Huihui2
JF-Expert Member
- Jan 5, 2012
- 7,021
- 11,475
Kuna mtego alikuwa anakuwekea. Una bahati sana na nakushauri ukimuona siku nyingine usijirahisi hivyo.Ila huyu bwana ana mazuri yake pia.
Binafsi sikuwahi kumjua Hadi pale nilipokutana Hospital usiku saa sita nikiwa na mtoto wangu ambae alizidiwa GHAFLA nyumbani na kumpeleka hapo hospital nikitegemea Bima mfukoni shi. Mia mbovu Sina🤣
Basi mtoto alipimwa akawa amelala kwa benchi.
Ndipo yeye alipotokea na kumkuta mtoto kalala akasema mtoto msiponji,
Kishaa akaagiza nesi ampe panado.
Mimi nikajua ndo Mganga Mkuu wa hapo.
Akaagiza apimwe na Homa ya dengue,Kipimo kulipia 50,000/ sisi tukasema hatuna pesa hiyo.
Yeye akamwagiza nesi ampime mtoto,atalipia yeye!!!
Majibu yakatoka hakuna kitu ila mtoto kachemka mbaya sana!!
Akatuambia tuchukue Bima atupeleke hospital nyingine! Mimi nikajisemea huyu ni MMILIKI wa hii hospital hivyo anatupeleka hospital yake nyingine kubwa🤣
Wale wahudumu wote walokuwa kaunta aliwapa 15,000 Kila mmoja na WALIKUWA kama 4 hivi.
Wakati nachukua bima yangu alikuja nesi mmoja AKANIAMBIA unahama hospital huyo mnamjua ??
Nikasema Mimi simjui na Mimi najua nyie ndo mmetujamisha.!!
Nikasema asije kuwa mtekaji,Nikaandaa meseji ya maelekezo kwenda kwa Kamanda wa polis nikaitegesha kabisa ili nikiguswa tu naisend🤣🤣
Nilipotoka nje nilikuta Gari jeusi V8 MPYAAA😀Kwa woga woga na kwa tahadhari ya hali ya juu nilipanda😀
Aliendesha Dakika 10 nyingi tulifika hospital hiyo ,Hapo bima hawatumii ni kulipa kwa kesho ,
Akaagiza tuhudumiwe Kila kitu gharama atakuja kulipa yeye!!!
Kweli mtoto alianza vipimo upya na kifupi gharama ilikuja 136,000/
Tylipomaliza matibabu tukampigia sekunde nyingi alikuja akalipa gharama zoote👏
Nilimuomba namba yake alinipa , Nilimuuliza upo wapi hakusema .
Siku Moja tulienda tena kwenye hiyo hospital wife anajuana na nesi mmoja alimuuliza yule mtu wa siku ile alikuwa nani,?
Akamwambia huyo ni Alex Msama huwa anapenda sana kusaidia wakinamama na hasa Watoto😀
Milima haikutani ,Binadamu hukutana !! Tulikutana nae tena baada ya miezi mingi hapo hapo na majira hayo,Tulimkumbuka tukamsogelea tukamkumbushia akaja akamuona mtoto akatuachia tena 50,000/=
Ndo mwisho wa kuonana nae tena Hadi Leo YAPATA miaka sita nyuma!!
Iko siku atakubebesha madawa ya kulevya kama alivyomtumia Rose Muhando