MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,775
- 71,893
- Thread starter
- #41
The Rashidun Caliphate imenikumbusha kuuwawa kwa kiongozi wa Dola ya Kiislamu Swahaba Uthmaani ibn Affaan (RadhiyaAllahu 'anhu) kulileta matatizo na mgawanyiko mkubwa katika Umma na athari zake mpaka Leo zimeathiri Uislamu
Ali alijichanganya kutowakemea wafuasi wake baada ya kumuua Uthaman. Yeye akadhani atatawala kirahisi huku kina Muawiya ndugu wa Caliph Uthman wanaangalia tu. FITNA ikaanza na uislamu ukagawanyika mpaka leo. The Rashidun Caliphate ikaanguka, The Ummayed Dynasty ikazaliwa na matatizo hayakuisha hapo. The Ummayed Dynasty ikaja kupinduliwa na Abbassid Dynasty ambapo alipona Abdulrahman peke yake kujificha Spain.
Baada ya The Rashidun Caliphate kuanguka, hakujawahi kutokea tena duniani dola la kiislamu lililowahi kufanya vizuri tena kuwaunganisha watu wa makabila yote chini ya bendera moja. The Ummayeds ndiyo waasisi wa siasa za Uarabu na Weusi, ambazo zilipelekea wakapoteza majimbo yao makubwa barani Afrika.
Ila yote haya yalianza na kifo cha kinyama cha Caliph Uthman. Huwezi kufanya fitna kwa kiongozi mkubwa wa nchi halafu ufikirie yameisha tu. Hapa Tanzania ni suala la muda tu, wewe subiri utashuhudia mazito.