Mfahamu Meja Jenerali Muhiddin Kimario. Ukisikia mzalendo ndio huyu

Mfahamu Meja Jenerali Muhiddin Kimario. Ukisikia mzalendo ndio huyu

Mzalendo anaenda kuuwa ndugu zetu waganda wakati Nyerere kaiba Mali za umma na kutunga katiba mbovu yakumlinda yeye .
Nyerere alitunga katiba feki ili imlinde na kuanzisha vita Uganda ili kumfurahisha na kumrudisha madarakani best yake Obote! askari wetu wengi wakafa bila hatia!! mara Mwalimu akaanzisha vita vya ukombozi Afrika nzima na kuharibu rasilimali za bongo bila ridhaa ya wananchi lengo ni kutafuta sifa za kijinga ili yeye na Kwame Nkrumah wapewe uongozi wa serikali ya Afrika!!

Mwalimu akaanzisha ujamaa ili nchi ibaki maskini wabongo wamtukuze yeye tu daima na watu wengi waliliwa na simba walipohamishiwa maporini eti kuanzisha vijiji vya ujamaa akaona haitoshi akashikia bango kiswahili na kuua lugha ya malkia ili wabongo washindwe kuwasiliana na watu wa nje wakamkimbia!! na hadi leo nchi imebaki kisiwa wachache wanaojua English ndio huweza kwenda nje sote tunazaliwa na kufia hapa hapa!! hata mkulima kuwasiliana na masoko lukuki ya nje hawezi!!

ukisoma vizuri ujamaa unaona kuwa ni mfumo usiofaa na yatakiwa nchi ichukue ubepari kwanza ikishaendelea labda ndio inaweza kuhamia ujamaa, mawazo ya kina Mwalimu ndio yameifanya Afrika kubaki nyuma kimaendeleo ukienda ulaya huamini maendeleo unayoyaona!! unabaki kujiuliza hivi sisi tumekwama wapi?

kwa wasiojua vizuri ujamaa ni mfumo unaopingana na human nature sababu mwanadamu ni selfish by nature na daima hutaka kujiendeleza mwenyewe na familia yake kwanza sasa ujamaa unamtaka mtu kujikana na kujali maslahi ya nchi kwanza kitu kisichowezekana na hivyo watendaji kuishia kuiba mali ya umma na kuifilisi nchi kama serikali ndio inashika njia kuu za uchumi, ni afadhali ya ubepari unaowapa raia umiliki wa uchumi kwa sehemu kubwa na kuilipa kodi serikali na hapo watu hawawezi kujiibia wenyewe!! kwakuwa watu hawajiibii basi shughuli za kiuchumi wanazomiliki na kushindania soko basi hupata faida kubwa na kuilipa serikali kodi kubwa inayojenga miundombinu ya nchi kwa spidi ya rocket!!

basi mzee wa watu aka Mwalimu akajifia bila kumuona rais wa awamu ya tano kama alivyotuahidi akaja fisadi Chenge akaifanyia marekebisho katiba ikawa chuma cha pua cha kumchapia bakora heavy raia wa bongo! katiba ikaondoa mamlaka yote ya raia, ikautengeneza uchaguzi usio huru wala haki kuwapa rungu wakurugenzi kuamua mshindi na hapo kuhakikisha ushindi ni wetu siku zote!! shame on Chenge lile zee fisadi limesahau kifungu lilichoandika lenyewe likiwa ndio mwanasheria mkuu kinachosema mali za watanzania zitatumika kuwanufaisha watu wote basi Zee likajigawia mgao wa escrow bila aibu!!niliumia sana roho mchungaji kaiba sadaka!!
 
R
Nadhani umekosea kwa bahati mbaya kuandika Shamim, ni Tamim. Ni kweli jamaa alipitia kipindi kigumu baada ya vita. Alikua ni askari mwaminifu na mtiifu kwa jeshi na nchi yake na alikua amepigana vita ya Uganda akiwa ni miongoni mwa makomandoo wa Tanzania waliotoa mchango mkubwa sana kwa ushindi wetu dhidi ya Amin.

Miaka miwili baada ya vita yaani 1981 alitumwa kwenye mission fulani nyeti nje ya nchi. Kwa kifupi mission ile haikua inajulikana na uongozi wa juu kabisa wa nchi. Kukawa na fununu kua waliomtuma walikua mbioni kuteuliwa kwenye nafasi kubwa sana jeshini na wakati huo kukawa na tetesi pia za malalamiko za hiyo nchi alipokwenda Tamimu kwenye operation aliyotumwa.

Kilichotokea ni kwamba hao waliomtuma kwa hofu ya kukosa nafasi kubwa za uteuzi wakiamini mamlaka ya uteuzi itachukizwa na operation ile wakamkana Comandoo Tamim kua hawakumtuma na kwamba eti ALIASI JESHI!!!! Commando Tamim akakatiwa support aliyotakiwa kupewa akiwa huko na akjikuta akiwa vulnerable huku akisakwa na kuwindwa kama digidigi ili kuuwawa huko alipotumwa. Ni kwa mbinu zake, juhudi na mafunzo aliyopewa ndio akaweza kutoroka na kurudi Tanzania

Aliporudi hakuamini kikichotokea. Alikutana na mashtaka ya uasi na kupelekwa court martial!!! Kifupi aliondolewa jeshini kwa dhulma na alijua na sababu za kuamini kwamba hata hapa kwenye nchi aliyoioenda sana alikua anawindwa auwawe! Kwakweli ilimchanganya sana. Inawezekana hii ndiyo ilisababisha ikawa rahisi Comandoo Mohamed Martin Tamimu kushawishika kuingia kwenye njama chafu na ovu za kutaka kupindua serikali. Ni kweli pia yote aliyopitia haihalalishi yeye kuingia katika njama za uhaini na kosa lake liko palepale lakini fact ipo palepale Tamim aliuzwa na kusalitiwa na wenye tamaa ya madaraka na wakamnyima fursa ya kuitumikia nchi yake ambayo miaka michache tu iliyopita alijitoa muhanga kufa uwanja wa vita akiitetea

Ama kuhusu shahidi X na shahidi Y ni kwamba mmoja ameshatangulia mbele za haki na mwingine ni yule aliyemfyatulia risasi Tamimu sina hakika kama alishapona maradhi yake yaliyomfanya awe kwenye coma kwa muda mrefu
Roho za waganda ndo zilimtesa alienda kuua ndg zetu waganda bila sababu za muhimu.
 
Pichani ni Marehemu Major Generali Muhiddin Kimario, ni moja kati ya mawaziri wawili tu waliowahi kudumu katika nafasi zao za wizara ya mambo ya ndani kwa muda wa miaka mitano (5) katika Historia ya Tanzania.

Mwaka 1978 alitumwa kwenda mkoani Mwanza na Mwalimu Nyerere kwenda kuwaaga Wanajeshi waliokuwa wanakwenda kupigana Vita vya Kagera kumn'goa Idd Amin Dada, wakati akitoa Hotuba yake ndani ya Viwanja vya Nyamagana ghafla aliamua kujivua uwaziri na kuamua kwenda vitani "Mkuu wa Mkoa ninaomba ufikishe taarifa hii kwa mh Rais kwamba najivua Uwaziri na ninaamua kurudi jeshini kuungana na wenzangu leo kwenda kumshikisha Adabu Amin"

View attachment 1498576
Mengi yaliyoandikwa huku sio sahihi.
Vita vya Kagera Kimaryo alikuwa RC Mwanza
Kimaryo amekuwa Waziri wa home affairs kwa ten years
Aliingia vitani na akapewa jina la kamanda Mbogo
 
Huu nao ni uwongo mwingi sana. Ni kweli Tamimu aliuwawa Kinondoni kutokana na uhusika wake katika njama za kupindua serikali mwaka 1982; hakuuzwa bali alijiunga na akina Zakaria Hanspope, Uncle Tom, Badru Kajaja na wengineo katika njama za kutaka kuipindua serikali kutokana na maisha magumu yaliyofuatia baada ya vita.

Tanzania ya leo tumelogwa nini kuamini hizi conspiracy theories kupita kiasi?
Anaye msema yeye si tamimu, Ni komando mwingine ambaye mwisho wake ulikuwa Mozambique kwa Joachim Chissano
 
Amefariki 2005, ila Kisa chake cha kusikitisha ndio hiki
Kuna askari wengi waliokuwa mstari wa mbele wanasema Lupogo alishindwa KABISA kuendesha vita na kurudishwa makao makuu. Kikosi chake cha 205 kuchukuliwa na Kimario. Kimario aliendesha mapigano makali na kikosi chake cha 205 kiliweza kukata katikati ya Uganda mpaka Nimule kwenye mpaka wa Uganda na Sudan. 205 ndiyo kikosi kilichopoteza kifaru kimoja baada ya mapigano makali ya masaa 8 ili kuteka daraja muhimu la Maporomoko ya Karuma Kwa maajabu,Mwl Nyerere alimpandisha cheo Lupogo kuwa Meja Jenerali na kumuacha yule aliyepiganisha vita na kushinda Kimario. Wewe jiulize inakuaje aliyeshindwa vita kupandishwa cheo na yule liyeshinda kuachwa mpaka alipopandishwa cheo na Rais A.H Mwinyi.Hizo ndizo changamoto za Mstari wa mbele walizokuwa wanazipata wapiganishaji wetu
Muhidini kimario sio kwamba aliachwa na nyerere kutopandishwa cheo sababu alikuwa Muislam???
 
Simulizi nzuri, wakuu legezeni hizo code kidogo na sisi kizazi kipya tupate kuelewa historia ya mashujaa wetu.
 
Mzalendo anaenda kuuwa ndugu zetu waganda wakati Nyerere kaiba Mali za umma na kutunga katiba mbovu yakumlinda yeye .
hujielewi na inaonekana hata historia ya nchi hii na vita vya kagera hauelewi
 
Pichani ni Marehemu Major Generali Muhiddin Kimario, ni moja kati ya mawaziri wawili tu waliowahi kudumu katika nafasi zao za wizara ya mambo ya ndani kwa muda wa miaka mitano (5) katika Historia ya Tanzania.

Mwaka 1978 alitumwa kwenda mkoani Mwanza na Mwalimu Nyerere kwenda kuwaaga Wanajeshi waliokuwa wanakwenda kupigana Vita vya Kagera kumn'goa Idd Amin Dada, wakati akitoa Hotuba yake ndani ya Viwanja vya Nyamagana ghafla aliamua kujivua uwaziri na kuamua kwenda vitani "Mkuu wa Mkoa ninaomba ufikishe taarifa hii kwa mh Rais kwamba najivua Uwaziri na ninaamua kurudi jeshini kuungana na wenzangu leo kwenda kumshikisha Adabu Amin"

View attachment 1498576
True son of the land,
Wazalendo wa siku hz ni wale wanaomsifia Maghu tu,na wanaovaa kijani,
 
Kuna kisa kingine cha kusikitisha cha jamaa mmoja alikua Captain wa Jeshi akiitwa Mohamed Martin Tamimu(Comandoo). Huyu aliuzwa vibaya sana kwa kupelekwa nje ya nchi kufanya kazi ambayo yeye akiamini ni yakulitumikia taifa.

Yalitokea mambo kadhaa. Waliomtuma wakamgeuka na kumruka, akawa adui wa huko alipotumwa na adui wa nchi iliyo mtuma! Akajikuta analazimika kuingia kwenye uasi/uhaini na aliuwawa pale Kinondoni Mkwajuni kwa kufyatuliwa risasi na mwanasiasa maarufu sana hapa nchini ambaye habari zake za mwisho alikua upinzani
Alikuwa dini gani
 
Hii nayo ni uwongo mtupu; Muhidini Kimario baada ya vita alikuwa waziri wa mambo ya ndani kuanzia mwaka 1983. Hata ukienda tovuti ya Wizara hiyo utakuta kuwa yeye aliendelea kuongoza wizara hiyo hadi 1988, yaani miaka kumi baada ya vita.

Hizi conspiracy theories mnazitoa wapi?
Gen Kimario alikuwa mpiganishaji wa vita alichomaanisha mwandishi Kimario alitakiwa apandishwe cheo cha kijeshi kama ilivyokuwa kwa wapiganishaji wenzake mambo ya uwaziri yalikuwa ni ya ziada tu. kutokumpandisha cheo na kumpandisha aliyeshindwa haikuwa sawa
 
Amefariki 2005, ila Kisa chake cha kusikitisha ndio hiki
Kuna askari wengi waliokuwa mstari wa mbele wanasema Lupogo alishindwa KABISA kuendesha vita na kurudishwa makao makuu. Kikosi chake cha 205 kuchukuliwa na Kimario. Kimario aliendesha mapigano makali na kikosi chake cha 205 kiliweza kukata katikati ya Uganda mpaka Nimule kwenye mpaka wa Uganda na Sudan. 205 ndiyo kikosi kilichopoteza kifaru kimoja baada ya mapigano makali ya masaa 8 ili kuteka daraja muhimu la Maporomoko ya Karuma Kwa maajabu,Mwl Nyerere alimpandisha cheo Lupogo kuwa Meja Jenerali na kumuacha yule aliyepiganisha vita na kushinda Kimario. Wewe jiulize inakuaje aliyeshindwa vita kupandishwa cheo na yule liyeshinda kuachwa mpaka alipopandishwa cheo na Rais A.H Mwinyi.Hizo ndizo changamoto za Mstari wa mbele walizokuwa wanazipata wapiganishaji wetu
Msiwasahau wapiganaji wenyewe.
 
magenerali wapumzike, leteni sifa za makoplo na masagent, msiwasahau.
 
Kwa hiyo unataka kusema kuwa Shamim alizwa baada ya vita ndipo akaamua kuja kujiunga na njama za mapinduzi? Halafu tunaposihana katika mswala haya jitahidi pia uniambia kama unawajua shahidi X na shahidi Y kwenye kesi ile ya uhaini ya mwaka huo. Hapa kuna vitu vingi sana vya kusimuliwa ambavyo havilingani na rekodi zenyewe halisi.
Ni tamim mkuu. Shamim ni mwanamke
 
Back
Top Bottom