Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Mfanyabiashara: Kiburi cha TRA kinasababishwa na Bosi wao Mwingulu Nchemba

Huyu mchaga anayesoma matatizo ya wafanyabiashara kwenye daftari inaonesha kabisa sio mfanyabiashara wa kariakoo.

Usanii unaendelea katika maisha ya watu...yaani mtu anasoma kwenye daftari utafikiri ni mwanafunzi wa chekechea
Kwa atarifa yako hao ndiyo matajiri wa mjini. wana uthubutu wa kuanzisha biashara na kuwaajiri wasomi. hawaogopi kuthubutu. wasomi ni waoga
 
Wewe kweli huna akili hujasikia hapa Mwigulu anaongeza Kodi ovyoovyo bila kuongea na wafanyabiasha.wakati wa Magufuli kama kungekuwa na matatizo makubwa wafanyabiasha wangegoma Tu Kwa Sababu hakuna mwanasiasa anayeweza kuwazuia wafanyabiasha.alafu shetani ni wewe hapa unayesema uongouongo.yaani miaka 2 baada ya Magufuli kuondoka hawajagoma mpaka Leo Kwa Sababu ya Kodi za ovyoovyo zilizoongezwa na serikali yako ya ovyoovyo.
Ameongeza kodi ipi mkuu?

VAT 18%
SDL 4%
PAYE
WHT 5%, 10% nk

Zote ziko hivyo hivyo miaka kibao.
 
Ndio mbona hili liko wazi sana nani unayemtegemea angethubutu?

Fikiria tu hiki kikao kingefanyika katika utawala wa Magufuli, ungemtegemea kumuona nani ambaye angekuwa ana point uozo wa viongozi kama Mwigulu bila hofu?

Nani angeweza?

Wakati Magufuli anakuja Chunya mkoani Mbeya kwenye ziara yake, kulikuwa kuna wananchi ambao walibeba mabango kuelezea kero ambazo zinaikumba wilaya yao lakinia TISS waliwakamata wale watu na kuwashushia vichapo, na yeye Magufuli alisema "hata mkilia mi siwaoni"

Wale watu walibebwa wakaenda kutupwa kule kona za mkoa wakiwa wamepigika

Achana na hilo

Siku ya meimosi Makonda alitoa kauli ya kuwatisha wafanyakazi kuhusu kunyanyua mabango ya kudai kuongezwa maslahi, sasa kwa uzito wa jambo hili nani angethubutu?
Wangegoma pale alipokufa tu!


Msikifiri kila mtu ana matope kichwani jamani
 
Hakuna mfanyabiashara anayekataa kulipa kodi na ndio maana umeona walivyotoa ushauri wa namna bora ya uchukuaji kodi ambayo ilizidi mara mbili ya ile kodi ya serikali ambayo ilitaka kukusanya.

Sio kila inayoitwa kodi ni halali, zingine ni utapeli ambazo serikali haendi kunufaika nazo zinaishia mifukoni mwa watu tu.

Kama ushawahi ku import product yeyote kupitia bandari halafu ukawa umeifata bidhaa hiyo nchi jirani kama Congo utaona utofauti wake

Bidhaa utayoichukua Congo iliyopitia bandari hii hii ya kwetu ukija kuinunua huku Kariakoo bei yake inakuwa twice au triple.

Hii kama hujawahi kui experience utaona ni ugai gai wakukwepa kodi lakini kama ushawahi hata siku moja kufika bandarini utaona haya madudu
Hizo ni fix, kodi za Afrika mashariki zinafanana tu.
 
Ndio mbona hili liko wazi sana nani unayemtegemea angethubutu?

Fikiria tu hiki kikao kingefanyika katika utawala wa Magufuli, ungemtegemea kumuona nani ambaye angekuwa ana point uozo wa viongozi kama Mwigulu bila hofu?

Nani angeweza?

Wakati Magufuli anakuja Chunya mkoani Mbeya kwenye ziara yake, kulikuwa kuna wananchi ambao walibeba mabango kuelezea kero ambazo zinaikumba wilaya yao lakinia TISS waliwakamata wale watu na kuwashushia vichapo, na yeye Magufuli alisema "hata mkilia mi siwaoni"

Wale watu walibebwa wakaenda kutupwa kule kona za mkoa wakiwa wamepigika

Achana na hilo

Siku ya meimosi Makonda alitoa kauli ya kuwatisha wafanyakazi kuhusu kunyanyua mabango ya kudai kuongezwa maslahi, sasa kwa uzito wa jambo hili nani angethubutu?
Hakuna mwanasiasa anayeweza kuwazuia wafanyabiasha wakigoma Kwa Sababu ya unyeti wao na matatizo mengi ya Kodi na tozo yametokea ndani ya serikali hii.
 
Ameongeza kodi ipi mkuu?

VAT 18%
SDL 4%
PAYE
WHT 5%, 10% nk

Zote ziko hivyo hivyo miaka kibao.
Hujasikia hapa kuna mmoja kasema walioongeza Kodi kutoka laki 8 mpka milioni 2 na akaongeza na kusema kama kuna watu walikuwa Wanashindwa kulipa hiyo 8k wataweza hiyo M2?na wewe unajua ndani ya serikali hii vitu vingi vilipanda bei Sana Sababu mojawapo ni Kwa Sababu ya kupanda Kwa Kodi mbalimbali na tozo.serikali inakuwa ya ajabu isiposikiliza watu wake kama huyo hapo alivyosema kuhusu mwigulu.mwigulu kapandisha Kodi bila kuwasikiliza wadau.
 
Na pia utaratibu wa kutokuwasikiliza watu ambao wapo site yaani unaweka Kodi kwenye secta Fulani bila kuwashikisha wenyewe Kwa hiyo hawatakuwa na furaha kama hivi.

..Ccm haiwasikilizi wananchi au wapigakura kwasababu hawategemei kura, bali hushinda uchaguzi kwa mbinu na mabavu.

..Serikali, wabunge, wakiwa wanapatikana kutokana na kura na uchaguzi wa haki basi utaona viongozi wanawasikiliza na kuwashirikisha wananchi ktk maamuzi mbalimbali.

..Katiba Mpya, Tume Huru ya Uchaguzi, wananchi wanaojielewa na kutambua haki zao, ndio suluhisho.
 
Wangegoma pale alipokufa tu!


Msikifiri kila mtu ana matope kichwani jamani
Wangegomaje wakati bado raisi ni mpya na hivyo kuna hatua za kufanya kabla ya kufikia mgomo?

Unafikiri mgomo unaanza tu kwasababu ya matakwa ya watu?

Mgomo kuufikia ni baada ya kufanya taratibu zote za kidemokrasia ikiwa ni pamoja na kuwaita viongozi kuwaomba watunge sheria mpya ambayo itakuwa fair.

Na hilo wamelisema kuwa waliwafikishia viongozi malalamiko yao ila baada ya kuona hakuna utekelezaji wakaamua wagome

Sasa utawala wa Magufuli nani angethubutu kugoma eti kwakua viongozi wamepuuza maombi yao?
 
Ameongeza kodi ipi mkuu?

VAT 18%
SDL 4%
PAYE
WHT 5%, 10% nk

Zote ziko hivyo hivyo miaka kibao.
kwa uzoefu wangu mdogo kwenye biashara.. Kodi huwa ni zile zile, ila biashara faida na hasara pamoja na mzunguko huwa haupo vile vile.. TRA kuna nafasi ya kukaa nao chini na hata kufanya makubalinao ( na ndio hapa wanafungua mwanya wa kukunyoosha sasa ).
 
Back
Top Bottom