DOKEZO Mfanyabiashara maarufu Arusha aibiwa Tsh. Milioni 100 kwenye akaunti ya Benki ya NMB

DOKEZO Mfanyabiashara maarufu Arusha aibiwa Tsh. Milioni 100 kwenye akaunti ya Benki ya NMB

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mfanyabiashara maarufu katika mikoa ya Arusha, Dar na Dodoma Joseph Kalugendo mkazi wa Moshoni jijini Arusha, ameibiwa fedha zake zaidi ya milioni 100 katika benki ya NMB tawi la Clock Tower Arusha na mtumishi wa benki hiyo.

Taarifa ambazo zimethibitishwa na Mfanyabiashara huyo amedai kuwa siku za usoni alienda katika benki hiyo kwa ajili ya kuchukua fedha ndipo alipopigwa na butwaa kukuta kitita hicho hakipo.

Meneja wa benki hiyo Kanda ya Kaskazini Praygod Mphuru alipohojiwa alikiri kuwepo kwa tukio hilo akidai tayari wamemsimamisha kazi mfanyakazi wao Samweli na kwamba suala hilo linafanyiwa kazi na kuomba suala hilo lisitangazwe.

Pia vigogo wa benki hiyo kwa sasa wanahaha kutafuta mchawi aliyetoa taarifa hizo kwa waandishi wa habari na tayari baadhi ya wafanyakazi wameitwa na kuhojiwa juu ya taarifa hizo za ndani kufika kwa wanahabari

Joseph ambaye hufanya biashara za bar na kusambaza vyakula kwenye kambi za jeshi anadaiwa kulundika kiasi hicho cha fedha kwa muda mrefu bila kutoa kiasi, na kwamba mfanyakazi huyo aliona huenda anayeimiliki alishakufa na kuanza kuchomoa kidogo kidogo na kufikia zaidi ya Tsh. Milioni 100.

Hata hivyo baada ya taarifa hizo kubainika uongozi wa benki ulifanya kikao kizito na kubaini kwamba mfanyakazi wao aliyefahamika kwa jina moja la Samweli ndiye aliyehusika na wizi huo kwa kuchomoa fedha hizo kidogo kidogo hadi kufikia hicho cha fedha.

Uongozi wa benki hiyo tayari umemsimamisha kazi lakini suala hilo bado lipo kimya huku Mfanyabiashara huyo akilalamikia hatima ya fedha zake, maana benki hiyo kuwa kimya na haimpi jibu linaloeweka namna ya kurejeshewa.

Mifumo haiko imara sana, nakumbuka back 2009 jamaa wa benk flani alikua makao makuu, mimi nilikua nazurura maofisini pa watu as sales officer, sasa sijui alipata kamwanya gani alikua anaweka laki4 au5 kila baada ya siku2 au 4, akishaweka ananistua tunakutana ATM kisha naitoa tukiwa wote anachukua laki3 nabaki na 1, aise hadi mshahara unafka nakua na mkwanja amazing, kidogo then nikashtukia hapa iko day ntanyakwa wakati sina hata 10 na jamaa atapotea.

Nikaachana na jamaa, baada ya muda mfupi jamaa akapotea hadi ofisini kumbe kapiga 300M kazihamishia exim bank huko nako akatambaa nazo, akatafutwa kidogo na polisi baadae tukasikia yupo UK.
Mifumo na kuaminiana kumezidi mno kwenye mabenki.
 
Siwezi kukudanganya kama wapo watu wa mtwara humu ndani watakuwa wanamfahamu mzee haule bambo ana fremu zake kama 10 pale sokoni karibu na shule ya chikongola na huyo kinyozi ni saidi mkwango ana saluni yake kule bima na pale kwenye jengo la mother house anayo saluni nyingine na hiyo kluger anayoendesha kapewa bure na huyo mzee bambo,na tukija kwa huyo kichaa aliekakopesha pesa ni rama lupanda maarufu daresalama ndogo na huyo aliekampa ni mbalawazi ambae siku hizi ana kiwanda cha kufyatua matofali hapo magomeni kwenye makutano ya barabara
Chai peleka fb
 
Sasa si ndo kaenda kufuatilia? Wewe unataka kila wiki akacheki balance? 😁😁😁
Screenshot_20230811-165051.jpg
 
Watu wana hela kuna mshkaji mmoja pale mtwara mjini aliwahi kumkopesha mtu milion 18 halafu akasahau kama kuna mtu aliemkopesha pesa ilikuja kugundulika baada ya miaka kama 7 hivi baada ya huyo mtu kuachana na mkewe ndipo mke akaja kufichua kuwa ulimdhulumu baba zai pesa yake alikukopesha ukakaa kimya bila kulipa basi aliposikia huyo mshkaji badala ya kuanza kudai aliishia kucheka tu,na kuna mzee mmoja anaitwa bambo yupo hapo mtwara wakati anatokea dar na klugger lake lenye miezi kama 5 tangu litue nchini kutokea japan alipata ajali pale rufiji ukatoka mlango wa nyuma tu na ilijichuna chuna tu rangi ila mzee alivyo kiburi alisema hii siitaki tena akaagiza nyingine siku ileile na ile iliyopata ajali akampa kinyozi mmoja ambaye huwa anawanyoa watoto wake na yeye mwenyewe na akamsaidia kuifanyia marekebisho na jamaa mpaka leo anavimba nayo mtaani
Najitahidi sana kuwaheshimu wazee ila wao hawataki kuniheshimu mimi

Sent from my SM-J410F using JamiiForums mobile app
 
Yaani hii inadhihirisha jinsi maadili ya utumishi bora yalivyokosekana kwa vijana wa kizazi hiki, binafsi niliwahi kutakua kuibiwa baada ya kutoka benki na hela ktk bashasha ya A4.nilishika mkononi ila nilishtukia mchongo wa bank Clark, nikiwa pale nimeshaomba nitoe pesa, Akasema Hana keshi ya kutosha, akachukua simu akaingia ndani, nikiwa pale Kuna jamaa akaingia ndani akajifanya kama anaulizia money gram nikiwa pale wasinione, yule cashier akamkonyeza, nikashangaa nikasema la bda mtu wake, ila roho ikawahaina Amani, nilipopewa hela yule jamaa a katoka nje bila kupewa huduma... Nikiwa unajiuliza huyu mbona simwelewe... Ni katoka nikawa nyuma yake, Mara a nasimama Mi nazuga na simu.. Ni kafika zebra akajifanya kurudi nyuma avuke na mim, sasa mim siku Simama pale nikacheki gari hakua karibu nikavuka fast a, wakataka kuvuka nae upesi gari likamzui... Uzuri gari ilikua inanisubiria upande wa pili.. Nikaingia jikaondoka a kabaki pale, zebra anashangaa😁😁
Mkuu siyo ulijishtukizia? Kwasababu nyie mkishikaga vimilioni mna wenge sana.
 
Ongezea hapo:

1. Kilimanjaro Cooperative bank iko huko Kilimanjaro( ombeni, Kingazi, makwebe) wapo magereza / wafungwe tu.

2. Akiba bank

3. Azania Bank ( kulikuwa na kijizi kimoja kinaitwa Swai, mtumishi wa Azania).

3. Saccos zote ni wezi wa mchana kweupe na wanashirikiana na mabank)
Mkuu tafadhali ongezea nyama hapo namba 1 Kilimanjaro coop kina ombeni kingazi na makwebe.
 
Mifumo haiko imara sana, nakumbuka back 2009 jamaa wa benk flani alikua makao makuu, mimi nilikua nazurura maofisini pa watu as sales officer, sasa sijui alipata kamwanya gani alikua anaweka laki4 au5 kila baada ya siku2 au 4, akishaweka ananistua tunakutana ATM kisha naitoa tukiwa wote anachukua laki3 nabaki na 1, aise hadi mshahara unafka nakua na mkwanja amazing, kidogo then nikashtukia hapa iko day ntanyakwa wakati sina hata 10 na jamaa atapotea.

Nikaachana na jamaa, baada ya muda mfupi jamaa akapotea hadi ofisini kumbe kapiga 300M kazihamishia exim bank huko nako akatambaa nazo, akatafutwa kidogo na polisi baadae tukasikia yupo UK.
Mifumo na kuaminiana kumezidi mno kwenye mabenki.
Ungenyakwaaa vibayaa wewe yani ungesotaa balaaa[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Benki za kibongo siziamini.

Mimi mwenyewe kuna rafiki yangu mpaka sasa anakimbizana na watu wa benki moja kubwa Bingo iliyopata tuzo hivi karibuni, kuna kama milioni 250 zake hazijulikani zilipo.

Maafisa wa usalama wa benki badala ya kuona aibu na kufanya kazi kuzirudisha, wanafanya uchunguzi mwezi wa 6 huu.

By comparison, more than 10 years ago, mimi nilishawahi kuibiwa $4,000 Citibank. Kuna jamaa walipata details zangu wakachonga kadi, wakatoa hela Dubai.

Citibank walikuwa so embarassed, niliwapigia simu Alhamisi, Jumatatu hela zikawa zimerudi tayari.

Walichofanya ni kuniuliza tu kuhakiki kama nimempa mtu kadi yangu na pin number. Nikasema sijampa. Wakaniuliza kama nimetoka nje ya Marekani wakati huo, nikasema sijatoka. Wakaangalia wenyewe wakaona mchezo umechezwa Dubai. Halafu wakajua kuwa kuna genge fulani linacheza ule mchezo. Wakanirudishia hela zangu mara moja.

Mpaka leo huniambii kitu kuhusu Citibank na Customer Service yao kwenye haya mambo ya kurudisha hela zinazoibiwa.

Bongo unaibiwa wewe halafu benki bado inakuzungusha haiogopi hata bad publicity!
10 years ago hiyo 4000$ ilikuwa hela ndefu sana.
 
10 years ago hiyo 4000$ ilikuwa hela ndefu sana.
Kichekesho nimeibiwa hela zangu Citibank wakati mimi mwenyewe nafanya kazi Global Information Security Administration ya Citigroup on Wall St.

Kwa hesabu za Wall St. hizo zilikuwa hela ndogo tu.

Kuna siku mshkaji alitoa hela kwenye ATM, akawa kama kasahau kuchukua ile risiti ya ATM. Mimi kuidaka nikakuta akaunti yake ina $60,000.

Halafu jamaa mshkaji poa tu ukimuangalia huwezi kumjua kama ana hata $10,000.
 
Nakumbuka kuna dada alikua Barclays ila ana miaka kadhaa sasa amefariki. Alipiga pesa million 500. Na ni binti wa familia bora sana. Na ni vigogo wa serikali humo. Kama sikosei alisoma chuo uingereza.
Ile account haikutumika muda sana. Basi wakafoji, akatengenezwa mtu akaja akasema anataka kujua akaunt yake na pesa ila amesahau password. Basi marehem akachezesha game mlolongo mzima ukapita. Jamaa akaambiwa akaingize finger print upya. Kitu kikajibu. Mil 500 ikasombwa. Dada mwenyewe alikua mtu wa bata sana. Hakuna cha maana hivyo. Kwanza always alikua na madeni. Najua lazima munamjua. Sitaki kutaja jina lake ama waliokua wana associate nae karibu kazini.

Hamad. Mwenye akaunt akaja. Hakuamini kilichotokea ktl akaunt yake. Basi tena bank ikawa responsible na bibie akawa na kesi hata sielewi iliishia wapi lkn alikua mtaani later
Pumzika kwa amani mla bata wetu
 
Duuh nani huyoo mla bataaa...[emoji3][emoji3][emoji3]Aisee unaweza viziwaa uuliwee bipa kujuaa watu wanapoteza ushahidi
 
Chai peleka fb
Hahahaha njaa itakuua sana dogo bahati mzuri nimewataja wahusika wote na humu wapo wengi watu wa mtwara tena wa sokoni na hivyo visa wanavijua vizuri sana...acha makasiriko sasa je nikikuletea kisa cha pedeshee kide baada ya kuipiga zaidi ya milion 150 za ambari kwa ujeuri wake akachukua karai lililo na mafuta ya moto ambayo wanakaangia chipsi akammwagia mtu pale mnarani na akampeleka yeye mwenyewe hospital na akawalipa ndugu zake mgonjwa Cash napo si utabisha?
 
Back
Top Bottom