Mfalme Suleiman (Solomon) alikuwa na wake 700 na michepuko 300 kweli? Kwanini?

Ukiambiwa vijana wa kileo hawana uwezo wa kummudu hata mmoja
 
Iko hivi, nyumbani kwa mfalme suleimani ilikuwa kama kijiji, ina maana alikuwa akitoka kwenda kutembelea maeneo mengine ndani ya ufalme wa wana wa israel alikuwa akimpenda mwanamke anampeleka kwenye makao yake ambayo yapo kama kijiji, ina maana jamaa alioa wake mpaka ikawa kijiji, na huenda ndani ya watumishi wake wa kiume walikuwa wanawashughulikia wake wake hao ila mtoto akizaliwa anahesabu kuwa ni wake. Yaani jamaa alikuwa na makao makuu ya himaya yake hiyo,asubuhi kila mwanamke anakuja kumsalimia,na huenda jamaa kuna wake zake aliwaoa na hakuwa anawafahamu. Naomba nisihojiwe maana nimetumia common sense tu si muumini wa dini yeyote bhandugu.
 
Kuna jamaa hapa kijijini kwetu anawake 12 na hajafika hata 45 yo
Kama kwa karne hii mtu anamudu wake 12 vipi enzi za mfalme Suleman
 
Aisee hesabu zinagoma, yaani wanawake 1000 kuwawekea utambi kila siku mmoja means mzunguko ni miaka takribani 3 au ukiamua kula wawili kwa siku ni siku 500. Hii naona imekaa kitapeli. Vitabu vya dini vinatupanga sana.

Eti Mtume aliugawanya mwezi vipande viwiliπŸ˜€ hizi dini zinatuonaje kwa mfano?

Tustuke wakurungwa.
 
I was listening to the Book of Esther the other day,

Mind you kati ya wanawake woote walichaguliwa ku contest kuwa Malkia, wakanakshiwa mwaka mzima na mafuta na nini, Esther ndo akawa the best akawa Malkia.

Baadaye wakati Mordekai anamuomba Esther awasaidie Wayahudi wasiuawe, nikashtuka kusikia Esther akisema mimi sijaitwa kwa mfalme siku 30 na siwezi kwenda bila kuitwa! ! !

I was like whaaat! ! Siku 30! ! !

So about Solomon, it doesn't mean alikuwa hata analala nao. Analala naye mara ya kwanza ndo imetoka, bidada anabaki tu kwenye kasri kula bata! ! !

Kwenye masherehe anawatoa kuringishia tu wageni! ! !
 
Hujapigwa kabisa (hujadanganywa); stori hiyo ipo kwenye maandiko ya kidini, lakini maana yake kihistoria ni tofauti na unavyofikiria. Kwenye Biblia ya Kikristo (kitabu cha 1 Wafalme 11:3), imeandikwa wazi kuwa Mfalme Suleimani alikuwa na wake 700 wa uzao wa kifalme na masuria (michepuko ya kihalali) 300.Hata hivyo, wanahistoria na wasomi wa mambo ya kale wanaeleza kuwa idadi hii kubwa haikuwa na uhusiano wowote na masuala ya mapenzi au ngono kama tunavyotafsiri leo.
 
Hali ya Maisha ya Wanawake Hao: Wanawake hawa hawakuwa wanaishi chumba kimoja au kukutana na mfalme kila siku. Wengi walikuwa wanaishi kwenye majumba yao maalum ndani ya ikulu, wakilindwa, wakilishwa, na kupewa heshima zote za kifalme, lakini wengine hawakuwahi hata kuwa karibu na mfalme kimapenzi
 
Kuna Mzungu yeye anasema pale nyoka anapoongea na Eva ni stori mtoto wake atamfundisha nyoka haongei na eti mwanamke alitoka ubavuni mwa mwanaume ni stori pia atamfundisha mtoto wake hakuna kitu kama hicho.
 
Ni fiction stories za Wayahudi
 
Upo sahihi kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…