Benki za kibongo siziamini.
Mimi mwenyewe kuna rafiki yangu mpaka sasa anakimbizana na watu wa benki moja kubwa Bingo iliyopata tuzo hivi karibuni, kuna kama milioni 250 zake hazijulikani zilipo.
Maafisa wa usalama wa benki badala ya kuona aibu na kufanya kazi kuzirudisha, wanafanya uchunguzi mwezi wa 6 huu.
By comparison, more than 10 years ago, mimi nilishawahi kuibiwa $4,000 Citibank. Kuna jamaa walipata details zangu wakachonga kadi, wakatoa hela Dubai.
Citibank walikuwa so embarassed, niliwapigia simu Alhamisi, Jumatatu hela zikawa zimerudi tayari.
Walichofanya ni kuniuliza tu kuhakiki kama nimempa mtu kadi yangu na pin number. Nikasema sijampa. Wakaniuliza kama nimetoka nje ya Marekani wakati huo, nikasema sijatoka. Wakaangalia wenyewe wakaona mchezo umechezwa Dubai. Halafu wakajua kuwa kuna genge fulani linacheza ule mchezo. Wakanirudishia hela zangu mara moja.
Mpaka leo huniambii kitu kuhusu Citibank na Customer Service yao kwenye haya mambo ya kurudisha hela zinazoibiwa.
Bongo unaibiwa wewe halafu benki bado inakuzungusha haiogopi hata bad publicity!