nimekupata vizuri mkuu, hasa kwenye hitimisho pametulia zaidi.
ninaking james yangu hapa yenyewe hata chakula inaita nyama (meat).
sina reference za kigiriki na kiebrania, zaidi huwa natafuta kwenye websites zinazotoa ufafanuzi wa neno kwa neno.
Taadhali ni muhimu katika kujadili huku ukiwa na backup ya ukweli. Binafsi naamini Bibilia ina ULTIMATE AUTHORITY kwenye maisha yangu ya Imani, chochote nje ni assumption kama zinaumana na bibilia naziamini kama zinapingana bibilia inabaki kama mamlaka kuu.
Natambua kuna maandishi mengi nje ya bibilia ambayo yanapewa hadhi sawa na bibilia lkn contents zinakinzana na bibilia. nimejiwekea wigo wa bibilia pekee.
Kuhusu suala la Tuiache bibilia ijitafsiri kusema wale ni malaika au sio malaika inaweza ikawa na impact ndogo katika imani. Lkn nadhalia ya wale kuwa malaika mkuu inafungulia mafuriko ya mafundisho tata kuaminika.
1: Itakutaka uamini kitabu cha Enoch &co ambacho kina contradictions kibao.
2:Bibilia inasema mwanadamu nimekuumba punde kidogo ya malaika, akiwepo nephili ambaye ni hybrid wa malaika maana yake atakuwa na intermediate ability, hivyo kama ambavyo majini na mapepo hayakufa katika mafuriko kuna uwezekano akawepo huyo mdau OGU kukwepa hiyo adhabu ya Mungu. Hii inahafifisha uwezo wa Mungu kuwa wanadamu hao wanaweza kukwepa adhabu ya Mungu kiujanjaujanja.
3:Itabidi tukubaliane na hadithi zilizopo uswahilini kuwa flani alizaa na jini.
4:Itabidi tutlie mashaka authoritative statement ya yesu kuwa Malaika hawazai, wala hawana hizo habari.
5:Itatutaka tujiulize hilo zoezi la mapenzi ya malaika na wanadamu lilikwamia wapi, maana baada ya gharika majin na malaika walikuwepo, na hao wanadamu wapo hivyo hadi kesho tunaweza kudate malaika na majini. Tutaipa mzigo bibilia kutoa majibu ambayo tayari yapo kwenye vitabu vinavyopingana na bibilia.
mtazamo kiongozi.