Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Leo wamejua kumuweka wazi… kazi kwake Mama.
Siasa haina rafiki wa kudumu ina maslahi ya kudumu. Pengine ile ni mbinu ya mfumo inayotumiwa na Rais mwenyewe kumuondoa Mwigulu katika cheo chake,kwamba hana msaada na wadau wake ni mashahidi.

Samia anatumia mbinu zile zile za JK za kumfanyia mtu kitu mbaya halafu jioni moja anakula nae chakula cha jioni huku wakitabasamu na kupiga picha nyingi.
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] Usihadaike na Kelele hizo. Serikali lazima ikusanye Kodi iwe isiwe.

Shida yenu mlidanganywa sana na Rais Magufuli.

Magufuli alitumia nguvu kubwa kuboresha kanda ya ziwa, Dar Es Salaam na Dom tu. Mikoa mingi hali ilikuwa mbaya sana, kimiundombinu na kiuchumi.
Sio kweli

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Tz hamna bunge
Nashangaa watu wasio na exposure inakuaje wanatunga sheria za Nchi?


Huu mjadala nimeona wafanya Biashara wapo na akili Sana kuyazidi makundi yote hapa TANZANIA wapo a head of time
Mfanyabiashara hata Kama kafilisika mtaji,bado anabaki na akili zake za kuanzia upya!!!
 
Ni jambo jema sana tena mno!

Nafuatilia mubashara TBC kiukweli angekuwepo Shujaa Magufuli kwa haya maelezo ya Wafanyabiashara Waziri angeliwa kichwa fasta!
Hebu acheni upuuzi na kero zenu!
'shujaa' wenu Magufuli:-

1. Aliongeza utitiri wa kodi, ushuru wa maghala, hata kodi za pango aliingilia.
Kipindi chake nchi iliongozwa na miongozo na 'maagizo toka juu' badala ya Katiba na Sheria za nchi.
Biashara na makampuni mengi vilifungwa, kuhujumiwa na/au kufikisiwa mfano burea de changes, makandarasi, wapinzani wake.

2. Nani aliyehalalisha rushwa kwa polisi, traffic na hata TAKUKURU? Ni Magufuli.
Nani alyeanzisha huo upuuzi wa task forces? Ni Magufuli
Sasa ndio sehemu ya matunda ya utawala mbovu wa shujaa wenu yanasumbua watu.

3. Retrospective tax nani muasisi wake? Ni huyo huyo shujaa wenu - fisadi Magufuli.

4. Rushwa, kubambika kesi za kila namna (uhujumu uchumi, kodi za forodha na plea bargains nk nk), vyote hivyo ni kazi na alama zake Magufuli.

5. Aliyetuletea hilo Bunge 'mfu' ni nani? Ni huyo shujaa wenu Magufuli.
Magufuli alikuwa doa na unajisi mkubwa kwa nchi na taasisi ya uRais.
Hiyo ndio legacy yake.

Leo hii Bunge limethbitisha TENA kwamba limeshindwa kabisa kuisimamia serikali - iwe sakata hili la Kariakoo, ripoti za CAG nk nk

Ni kwa vile tu siasa zimejaa unafiki na upumbavu; maana hata PM huyu huyu alishiriki kutengeneza hayo ambayo leo amekiri kuwa hayafai.

Tunataka Katiba Mpya!
 
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kariakoo, leo Mei 17, 2023.



Wafanyabiashara wa Soko Kuu la Kimataifa la Kariakoo wametoa malalamiko mbele ya Waziri Mkuu ambapo wameilaimu TRA kwa kutokufuata taratibu sahihi za utozaji kodi wakishirikiana na Jeshi la Polisi.

Mfanyabiashara mmoja akitoa malalamiko yake amesema kampuni yake imewahi kusumbuliwa na Askari wa Kituo cha Kamata akidaiwa kutokuwa na risiti halali za mizigo yake, jambo ambalo sio la kweli. Pia, amemtaja kwa jina moja Askari anayehusika na kashfa nyingi za hapo kuwa ni "Mpemba"

"Kuna Askari anaitwa Mpemba hapo Kamata amenipelekesha sana, pia kuna mwingine mweusi yuko hapohapo wanatupelekesha sana. Inashangaza sana Askari wanakusumbua kama vile TRA hadi unajiuliza kazi ya TRA inafanywa na Askari"

Ameendelea, "Kwa kuwa umesema tufunguke, niseme Nchi hii hadi Polisi ni wezi mno, hakuna wakati mgumu kufanya biashara kama wakati huu, tunaiwezesha Nchi lakini wanatukatisha tamaa

Ameongeza, "Tufanye mabadiliko makubwa ili twende mbele, mengine siwezi kusema hapa, nikiyasema watanikamata, nawajua hawa"

Aidha, mfanyabiashara mwingine aliyesimama kwa niaba ya wafanyabiashara wa Vitenge amemhoji Waziri Mkuu kama Serikali haitaki wanawake nchini wapendeze maana wamekuwa wanachukuliwa kama wanauza madawa ya kulevya.

Wamewalamumu pia watu wanaohusika na uzoaji wa taka kuwa wanadai pesa zisizotakiwa, kwani huenda hadi kwenye stoo zao. Pia, watu wa TRA wamekuwa wanawafata hadi majumbani wakitaka pesa. Mama huyo amehoji, "Kwa hiyo tukadange?, hapa sio mahali sahihi kwa kuongea, nitahatarisha maisha yangu. Nipe namba nije chemba tuzungumze"

Kuhusu sababu ya kufunga maduka, mfanyabiashara mmoja amesema walifanya hivyo kutokana na;
  1. Uwepo wa utitiri wa kodi usioendana na uhalisia, "Double Taxation"
  2. Kuhamia kwa maduka barabarani kwa jina maarufu la machinga, watu ambao wamekuwa wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa hivyo kubana biashara zao (wafanyabiashara waliosajiliwa). Duniani kote hakuna machinga kwenye vituo halisi vya kibiashara
  3. Adhabu za makosa ya kutolipa kodi zisizolipika sababu ya ukali wake hivyo kuweka mianya ya rushwa
Kero nyingine iliyotajwa ni maafisa wa TRA kuwa na mamlaka makubwa ya kukadiria faini za malipo pindi wanapowakatama wafanyabiashara kwa makosa mbalimbali, ambayo mengi ni ya kusingiziwa. Jambo hili huleta mianya ya rushwa kwa sababu TRA huwaalika kwa mazungumzo ya pembeni kinyume cha taratibu.

Mfanyabiashara huyo amesema, "TRA wanatufuata mpaka nyumbani jamani, tunaomba namba wakija ili tuwatumie picha, wanatutishia wanazuia Biashara zetu, kwanini watufuate nyumbani? Waziri Mkuu siwezi kukwambia kila kitu, hapa sio sehemu salama nipe namba nikufuate chemba, la sivyo nitahatarisha Maisha yangu

Ameendelea, "Kuna kodi mpya ya Stoo ambayo inaelekeza ukikutwa na kosa unapigwa faini ya Tsh. Milioni 4. Kodi hiyo inatengeneza mazingira ya Rushwa na hatujui kama ipo kihalali au la.

Ameongeza, "Mfanyabiashara hauwezi kukamatwa kwa Mwezi mara tatu, inabidi mzungumze pembeni"

Pia, urasimu kwenye mamlaka za serikali hasa utoaji wa leseni, kupandishwa kila mwaka kwa makadirio ya kodi kwa lugha maarufu ya "Maelekezo kutoka juu", kodi kubwa ya stoo za bidhaa, mfumo mbovu wa kodi ya forodha bandarini pamoja na kamatakamata za aina mbalimbali zinazofanyika sokoni hapo.

Hoja nyingine iliyoibuliwa ni Matamshi ya Waziri Mwigulu Nchemba kudharau wabunge wengine ambao ni wawakilishi wa wananchi, amekuwa na kauli chafu zinazokatisha tamaa wafanyabiashara, mfano ni ile ya kuwa yeye ni daktari wa uchumi, hawezi kubishana na waganga wa kienyeji.

Mfanyabiashara huyo amesema jeuri yote ya TRA inasababishwa na Waziri wa fedha ambae ni bosi wao.

Waziri wa Biashara amelaumiwa pia kwa kutosimama na wafanyabiashara hasa kwa kauli yake ya Bungeni kuwa hakukuwa na mgomo Kariakoo. Wafanyabiashara hao wamesema kuwa haijawahi kutokea hata mara moja Waziri huyo akasimama na wafanyabiashara hivyo hafai kuwa Waziri wao.

Urasimu mkubwa wa mizigo inayotoka Zanzibar umetajwa kuwepo tofauti na wafanyabiashara wanaotoa mizigo nchi zingine kama Dubai n.k. Pia, kumekuwepo na watu wengine wanaotoza kodi baada ya kutoa mzigo bandarini, watu hao wanapaswa kuwepo bandarini ili kurahisisha uliopaji wa kodi na kuokoa muda.

Mfanyabiashara mwingine amesema TRA wamepewa mamlaka ya kuomba rushwa kisheria, kwa kuwa wanalindwa na Sheria mbovu, wanataka rushwa kwa nguvu. "Rushwa ni mfumo, na sheria inawalinda. Wanatumia loophole ya elimu ndogo ya wafanyabiashara kudai rushwa....."

Mfanyabiashara wa vitenge (Mama Bonge) ametoa dukuduku lake la kudaiwa kodi zaidi ya bilioni 30, kisha baadae kutakiwa kulipia bilioni 10.3 ambazo hajalipa hadi leo.

Baada ya kushindwa kulipa alitakiwa kupelekwa mahakamani kwa kesi ya uhujumu uchumi kisha kutakiwa walau moja ya tatu ya gharama zote (3.4 bilioni) wakati hajafanya kazi kwa zaidi ya miezi 8 na kontena zake 10 za vitenge zimekamatwa na TRA Ubungo.

===

UPDATE:
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa Anazungumza

Amesema Serikali ya Samia Suluhu Hassan inayo dhamira ya dhati ya kuwasaidia wafanyabiashara wa Nchii kwa kuwasikiliza na kutatua matatizo yao.

Waziri Majaliwa amesema kikao hiki sio cha mwisho, bali vikao zaidi vitaendelea kufanyika ili kutatua kero na kuinua Sekta hii muhimu kwa uchumi wa Nchi.

Hoja zote zimechukuliwa na Serikali na zinaendelea kufanyiwa kazi kwa mfumo Shirikishi baina ya Serikali na wafanyabiashara wenyewe ikiwemo kuunda tume ya pamoja kati ya Serikali na wafanyabiashara. Timu hiyo itakuwa na watu 14, itapaswa kupitia na kuchukua yote yanayotekelezeka ili yafanyiwe kazi haraka, yanayohusu sheria yatapaswa kushughulikiwa bungeni haraka.

Amewataka Polisi kulinda usalama wa Raia na sio kujihusisha na kazi za TRA na task force hiyo imeondolewa.

Amesema "ipo sheria ya maghala ambayo haina mgogoro, kwanini kelele zibuke kwa TRA? Anayetakiwa kulipa kodi ya stoo ni mmiliki ambaye Wafanyabiashara wanaweka Bidhaa zao, hivyo hadi hapo itakapotangazwa upya, naagiza kamati ipitie upya utaratibu huo

Pia, "Jukumu la Jeshi la Polisi ni kulinda Mali na Watu, kazi ya kukagua risiti sio yao mpaka tu pale watakapokuja kwa dhamana hiyo na waie kwa kuïtambulisha wakiwa na kibali. Kwenda Kariakoo kukusanya kodi italeta malalamiko, hilo hatutaruhusu"

Waziri Mkuu amesema, "Agizo la kuvunia Kikosi Kazi lipo palepale, TRA walileta Vijana ambao hawajasomea kazi ya kodi, wamekuia Viiana ambao wana tamaa zao za Maisha, hapana, haikubaliki. Kodi zitakusanywa na Maafisa wa TRA ambao wamesomea na wana Maadili ili wakikosea tuwabane"

Ameongeza, "Tunajua Wafanyabiashara wana Mikopo, wanahitaji kupanua Biashara. Siku nne zilizopotea ni nyingi mno, nawaomba sana sana tuwarudishe Wafanyabishara walioondoka na kuhama Soko la Kariakoo"

Hoja za wafanyqbiashara ni aibu kubwa kwa CCM na serikali nzima


Serikalini watumishi wezi ndo wanapanda madaraja haraka na wakipewa nafasi zaidi wanawania nafasi za uteuzi.

Hapo wa kuwajibishwa ni CCM maana mwigilu yeye ni waziri tena mwanasiasa nguli wa CCM ..
 
Hebu acheni upuuzi na kero zenu!
shujaa Magufuli si ni yeye:-

1. Aliyeongeza utitiri wa kodi, ushuru wa maghala, hata kodi za pango aliingilia

2. Aliyehalalisha rushwa kwa polisi, traffic na hata TAKUKURU? Nani alyeanzisha huo upuuzi wa task forces?
Haya ndio sehemu ya matunda ya utawala mbovu wa shujaa wenu.

3. Retrospective tax nani muasisi wake? Ni huyo huyo shujaa wenu.

4. Rushwa, kubambika kesi za kila namna (uhujumu uchumi, kodi za forodha na plea bargains - vyote ni kazi na alama zake.
Umeshapanic 😂😂😂😂😂😄😄
 
Tz hamna bunge
Nashangaa watu wasio na exposure inakuaje wanatunga sheria za Nchi?


Huu mjadala nimeona wafanya Biashara wapo na akili Sana kuyazidi makundi yote hapa TANZANIA wapo a head of time
Graduate kibao wapo Kariakoo wanapiga mishe zao,na wengine pia wako huko huko serekalini! Wanapiga migu yote miwili!!!
 
Huyu mchaga anayesoma matatizo ya wafanyabiashara kwenye daftari inaonesha kabisa sio mfanyabiashara wa kariakoo.

Usanii unaendelea katika maisha ya watu...yaani mtu anasoma kwenye daftari utafikiri ni mwanafunzi wa chekechea
Kwa hiyo mtu anayepangilia hoja kwa kuziandika si mtu sahihi bali yule anayetiririka bila mpangilio?
 
Back
Top Bottom