DOKEZO Mfanyabiashara maarufu Arusha aibiwa Tsh. Milioni 100 kwenye akaunti ya Benki ya NMB

DOKEZO Mfanyabiashara maarufu Arusha aibiwa Tsh. Milioni 100 kwenye akaunti ya Benki ya NMB

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Nimpe pole aliyepatwa na mkasa huu,iwe funzo pia kwetu kuwa hata kama hatutoi basi walau kwa mwezi uwe unaangalia kasalio ili kujiridhisha na 'wadukuaji' kama hao.
NMB inabidi wawe wakali kwa wafanyakazi wao vinginevyo hii itawapunguzia kuaminiwa.
 
Hao niwezi walishamwibia bab wawatu bosy wetu ml 250 tena zilikuja kwa dola na ilikuwa ya wateja wanakuja huku tanzania wa mwaka mzima palikuwa hapatoshi walituzungusha sana , benki zenye wizi wakuonekana ni hizi CRDB, NBC , BOA, NMB,STANBIC ,EXIM BANK NDIO WANATABIA ZA WIZI HAPA TANZANIA
Ongezea hapo:

1. Kilimanjaro Cooperative bank iko huko Kilimanjaro( ombeni, Kingazi, makwebe) wapo magereza / wafungwe tu.

2. Akiba bank

3. Azania Bank ( kulikuwa na kijizi kimoja kinaitwa Swai, mtumishi wa Azania).

3. Saccos zote ni wezi wa mchana kweupe na wanashirikiana na mabank)
 
NMB wana shida sana, inaonesha mfumo wao wa kielektroniki unaotuma ujumbe kwa mwenye akaunti ni wa hovyo kiasi kwamba mfanyakazi wa hiyo bank anaweza kuuchezea anavyotaka.

Nimewekeza pesa kwenye hii bank, ila cha ajabu muda wa gawio ukifika pesa zinaingia kimya kimya.
Nimeshawalalamikia sana na kuwaambia huo utaratibu ni mwanya wa wizi, wakaziba masikio....yametimia!
Hata mm nilishangaa. Waliniingizia gawio langu kimyakimya. Nilijiuliza kulikoni, nikakosa jibu. Walisema hakutakuwa na mkutano wa wanahisa kukutana. Jambo la ajabu mkutano ulifanyika Arusha kimyakimya. Na watu kadhaa walishiriki. Benki hii inatakiwa ifumuliwe iundwe upya
 
Benki za kibongo siziamini.

Mimi mwenyewe kuna rafiki yangu mpaka sasa anakimbizana na watu wa benki moja kubwa Bongo iliyopata tuzo hivi karibuni, kuna kama milioni 250 zake hazijulikani zilipo.

Maafisa wa usalama wa benki badala ya kuona aibu na kufanya kazi kuzirudisha, wanafanya uchunguzi mwezi wa 6 huu.

By comparison, more than 10 years ago, mimi nilishawahi kuibiwa $4,000 Citibank. Kuna jamaa walipata details zangu wakachonga kadi, wakatoa hela Dubai.

Citibank walikuwa so embarassed, niliwapigia simu Alhamisi, Jumatatu hela zikawa zimerudi tayari.

Walichofanya ni kuniuliza tu kuhakiki kama nimempa mtu kadi yangu na pin number. Nikasema sijampa. Wakaniuliza kama nimetoka nje ya Marekani wakati huo, nikasema sijatoka. Wakaangalia wenyewe wakaona mchezo umechezwa Dubai. Halafu wakajua kuwa kuna genge fulani linacheza ule mchezo. Wakanirudishia hela zangu mara moja.

Mpaka leo huniambii kitu kuhusu Citibank na Customer Service yao kwenye haya mambo ya kurudisha hela zinazoibiwa.

Bongo unaibiwa wewe halafu benki bado inakuzungusha haiogopi hata bad publicity!
 
Mfanyabiashara maarufu katika mikoa ya Arusha, Dar na Dodoma Joseph Kalugendo mkazi wa Moshoni jijini Arusha, ameibiwa fedha zake zaidi ya milioni 100 katika benki ya NMB tawi la Clock Tower Arusha na mtumishi wa benki hiyo.

Taarifa ambazo zimethibitishwa na Mfanyabiashara huyo amedai kuwa siku za usoni alienda katika benki hiyo kwa ajili ya kuchukua fedha ndipo alipopigwa na butwaa kukuta kitita hicho hakipo.

Meneja wa benki hiyo Kanda ya Kaskazini Praygod Mphuru alipohojiwa alikiri kuwepo kwa tukio hilo akidai tayari wamemsimamisha kazi mfanyakazi wao Samweli na kwamba suala hilo linafanyiwa kazi na kuomba suala hilo lisitangazwe.

Joseph ambaye hufanya biashara za bar na kusambaza vyakula kwenye kambi za jeshi anadaiwa kulundika kiasi hicho cha fedha kwa muda mrefu bila kutoa kiasi, na kwamba mfanyakazi huyo aliona huenda anayeimiliki alishakufa na kuanza kuchomoa kidogo kidogo na kufikia zaidi ya Tsh. Milioni 100.

Hata hivyo baada ya taarifa hizo kubainika uongozi wa benki ulifanya kikao kizito na kubaini kwamba mfanyakazi wao aliyefahamika kwa jina moja la Samweli ndiye aliyehusika na wizi huo kwa kuchomoa fedha hizo kidogo kidogo hadi kufikia hicho cha fedha.

Uongozi wa benki hiyo tayari umemsimamisha kazi lakini suala hilo bado lipo kimya huku Mfanyabiashara huyo akilalamikia hatima ya fedha zake, maana benki hiyo kuwa kimya na haimpi jibu linaloeweka namna ya kurejeshewa.

Unaelewa nini juu ya 'siku za usoni'!?
 
Kumbe hawa jamaa wana uwezo wa kukwapua hela zetu
Kuna kisa kimoja kilinipa maswali sana.

Kuna shangazi yangu mmoja Huwa yuko kijijini ana shughuli zake za kilimo. Sasa kuna kiwanja chake kilikuwa Morogoro maeneo ya ifakara, Binti yake akakiuza. Akamwambia binti yake Mil 1 amuwekee kwenye simu yake na laki 5 amuwekee bank. Sasa ile ya kwenye simu ilikaa zaidi ya mwaka hajaigusa.

Sasa siku ya siku ameenda 'center' kwa wakala kutoa laki 1, inagoma. Kumpa wakala anamuambia 'mama mbona hii line haijasajiliwa ....money?' Shangazi akamuonyesha message ya muamala wa kupokea Mil 1. Kuwapigia Call center, wanamuambia hajawahi jiunga 'air...money'. Ikabidi aende wilayani duka la huduma kwa wateja, nao wakawa na jibu hilo hilo. Alisumbukia week nzima; ulokole wake akaamua muachia Mungu tu.

Nimekuja learn hili tukio baada ya Mwezi, kuna jamaa yangu yukn kwenye mitandao, akaniambia hiyo issue imepigwa na watu juu wa mtandao huo.
 
Siwezi kukudanganya kama wapo watu wa mtwara humu ndani watakuwa wanamfahamu mzee haule bambo ana fremu zake kama 10 pale sokoni karibu na shule ya chikongola na huyo kinyozi ni saidi mkwango ana saluni yake kule bima na pale kwenye jengo la mother house anayo saluni nyingine na hiyo kluger anayoendesha kapewa bure na huyo mzee bambo,na tukija kwa huyo kichaa aliekakopesha pesa ni rama lupanda maarufu daresalama ndogo na huyo aliekampa ni mbalawazi ambae siku hizi ana kiwanda cha kufyatua matofali hapo magomeni kwenye makutano ya barabara
Daah wewe wa mtwara kabisa unamkumbuka kweka boss nsijute na skoya alikua ana pesa ndefu ila alifariki tayari.
 
Benki za kibongo siziamini.

Mimi mwenyewe kuna rafiki yangu mpaka sasa anakimbizana na watu wa benki moja kubwa Bingo iliyopata tuzo hivi karibuni, kuna kama milioni 250 zake hazijulikani zilipo.

Maafisa wa usalama wa benki badala ya kuona aibu na kufanya kazi kuzirudisha, wanafanya uchunguzi mwezi wa 6 huu.

By comparison, more than 10 years ago, mimi nilishawahi kuibiwa $4,000 Citibank. Kuna jamaa walipata details zangu wakachonga kadi, wakatoa hela Dubai.

Citibank walikuwa so embarassed, niliwapigia simu Alhamisi, Jumatatu hela zikawa zimerudi tayari.

Walichofanya ni kuniuliza tu kuhakiki kama nimempa mtu kadi yangu na pin number. Nikasema sijampa. Wakaniuliza kama nimetoka nje ya Marekani wakati huo, nikasema sijatoka. Wakaangalia wenyewe wakaona mchezo umechezwa Dubai. Halafu wakajua kuwa kuna genge fulani linacheza ule mchezo. Wakanirudishia hela zangu mara moja.

Mpaka leo huniambii kitu kuhusu Citibank na Customer Service yao kwenye haya mambo ya kurudisha hela zinazoibiwa.

Bongo unaibiwa wewe halafu benki bado inakuzungusha haiogopi hata bad publicity!
City bank sio hiyo ilitokea Tukio la kasusura zikaibiwaa Dollar za kutoshaa[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Kuna kisa kimoja kilinipa maswali sana.

Kuna shangazi yangu mmoja Huwa yuko kijijini ana shughuli zake za kilimo. Sasa kuna kiwanja chake kilikuwa Morogoro maeneo ya ifakara, Binti yake akakiuza. Akamwambia binti yake Mil 1 amuwekee kwenye simu yake na laki 5 amuwekee bank. Sasa ile ya kwenye simu ilikaa zaidi ya mwaka hajaigusa.

Sasa siku ya siku ameenda 'center' kwa wakala kutoa laki 1, inagoma. Kumpa wakala anamuambia 'mama mbona hii line haijasajiliwa ....money?' Shangazi akamuonyesha message ya muamala wa kupokea Mil 1. Kuwapigia Call center, wanamuambia hajawahi jiunga 'air...money'. Ikabidi aende wilayani duka la huduma kwa wateja, nao wakawa na jibu hilo hilo. Alisumbukia week nzima; ulokole wake akaamua muachia Mungu tu.

Nimekuja learn hili tukio baada ya Mwezi, kuna jamaa yangu yukn kwenye mitandao, akaniambia hiyo issue imepigwa na watu juu wa mtandao huo.
Aaha shida huyo maza nae alikwamaa Unaweka hela yote hiyo kwenye simu na huitumii laini???? Huwa zinafungwaa tena ubayaa wanafunga na Kumpa mtu mwingine chap chap mzeee ili mradi helaa ipigwee kihalaliii bila longolongooo[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]
 
Mzee hiyo line alikuwa anaitumia kwenye Mawasiliano kama kawaida
 
City bank sio hiyo ilitokea Tukio la kasusura zikaibiwaa Dollar za kutoshaa[emoji3][emoji3][emoji3]
Hii Citibank North America mkuu, sio Citibank ya Bongo.

Halafu, point si kwamba hela haziibiwi. Benki hela zitaibiwa tu.

Hiyo si issue.

Issue ni, hela zako zikiibiwa, benki inakurudishia kwa haraka vipi?

Hivi Bongo hela zikiwa benki ziko insured kivipi?

Maana najua Marekani hela mpaka $100,000 ziko FDIC insured.
 
Back
Top Bottom