoja mmoja na kwa ujumla kwa jiji zima. Tulihitaji kujua population ya Arusha ni watu wangapi je wanakasoro maji kiasi gani atafanya nn baada ya kuhamia CCM je Elimu ipoje yaani hapa ungenipa muda wa kumwandalia Speech huyu jamaa ya kuhama ningewalaza na viatu kwa statistics na solutions.
Sio mtu anahama kwa sababu ya kunyimwa kusifia.... Mtanisamehe kidogo wana Wana CCM. Wanaccm wenzangu tusiogope kujadili Hili kwa kuwa hawa wanaohamia na sisi ndio Rasilimali watu muhimu kabisa kwenye chama. Hakuna chama bila watu na hakuna watu bila kichwani kuwa smart
Karibuni jalalani....
 
Ngoma inogile, Lema ,mtu wa CCM utakaye pambana nae kwenye kinyanganayiro cha ubunge 2020 kupitia tiketi ya CCM ni huyu Kalisti, piga ua na atakutoa nokauti.

Mpaka tunafika 2020 penye uhai ni bora usigombee kutunza heshima yako.
Mambo ni magumu sana
Duh wewe hujui siasa za Arusha
 
Nimecheka sana, yaani mtu anahama alafu bado anawaza kuiongoza Tena hiyo kata!, Inamaana ccm hakuna watu wenye uwezo wa kuiongoza hiyo kata mpaka yeye tu, mimi nadhani itoshe Sasa watu kuwamia ccm kwa lengo la kupata vyeo, wanna ccm amkeni haiwezekani mkitumikie chama miaka yote hiyo alafu mwisho wasiku anatokea mtu anahamia huko kwa ahadi ya zawadi ya cheo, huku nyinyi mliokipigania chama mnaishia kuvaa sare mitaani[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23]
Yaani CCM ni chama cha ajabu sana, nguvu wanazozitumia kupata uungwaji mkono ni sawa na mtu anayepulizia Airfreshner ili kuondoa harufu ya choo.
 
Back
Top Bottom