Mfanyabiashara Alex Msama akamatwa kwa tuhuma za Utapeli wa Viwanja vya Tsh. Milioni 800

Mfanyabiashara Alex Msama akamatwa kwa tuhuma za Utapeli wa Viwanja vya Tsh. Milioni 800

mkuu Kashishi yetu mtu kusaidia watu si kigezo cha huyo mtu kuwa mwema, unaweza kuona mwema kwa vile alikusaidia ila kuna anaowaumiza vibaya mno, kuna mwamba moro alikuwa anasaidia watu sana na mtoaji mzuri kanisan, ila nyuma ya pazia ni mafia hatar, wahindi wa moro walikuwa wanapata tabu sana kwa kutekwa magari yao ya sukar kutoka mtibwa, alikuwa na kikundi chake cha utekaji, alikuja kuuwawa getin kwake baada ya kujichanganya na kuteka gari ya mke wa waziri mkuu mstaafu kuchua kiasi kibubwa cha hela alichokuwa nacho na kumbaka, huo ndo ulikuwa mwisho wake, alikuwa amemweka kamanda wa moro mfukoni, hakuna tukio lililoripotiwa polisi kuhusu yeye akakamatwa.
 
"Umekuja na gari inayofanana na hadhi yake? Pickup?"
Kumbe matabaka hayawezi kwisha
 
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam kwa tuhuma za kutapeli viwanja vinne vya Beatrice Mshumbuzi, vinavyokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi milioni 800.

Msama amekabidhiwa kwa polisi leo na Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa.

PIA SOMA
- Jerry Silaa: Alex Msama ni tapeli namba 3 wa Viwanja, ajisalimishe

---

Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Promotion, Alex Msama, anashikiliwa na Polisi jijini hapa.

Kwa mujibu wa video iliyowekwa kwenye mtandao wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC Digital), Msama amekamatwa akiwa ofisini kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa.

Video hiyo inamwonyesha Silaa akiwa ameketi akitoa maelekezo kwa askari Polisi mwenye sare kumkamata Msama.

Silaa amesikika katika video hiyo akiuliza iwapo askari huyo ana pingu akajibiwa zipo chini.

Msama aliyekuwa amevaa fulana yenye mistari na koti lenye rangi ya kaki, ameonekana akiingia na askari kwenye gari dogo lenye rangi nyeusi lililokuwa limeegeshwa nje ya geti la jengo la Wizara ya Ardhi, lililopo Kivukoni jiji hapa.

Mbali na video hiyo, taarifa kutoka kwa watu walio karibu na Msama zimesema amekamatwa leo saa 10.00 jioni.

Mwananchi Digital imemtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro kwa simu, ambayo ilipokewa na msaidizi wake aliyeeleza yuko kikaoni.

Juhudi za kupata taarifa kutoka Jeshi la Polisi zinaendelea.

Ingawa haijawekwa wazi sababu ya kukamatwa kwa Msama, hivi karibuni Waziri Silaa alikaririwa na vyombo vya habari akimuhusisha na utapeli wa ardhi.

Mwananchi
Mbona Kama hili igizo liko scripted....
 
Ila huyu bwana ana mazuri yake pia.

Binafsi sikuwahi kumjua Hadi pale nilipokutana Hospital usiku saa sita nikiwa na mtoto wangu ambae alizidiwa GHAFLA nyumbani na kumpeleka hapo hospital nikitegemea Bima mfukoni shi. Mia mbovu Sina🤣

Basi mtoto alipimwa akawa amelala kwa benchi.

Ndipo yeye alipotokea na kumkuta mtoto kalala akasema mtoto msiponji,

Kishaa akaagiza nesi ampe panado.

Mimi nikajua ndo Mganga Mkuu wa hapo.

Akaagiza apimwe na Homa ya dengue,Kipimo kulipia 50,000/ sisi tukasema hatuna pesa hiyo.

Yeye akamwagiza nesi ampime mtoto,atalipia yeye!!!

Majibu yakatoka hakuna kitu ila mtoto kachemka mbaya sana!!

Akatuambia tuchukue Bima atupeleke hospital nyingine! Mimi nikajisemea huyu ni MMILIKI wa hii hospital hivyo anatupeleka hospital yake nyingine kubwa🤣

Wale wahudumu wote walokuwa kaunta aliwapa 15,000 Kila mmoja na WALIKUWA kama 4 hivi.

Wakati nachukua bima yangu alikuja nesi mmoja AKANIAMBIA unahama hospital huyo mnamjua ??

Nikasema Mimi simjui na Mimi najua nyie ndo mmetujamisha.!!

Nikasema asije kuwa mtekaji,Nikaandaa meseji ya maelekezo kwenda kwa Kamanda wa polis nikaitegesha kabisa ili nikiguswa tu naisend🤣🤣

Nilipotoka nje nilikuta Gari jeusi V8 MPYAAA😀Kwa woga woga na kwa tahadhari ya hali ya juu nilipanda😀

Aliendesha Dakika 10 nyingi tulifika hospital hiyo ,Hapo bima hawatumii ni kulipa kwa kesho ,

Akaagiza tuhudumiwe Kila kitu gharama atakuja kulipa yeye!!!

Kweli mtoto alianza vipimo upya na kifupi gharama ilikuja 136,000/

Tylipomaliza matibabu tukampigia sekunde nyingi alikuja akalipa gharama zoote👏

Nilimuomba namba yake alinipa , Nilimuuliza upo wapi hakusema .

Siku Moja tulienda tena kwenye hiyo hospital wife anajuana na nesi mmoja alimuuliza yule mtu wa siku ile alikuwa nani,?

Akamwambia huyo ni Alex Msama huwa anapenda sana kusaidia wakinamama na hasa Watoto😀

Milima haikutani ,Binadamu hukutana !! Tulikutana nae tena baada ya miezi mingi hapo hapo na majira hayo,Tulimkumbuka tukamsogelea tukamkumbushia akaja akamuona mtoto akatuachia tena 50,000/=

Ndo mwisho wa kuonana nae tena Hadi Leo YAPATA miaka sita nyuma!!
Yaani anatapeli milioni 800 harafu anazuga na kimsada Cha laki
 
Nilishasemaga humu huyu jamaa
Ni mzushi sana...
Kwa wanaomjuwa huyu jamaa
Wala hawahangaiki,dili zake issue zake nyingi ni longolongo
Ukifanya naye jambo kulipa napo
Mtihani!
Pale alipopangaga mgahawa wa food point opposite na bestbite
Napo alitaka kumletea usanii mwenye eneo pale,mama yangu mama naniii---kwenye mkataba
Msama sjui alimchukulia poa yule mama,yule mama alipomuhusisha mme wake mtu ambaye tena yuko kwenye mfumo,alimtoa baru msama pale kama mwizi
Huyu msama anajifanya pekee yake anaijuwa hela
Alafu sasa kwa kujifanya mchamungu 😄

Ova
Duu ile restaurant pale kipindi inazinduliwa niliioona mpaka nikasema jamaa ana akili ya kuona mbali guess what nikatoka kitaa kile baada ya siku nyingi kidogo nikarudi town napita pale imekufa kifo cha mende nikajua tu huyu jamaa tapeli kuna tukio alipiga kwa ninavyomfahamu!
😁😁
 
Njia ya kujificha ile,ndomana makonda alupokuwa rc dar alimnyima vibali kufanya matamasha yake ya upigaji
Anamjuwa

Ova
Makonda alimuassist sana jamaa kutubana watu tunaokodisha movies.

Hadi Siro akatumika kwenye hilo sakata. Kama alinyimwa vibali na Makonda labda kwa mambo mengine lakini hao wanajuana
 
Ana mgahawa pale jengo la life house,kwa chini na kama kapanga pale sijui kama kodi analipa,huyu akipanga sehemu lazima afanye uzushi

Ova
Mfano mkataba unasema kodi italipwa kwa mwaka na akasaini.

Yeye anao na mwenye jengo anao.

Kikifika kipindi cha kodi anazusha nini ili asilipe kodi na hapohapo aendelee kupanga?
 
Yaani anatapeli milioni 800 harafu anazuga na kimsada Cha
Mimi kwa kipindi hicho na sikuwa na pesa siwezi kumsema vibaya kikubwa ni kumulmbea Mungu amfanyie wepesi.

Na Sina hakika kama katapeli kweli au laa maana MFUMO wa mahakama wenye kutoa haki haujamtangaza rasmi kuwa tapeli.

Ukifuata wanasiasa wengi hupenda kujitengenezea umaarufu bila kuja upande mwingine na ndiyo maana maamuzi Yao wakipelekwa mahakamani yanatenguliwa!!
 
Tayari anatuhuma zaidi ya Moja za utapeli Tena katuhumiwa na mhimili mzito sana ambao ni serikali kwaiyo matatizo yako ya kushindwa kutimiza majukumu yako mama wa mtoto yasikufanye kuja kumpampa huyo bwana humu
 
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Dar es Salaam kwa tuhuma za kutapeli viwanja vinne vya Beatrice Mshumbuzi, vinavyokadiriwa kuwa na thamani ya shilingi milioni 800.

Msama amekabidhiwa kwa polisi leo na Waziri wa Ardhi, Jerry Silaa.

PIA SOMA
- Jerry Silaa: Alex Msama ni tapeli namba 3 wa Viwanja, ajisalimishe

---

Mkurugenzi wa Kampuni ya Udalali ya Msama Promotion, Alex Msama, anashikiliwa na Polisi jijini hapa.

Kwa mujibu wa video iliyowekwa kwenye mtandao wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC Digital), Msama amekamatwa akiwa ofisini kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Silaa.

Video hiyo inamwonyesha Silaa akiwa ameketi akitoa maelekezo kwa askari Polisi mwenye sare kumkamata Msama.

Silaa amesikika katika video hiyo akiuliza iwapo askari huyo ana pingu akajibiwa zipo chini.

Msama aliyekuwa amevaa fulana yenye mistari na koti lenye rangi ya kaki, ameonekana akiingia na askari kwenye gari dogo lenye rangi nyeusi lililokuwa limeegeshwa nje ya geti la jengo la Wizara ya Ardhi, lililopo Kivukoni jiji hapa.

Mbali na video hiyo, taarifa kutoka kwa watu walio karibu na Msama zimesema amekamatwa leo saa 10.00 jioni.

Mwananchi Digital imemtafuta Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro kwa simu, ambayo ilipokewa na msaidizi wake aliyeeleza yuko kikaoni.

Juhudi za kupata taarifa kutoka Jeshi la Polisi zinaendelea.

Ingawa haijawekwa wazi sababu ya kukamatwa kwa Msama, hivi karibuni Waziri Silaa alikaririwa na vyombo vya habari akimuhusisha na utapeli wa ardhi.

Mwananchi
Mwana mpiga mbaya, ukiuliza majaji mahakama ya Rufaa wanamjua.
ana kesi za ardhi kila uchao.
Inasemekana alikuwa anakula "Lozi Mwando"
 
Back
Top Bottom