Mfalme ‘akiuawa’ huwa inachukua muda mrefu sana Taifa kupona

Aisee.

Baada ya kupata Uhuru,
Baadae miaka 4 , pakatokea mapinduzu yasio fanikiwa, mwalimu akawalaumu wa Tanganyika kwa ujumla wake kwamba wamelitia aibu Taifa kidunia. Wakati mapinduzi yalifanywa na wanajeshina sio raia.
Hawa wanamapinduzi walikuwa wanataka Hali Bora ya maslahi ya KAZI na maisha Bora,

Baada ya hapo mwalimu akaleta ujamaa na kujitegemea kama hali ya tahadharu na kujijenga kijasusi zaidi, ila hakufanya maridhiano ya kitaifa.

Kwa hiyo tatizo la maslahi ya maisha Bora Kwa wananchi halikutatuliwa bali ujamaa ndio ulikuja kuwapokonya hata kile kidogo walicho kuwa nacho refer kuwawa kwa RC wa iringa.

Kwa hiyo mwalimu akazidi kujiongezea maadui zaidi, imagine BiBI Titi alipewa kifungo kirefu gerezani .

Lengo la kudai Uhuru wa Tanganyika ilikuwa ni lengo la kuwajengea uwezo wananchi kujitegemea hasa kiuchumi, na hilo mwalimu hakulitimiza kabisa 😂.

Ndio Kwanza wa uk wakafukuzwa na akawabakisha wa Asian kama ndio ma mentors wake wa kiuchumi,fedha, refer Jamal.
Baade mwalimu aliwaandikia kitabu kuwalaamu wa Asia kuwa ni wanafiki🎯

Ndio ni kweli mwalimu alijenga viwanda vingi sana , lakini wananchi hawakuwa na purchasing power,
Kumiliki TU gari ilikuwa ni mtiti unaonekana wewe ni mwizi wa mali za umma, sasa general Tyre watawauzia matairi watemebeza mikokoteni.

Viwanda vya bia vilikuwa hoi , ambavyo ndio injini ya mapato ya ndani , kunywa bia ilikuwa ni anasa , watu wanaishia kunywa ulanzi, mbege etc.

Kwa hio mwalimu kwa miaka yote ya utawala wake alikuwa akigombana na wapigania uhuru wanaodai maslahi ya kumiliki uchumi wa Nchi.

Kwa hio wananchi na viongozi lazima mutambue kuwa maslahi ya wananchi Kwanza.
Nilishangaa sana kwenye rasimu ya katiba ya warioba eti wanataka serikali 3, ndio maana alichezea mabanzi.

Usalama nao ni kama kuna shido mahali, ina maana walishindwa kumwambia mwalimu ukweli kuwa wa Tanganyika wanadai maslahi ya kiuchumi,👈 unafiki,fitina, ujinga vilianzia hapa
 
Umewaza vyema
Japo nilikuwa sijazaliwa kipindi hiko 1995 ila Kuna video ipo kwenye simu yangu nimecheki tukio zima la kuchangia mgombea wa Uraisi Dodoma kwa muhtasari na nimegundua mengi baada ya kusikiliza hotuba ya Mwinyi siku hiyo , Nyerere na baada ya matokeo Kikwete alishangiliwa sana na wajumbe kama mshindi vile na alitoa hotuba nzuri sana mpaka ukumbi mzima ukasimama kupiga makofi.

Alichosema kwenye hotuba yake nimelink na alichokisema kwenye Yanga day Moja kipindi hiko Yanga wanalia Lia kufanyiwa hujuna na Simba kumuiba mchezaji wao Bernard Morison ambapo alisema hivi "haina haja ya kulalamika Wala kulia kama wao wameiba mchezaji wenu muhimu na nyinyi tafuteni wa kwao mulipe kisasi kesi inaisha sio kulilia "

Nikagundua yeye ukimfanyia ubaya atacheka tu hana maneno mengi wala kuonyesha wazi nia ya kufanya ubaya anatulia benchi na kupanga kete zake kwa utulivu mkubwa Kisha wewe utajipa matumaini mwamba karelax kapuuzia hana mbaya kumbe pumzi ya moto inakuja kimya kimya .

Rais wa Egypt Anwaar Sadat aliitambulisha hii mbinu katika vita ya Yom kippur dhidi ya Israel inaitwa " Sedation " aliwapumbuza Israel kuwa anataka Amani na kwenda Marekani kuomba mazungumzo huku anafanya maandalizi makubwa ya kuishambulia Israel kwa usiri na umakini mkubwa wakati huo MOSSAD na CIA walijiamisha kuwa Sadat Hana uwezo wa kuishambulia Israel hata kwa miaka kumi ijayo matokeo yake Israel akipata aibu kubwa kwa suprise attack .

Allen Kilewella
 
Kaka RRONDO nimefurahi sana kukuona mzima. Juzi hapa nilitaka hadi kuanzisha uzi kuuliza kama uko salama. Kukuona hapa mzima napata faraja.

Kiufupi ni kwamba MUDA NI MSEMA KWELI hasahasa kwa kinachoendelea kipindi hiki. CCM wanaweza kudhani tatizo lao ni Samia na akitoka nchi itatulia kumbe wapi. Matatizo ni makubwa mno na yana mzizi mrefu.
Siasa za 2015-2021, zilichangwa vibaya mno kwa kuangalia matumbo na leo. Hawakuzingatia kesho kitatokea nini.

I hope I'm wrong, lakini Tanzania yetu is headed for a very bigger crisis. Mbaya zaidi ni kwamba baadaya Mzee Mkapa kufariki nchi imekuwa haina BABA MLEZI ambaye anaweza kusema au kukemea kitu na watu wote wakaacha na kuogopa.
​
Mkuu naamini unatueleza kuwa si Kaisari maana hakuwa anaangalia tumbo lake. Ila ni wabaya wake ambao baada ya kumg'atua wakaanza kuibebena nchi kiuroho bila aibu
 
Inaoneka ya mwaka 1995 mwamba alivyonyimwa ilimuama sana akajiapiza kuwa Mafia maana yeye ndiye alikuwa na ushawishi mkubwa na kukualika zaidi kipindi hiko kushinda mpinzani wake ila matokea yakaja ndivyo sivyo akaona kumbe kuwa kinyonge hakuna maana kabisa
Kuna mambo machachache hapa:

Mosi, najiuliza kama angekuwa Raisi 1995 wakati wakubwa wapo, Je angefanya yale ambayo aliyafanya baada ya 2005. Angepewa Uraisi mwaka 1995 bila shaka MTANDAO usingekuwepo, kama ungekuwepo basi ungekuja kivingine kabisa.

Pili, angeupata uraisi mwaka 1995 kuna uhakika gani kwamba angeongoza nchi vizuri ? Lazima tukubaliane kwamba unaweza ukakipenda kiti cha Uraisi hata kukikalia lakini chenyewe kisikupende. Wengi wanakalia viti visivyo vyao. Uraisi siyo asali kwamba kila mtu lazima alambe.

Tatu, angeupata Uraisi kidemokrasia mwaka 1995 basi Tanzania na CCM tungekuwa tumepiga hatua kubwa mno kidemokrasia. Hili lingeweza kutusaidia kujenga taasisi za kuweza kuwawajibisha viongozi pale wanapokosea. Kama aliingia kidemokrasia basi ni rahisi kumtoa kidemokrasia.

Nne, kama demokrasia ingechukua mkondo wake mwaka 1995 na Cheki-Bobu kushinda, sidhani kama angeshinda uchaguzi mkuu dhidi ya Augustino Mrema. Mwaka 1995 kulikuwa na matatizo mawili. Demokrasia ndani ya chama ilivurugwa na demokrasia katika ngazi ya kitaifa ilivurugwa pia.

Yote haya ni Hypothetical Could Have Beens...Tunachokifahamu ni kwamba Uraisi aliupata na akavurunda sana. Yeye ni moja kati ya watu ambao historia ya nchi hii itamhukumu kwa vizazi vingi sana vijavyo. Alikuwa na nafasi ya kufanya vizuri. Aliachiwa nchi iko kwenye hali nzuri sana lakini akaharibu kila kitu.
​
 
Hapo kwa Kenya wana mzimu wao wa makamu wa rais tangu nchi kupata uhuru mpk rais aliyepo leo kila wakishika nchi lazima agombane na kaimu wake,,
Dhambi ya 2021 itaitafuna nchi,, ni mtafunano
Kenya wanavuna waliyoyapanda. USALITI na KUENDEKEZA UKABILA.

Kenyatta alimgeuka Odinga jambo ambalo mpaka leo linaleta taharuki kubwa.

Baadaye Moi akaanza kuvuta na Kibaki hivyohivyo.

Baadaye Kenyatta Jr na Odinga Jr wakaliendeleza na mpaka leo ushakuwa utamaduni.
​
 
Kiufupi ni kwamba MUDA NI MSEMA KWELI hasahasa kwa kinachoendelea kipindi hiki. CCM wanaweza kudhani tatizo lao ni Samia na akitoka nchi itatulia kumbe wapi. Matatizo ni makubwa mno na yana mzizi mrefu. Siasa za 2015-2021, zilichangwa vibaya mno kwa kuangalia matumbo na leo. Hawakuzingatia kesho kitatokea nini.
Umeongea kitu kikubwa sana mkuu, karibu tena jamvini kitambo sana.
 
Kuna kikao fulani kiliwahi kufanyika mwaka 2014, walikuja watu wengi wasomi wa ndani na nje ya nchi. Mzee Mkapa alikuwa mgeni rasmi. Walimshambulia maswali mengi mno, lakini yule Mzee alikataa kabisa kumshambulia CHEKI-BOBU na akasema wazi, hawezi kukanyaga vidole vya mtu. Miaka ya mwanzo CHEKI-BOBU alimfanyia vituko sana Mzee Mkapa lakini yule alitulia tu.

Kuna kipindi alianza kutembelea balozi za nchi mbalimbali baada ya kuambiwa zinamilikiwa na Mzee Mkapa. Alienda Afrika Kusini na maksudi kuomba auziwe jengo la ubalozi maana tunalipa gharama nyingi. Wakamuambia mbona ni la Mtanzania mwenzako Mhindi. Muhindi kuitwa akabanwa akasema jengo siyo lake ni la Mzee. CHEKI-BOBU kwa madaha akapiga simu kwa maksudi kwa Mzee kumuuliza kama jengo ni lake, na Mzee akakataa.

Basi CHEKI-BOBU akalitaifisha kuwa mali ya ummah. Alifanya hivyo kwa baadhi ya nchi. Kipindi hicho na Kiwila ikapamba moto, Mzee akabanwa akarudisha. Lakini ulikuwa huwezi kumkuta yule Mzee anaingilia majukumu ya mwenzake wale kutaka kumhujumu. Walipishana wazi-wazi kwenye gesi ya Mtwara ambapo CHEKI-BOBU akiwepo Mtera Iringa mwaka 2014 alitishia wazi-wazi kwamba wanaosababisha vurugu "Wenye pembe kubwa tutazikata" akimtishia Mzee.

Kiufupi JPM na CHEKI-BOBU walipwaya mno kwenye hili somo la STOICISM. Kuna kipindi tuliwaambia watu kwamba JPM kuna mambo anafanya hatakiwi kushangiliwa. Ndiyo tunapambana na rushwa, lakini kuna nyenzo nyingi na hili taifa bado ni changa sana abadilike. Wafuasi walitufurumushia matusi na kusema sisi ni tarumbeta za mafisadi.

================================================================================
Binafsi huwa naamini kitu kimoja hapa Tanzania: Mzee Mwinyi ndiye Raisi pekee wa Tanzania ambaye amekufa A Natural Death na kifo chake hakina minong'ono. Amekufa kwenye uzee mwema mno, ameshuhudia kijana wake kawa Raisi na amakufa kila mtu akiwa anampenda.

Mzee Nyerere, Mzee Karume, Mzee Mkapa na Mzee Magufuli vifo vyao vimejaa sana minong'oni ambayo inatia ukakasi, hata kama walikufa vifo vya kawaida kweli. Lakini vifo vyao vyote vinatokea wakiwa kwenye fukuto fulani la kisiasa au mabadiliko makubwa ya utawala wa nchi.

Yote tisa, mtawatia moyo watanzania, lakini siasa ni sayansi na ukikosea kanuni ni lazima ikulambe. JPM aliongwa akashupaza shingo. SSH anaonywa anashupaza shingo. Cheki-Bobu anaonywa akae mbali aridhike anashupaza shingo. Well Nature Has a Bad Way of Fixing Things.

Suala la muda tu
​
Nahisi ni kigoda cha mwalimu pale nkurumah hall udsm
 
Basi maamuzi ya mkapa hayakuwa sahihi kwetu kama taifa hasa kwa kutuletea mtu kama magufuri.
Maana kila kinacho endelea sasa muasisi wake ni magufuri wenda angemuacha Rowasa akawa rais kusinge asisiwa siasa za ubabe na kutekana.
Alafu mkapa hana usafi wowote kiasi cha kuwa mfano kwa wengine maana hata yeye amejaa damu za watz kwenye mikono yake.
Hujui lolote
 
Huenda alihofia CCM kufa!
 
Mwaka 235 A.D kule Roma aliuwawa Kaisari aitwaye Severus Alexander. Aliuwawa kwa hila za majasusi wake waitwao The Praetorian Guard ambao walikuwa ndiyo kikosi cha ulinzi na ujasusi cha watawala wa Roma. Mtu ulikuwa huwezi kutawala Roma bila kutumia hichi kikosi.

Makaisari wa Roma walikuwa wanaheshimika kama miungu (Demi-gods), na hata kuwagusa ilikuwa ni sawa na kupingana na amri ya miungu. Utulivu na mafanikio ya dola la Roma, ulitegemea sana uimara wa kiti cha Kaisari. Makaisari wengi wa Roma kabla ya mwaka 235 A.D walikuwa ni lazima watokwe kwenye familia kubwa Roma (Roman Aristocracy) ambapo walifundishwa mambo ya utawala na siasa tangu wadogo.

Severus Alexander alivyoingia kwenye kiti alianza kufanya mabadiliko makubwa sana ya kiuchumi, kisheria na kisiasa ambayo yaliifanikisha mno Roma ndani ya muda mfupi. Japo alikuwa na udhaifu mwingine mkubwa kwamba, alikuwa ni mtoto wa mama (Mama's Boy) ambaye hakuwa na uzoefu wowote wa vita. Hivyo alisoma mambo ya vita bila kwenda uwanja wa vita kama ilivyokuwa lazima kwa vijana wote wa Roma.

Hili tatizo ndilo lilimletea changamoto kwasababu alishindwa kusimamia nidhamu ya jeshi lake. Wanajeshi walikuwa wanafanya vitu vya hovyo lakini yeye kwakutokuwa na uelewa akawa anafanya nao mijadala tu. Watawala kabla yake walikuwa wanafahamu siasa za jeshi na waliweza kulidhibiti. Severus Alexander akiwa kijana mdogo alizidiwa na jeshi, kisha yeye na mama yake wakauwawa.

Baada ya kuuwawa, jeshi likamuweka madarakani askari mwenzao Maximius Thrax kama Kaisari mpya. Huyu hakuwa ametokea familia za watawala, na alikuwa hana elimu ambayo ingemsaidia kutawala. Katika utawala wake Roma ikaanza kuporomoka na ambapo kwa miaka 50 nchi haikuwa na mfalme anayeweza kumaliza muda bila kuuwawa na wanajeshi au majasusi. Hiki kipindi wanahistoria wanakiita The Third Century Crisis.

==================================================================
Kila nchi huwa na utaratibu wake wa kiutawala. Huo utaratibu ukivunjwa lazima madhara makubwa yawepo. Kwenye The Third Century Crisis walikuwepo watu zaidi ya 50 waliouwawa kwa kutaka kukalia kiti cha Kaisari ndani ya kipindi cha miaka 50. Kiufupi Roma ilikuwa imejaa vurugu kama utekaji, mauaji ya kutisha, vita, rushwa na dola kugawanyika.

IKO HIVI: Tokea mwaka 1961-2021, Tanzania imekuwa ikishikiliwa na kiti cha Uraisi. Raisi ni Baba, Raisi ni Mfalme, Raisi ni mungu-mtu, Raisi ni Jalala la lawama, Raisi ni alama ya umoja wa kitaifa na Raisi ni nguzo ya matumaini. Hii ndiyo Tanzania aliyoijenga Mzee Nyerere. Raisi anaweza akawa na madhaifu lakini tunamsitiri na kumstahi tukiwa na matumaini kwamba atamaliza muda wake halafu atakuja mwingine kurekebisha.

Ukweli mchungu ni kwamba miaka ya 1960's-1980's bara la Afrika liligubikwa na mapinduzi na muaji ya Maraisi. Mzee Nyerere alipona mara nyingi. Siyo kwamba alikuwa na nguvu, lakini watu wa ndani ya vyombo vya dola walikuwa wanamchukulia kama BABA YAO MZAZI. Wengi walijiuliza kwamba Mzee Nyerere akitoka nini kitafuata ???

Hata alipokuja Mzee Mwinyi ambaye Mzee Nyerere na kina Imran Kombe walimfanyia vimbwanga vingi kwasababu walikuwa hawamkubali, ukweli mchungu ulikuwa ni kwamba lazima amalize muda wake. Hili lilikuwa siyo suala la majadiliano bali mustakabali wa nchi.

Tatizo likaja mwaka 2005 alipoingia kaingia Cheki-Bobu Ikulu. Alivurunda mno nchi ikafika hadi kipindi wakafanya jaribio la kumleta Dikteta kurekebisha. Cheki-Bobu na udhaifu wake wote alivumiliwa na muda wake ukaisha. Mwaka 2015, aliingia Dikteta kwelikweli. Alifanya makubwa ndani ya muda mfupi huku akiacha vilio na maumivu mengi pia.

Bahati mbaya sana, wengi hawakumpenda na hawakumvumilia ambapo ilitakiwa mwaka 2025 awe anaondoka madarakani. Mbaya zaidi Tanzania kuna utamaduni wa pande mbili kupokezana miaka 10/10. Hivyo ni lazima Raisi amalize muda wake, mpende au msipende. Utamaduni huu ndiyo umeleta utulivu na amani kwa kipindi kirefu nchini.

Anaweza akaingia mvaa kobasi akasemwa sana, lakini hawezi kutolewa kwasababu lazima Raisi amalize muda wake. Kama hamumpendi msingepitisha jina lake kule NEC. Hivyo hata Wagalatia watasema na kutoa matamko, lakini hawafanyi jambo la kijinga kwasababu wanafahamu zamu yao itakuja.

Huu utaratibu unaweza kuonekana ni una ufedhuli mwingi lakini ndiyo ambao unafanya kazi kwa taifa changa kama letu (The Only Practical Method to Ensure Political Stability). Ni lazima mzani uwiane (Balance of Power), usipowiana ni lazima mtapata matatizo.

SHIDA INAANZA HAPA: Watu walio karibu na Raisi masaa 24/7/365 ni Majasusi na Wanajeshi. Hawa ndiyo humsaidia Raisi kutawala. Hapa Tanzania hili kundi tokea mwaka 1964 hadi 2021 lilijengwa kwa dhana kwamba Raisi hagusiki, hata iweje. Raisi ni mungu-mtu. Raisi ni Nchi. Raisi ni Baba. Hivyo kama kumdhuru subirini amalize muda wake ndiyo mtamgusa lakini mkimgusa akiwa madarakani mtayumbisha nchi nzima. Hili hata wale wenye falsafa tofauti ndani ya mfumo walikuwa wanakubaliana.

Baada ya mwaka 2021 utaratibu ulibadilika vibaya mno. MKUU WA NCHI aliguswa, kukawa na minong'ono, huku mahasimu wake wakajisifu hadharani kwamba "Sasa Bahari Iko Shwari" na kutamba kwa kejeli nyingi. Hakuna aliyewakeme. Miaka michache baadaye tunasikia minong'ono kwamba MKUU WA NCHI kweli alihujumiwa.

Ndiyo alikuwa Dikteta, Ndiyo alikosea mambo mengi tu. Lakini kwanini mlimpitisha mkifahamu tabia zake fika. Kwanini hamkusubiri amalize muda wake kama ambavyo mlimvumilia CHEKI-BOBU aliyekuwa anafanya mambo ya ajabu Ikulu yenye madhara makubwa kwa nchi ???

=================================================================
Tokea mwaka 2021 yametokea muaji makubwa ya kutisha kuwahi kutokea hapa Tanzania. Hayatakuwa mwisho kwasababu mzani wa madaraka haujakaa sawa. Mbaya zaidi imefahamika kwamba MKUU WA NCHI naye anagusika vizuri na haliwezi kutokea jambo lolote lile kubwa. Historia inaonesha kwamba mara nyingi mapinduzi makubwa, huzaa mapinduzi mengine. Nchi huchukua muda mrefu mno mpaka ije kutulia:

​
  • Mwaka 1651 waingereza walipindua mfalme wao na kumnyonga ila nchi ilikuja kutulia mwaka 1688 baada ya kuanzisha utaribu mpya wa kiutawala.​
  • Mwaka 1789 wafaransa walipindu mfalme wao na miaka zaidi ya 30 nchi ilijaa damu na vita, ikaja kutulia mwaka 1814.​
  • Mwaka 1776 makoloni 13 ya Marekani yaliasi dhidi ya Mfalme, na nchi ilikuja kutulia mwaka 1815 baada ya kumaliza ugomvi na Muingereza.​

Hata hapa Afrika mchezo ni uleule tu:

RWANDA: walimfukuza Mfalme Kigeri ila mpaka leo kila utawala mpya umeingia kwa kumwaga damu. General Kayibanda, General Habyarimana na General Kagame, wote wameingia kwa bunduki. Ila makosa yalianza kule kwa Mfalme Kigeri.

UGANDA: walianza na kumtoa Mutesa. Akaja Obote akatolewa. Akaja Amini akatolewa. Akarudi Obote akatolewa. Sasa yuko Museveni naye akiondoka haijulikani Uganda itakuwa kwenye hali gani. Hakuna anayeweza kuvaa viatu vya Museveni.

ZIMBABWE: nako ni hivyo-hivyo tu. Mubage alitolewa akaingia Munangagwa.

NIGERIA: walau kipindi hiki wametulia na wanapokezana kimakabila na kidino

Tanzania na Kenya, MUNGU alitupendelea mno. Jinsi tulivyokuwa tunayaangalia madaraka (Approach Towards Leadership) mbali na madhaifu yetu mengi imakuwa ni kuvumiliana mno (Tolerance). Siyo kwamba sisi tuna kitu cha ziada kuliko wenzetu lakini tuna kiwango kikubwa cha kuvumiliana.

GHANA, South-Africa na Botswana ni mataifa ambayo yameanza kukomaa hapa Afrika linapokuja suala zima la kuvumiliana kisiasa. Sisi hapa Tanzania tunarudi miaka ya 60's kuishi maisha ambayo hatukuyaishi. Maisha ya machafuko (Political Instability). Kitakachotokea Tanzania kipindi hiki ni kwamba kiti cha Uraisi kitatingishwa mno kwa miaka mingi, hata huyu wa sasa akitoka.

Tumeshatengeneza BAD PRECEDENT, na kutulia mpaka pande zote ziumie na kupata hasara kubwa ndiyo tutarudi kuwa kawaida. Ila kwasababu NOBODY IS SAFE. Kiufupi hata uweke wanajeshi barabarani, muda wako utafika tu. Mlichokianzisha mwaka 2021 lazima mkinywee, tena mtakinywea vibaya sana.

Siasa ndivyo ilivyo, historia imejaa ushahidi wa hichi nachokisema kuanzia Rome, The Rashidun Caliphate, Mongol Empire, Tang Dynasty n.k Kumuua mfalme (Mzuri au Mbaya) na machafuko yasitokee huwa ni nadra mno.

====================================================​
Heko nyingi kwako brother!! Ama hakika ubongo wangu umepata chakula murua kabisa siku ya Leo. Uliyoyasema ni kweli tupu, Kuna mahali tulijikwaa sana kama taifa.!
 
Kaka RRONDO nimefurahi sana kukuona mzima. Juzi hapa nilitaka hadi kuanzisha uzi kuuliza kama uko salama. Kukuona hapa mzima napata faraja.

Kiufupi ni kwamba MUDA NI MSEMA KWELI hasahasa kwa kinachoendelea kipindi hiki. CCM wanaweza kudhani tatizo lao ni Samia na akitoka nchi itatulia kumbe wapi. Matatizo ni makubwa mno na yana mzizi mrefu. Siasa za 2015-2021, zilichangwa vibaya mno kwa kuangalia matumbo na leo. Hawakuzingatia kesho kitatokea nini.

I hope I'm wrong, lakini Tanzania yetu is headed for a very bigger crisis. Mbaya zaidi ni kwamba baadaya Mzee Mkapa kufariki nchi imekuwa haina BABA MLEZI ambaye anaweza kusema au kukemea kitu na watu wote wakaacha na kuogopa.
​
Mi nadhani baada ya kuondoka mzee Mkapa, ili apatikane mwingine wa kuweza kukemea na nchi ikaelewa kuna mmoja humu katikati ameonekana kupoteza sifa za "ubaba" na hivyo nguvu ya kukemea hana tena

Katika hali kama hii linakuja swala ambalo sio zuri sana kulisema lakini inabidi liwe hivyo; aondoke kwa utata kama walivyoondoka wengine ama akalishwe chini na wazee wenye busara (naamini wapo) aambiwe "amepoteza sifa za kukemea lolote" hivyo atambulishwe mtu atakayeweza kukemea na akasikilizwa
 
Nahisi ni kigoda cha mwalimu pale nkurumah hall udsm
Hapana ilikuwa TANPROF iliandaliwa na Marehemu Jaji Mwaikasu na kina Andrew Massawe. Baadhi ya wazungumzaji waliokuwepo ni kina Peter Noni, Father Kitima, Juma Mwapachu. Ilikuwa nzuri sana kwasababu walijaa wasomi wenye uzoefu mkubwa. Kule Kigoda huwa kumejaa Academics ambao wanataka kurudisha nchi kwenye AZIMIO LA ARUSHA.​
 
Sisi walalahoi haya hayatuhusu, hatuna mali za kuharibikaz hatuna utajiri, tumezaa hovyo hovyo na watoto hawana Future, kimsingi sisi hatuna cha kupoteza.

Acha wapimane nguvu.

Back
Top Bottom