Meya wa Jiji la Arusha (Chadema),
kalisti lazaro leo Novemba 19, 2019 amekihama chama hicho na kujiunga na Chama cha Mapinduzi
Amesema amefikia uamuzi huo baada ya kupitia wakati mgumu kutoka kwa uongozi wa chama chake ikiwamo kupokea barua za onyo mara kwa mara ambazo zilimtaka kutokutoa ushirikiano kwa viongozi wa Serikali ambao anatakiwa kufanya nao kazi ngazi ya Mkoa na Wilaya na kutompongeza hadharani Rais Dk. John Magufuli.
Kalisti Lazaro amenena kwamba,
"
Nimekuwa nikifanya kazi katika mazingira magumu nakutana na changamoto, nimeshletewa barua nyingi za onyo kwa sababu ya kumsifia Rais, lakini pia siwezi kukaa chama ambacho kimejitoa kwenye Uchaguzi, leo Arusha inaenda kuwa ya CCM sababu wenzetu wamejitoa."
"
Nitaendelea kuwa Mwanasiasa kwa sababu niwaombe wananchi wa Kata yangu, nitaendelea kuwatumikia kwa nafasi nyingine ambayo chama changu itaamua mimi nirudi"
Pia soma
Meya wa Jiji la Arusha Mheshimiwa Kalist Lazaro amemuomba mkuu wa Mkoa wa Arusha amualike Mheshimiwa Rais John Pombe Magufuli jijini Arusha ili aje kupokea Shukrani na pongezi badala ya malalamiko. Meya Lazaro ametaja baadhi ya miradi ya mfano na mafanikio iliyofanywa na Serikali jijini Arusha...
www.jamiiforums.com
Mpasuko ndani ya chadema. Huko Arusha Meya wa Arusha Kalisti Lazaro ambaye pia alikua ni Katibu wa chadema wa mkoa amevuliwa uongozi huo Jana jioni Ikumbukwe Kalisti Lazaro alikuwa mwiba mkubwa kwa marehemu Ndesamburo katika kinyang'anyiro cha uenyekiti wa kanda ya kaskazini,'ujenzi Mnara wa...
www.jamiiforums.com