Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Sasa huna receipt mzigo ameutoa wapi lazima mkwepa kodi, kama wewe umekwepa kodi utaweza vipi kudai kodi wakati huyo mtu ni muhujumu uchumi.

Lakini kama wewe ni mfanyabiashara umeagiza au umenunua mzigo una receipt zako za manunuzi kuonyesha kama ulilipa VAT.
 
Mafisadi yana nguvu sana awamu hii. Hivyo hakuna waziri atasimama awamu hii ambaye atapingana na mafisadi
 
Tanzania intelligence and security service
 
Sasa huna receipt mzigo ameutoa wapi lazima mkwepa kodi, kama wewe umekwepa kodi utaweza vipi kudai kodi wakati huyo mtu ni muhujumu uchumi.
Ukifanya biashara utaelewa.

Mfano 1. mpo 30, mmeagiza mzigo China ili kujaza contena, mzigo unapita kwa tin moja pale bandarini. Mkishagawana mzigo unatoa wapi risiti yenye tin yako?

Mfano 2. Una hoteli ww unahitaji hoho, biringanya, nyama n.k kwa wakulima wasio na risiti. Utanunua hayo mavitu yote bila risiti utaiclaim wapi?

Mfano 3. Contractors wadogo, umeshawahi kupata tenda vijijini? Sehemu ambayo hakuna hardware kubwa zenye risiti za VAT? Unabakiwa na option mbili, either usafirishe cement/nondo zako au ukubali VAT ikuumize.

VAT ni ya kutazamwa upya. Ni kisababishi cha kutokutoa risiti. Watu wanakwepa kuingia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…