DOKEZO Mfanyabiashara maarufu Arusha aibiwa Tsh. Milioni 100 kwenye akaunti ya Benki ya NMB

DOKEZO Mfanyabiashara maarufu Arusha aibiwa Tsh. Milioni 100 kwenye akaunti ya Benki ya NMB

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Ni kweli. Kuna kesi nyingi za warithi kudhulumiwa na kudanganywa kuhusu kiasi cha fedha kilichokuwa kwenye account ya marehemu.

Binafsi mzee wangu alikuwa anafanya shughuli zake na alikuwa anaweka fedha benki pia Alikuwa mstaafu so alikuwa analipwa Pension yake via NMB. Mwaka ambao mzee alifariki, alivuna mpunga na akauza gunia zaidi ya 500 ambazo alipeleka benki. Baada ya kufariki na tulikaa muda mrefu kupata utaratibu wa mirathi kwenda benki tunaambiwa mzee alikuwa na laki saba tu benki.
Kwanini msiombe bank statement??
 
Wanachofanya anagushi sahihi yako kisha kila kitu kinaendelea kwa kughushi tu kuanzia kuomba kadi na kuendelea. Naku-mention kwenye uzi mmoja ambao mfanyakazi wa CRDB ubungo aliiba pesa za mteja zaidi ya milioni 100 kwa mtindo huu mwaka 2019.
Uzi uko wapi mkuu?
 
Inaonyesha watumiaji wengi wa huduma za kibenki hawajui haki zao. Taarifa hii imebandikwa kila banking hall kwa sababu ni regulatory requirement, kwamba ukipeleka malalamiko yako benki na usipopata majibu una haki ya kwenda kupeleka malalamiko dawati la malalamiko la benki kuu. Hakikisha una ushahidi kwamba ulishapeleka malalamiko benki. Hapo utaona jinsi watakavyikimbizana kusolve issue yako. Huna haja ya kusubiri pesa yako miezi sita wakati zimeibiwa kwa uzembe wao
 
Wakuu baada ya kuona huu uzi si nikasema ngoja nikaangalie salio japo kwenye account yangu, Bwana weeh hawa jamaa kikweli kabisa wanapiga bhana hii sio sawa yaani nilitegemea kwenye acc yangu nikute _.2 nimekuta _.1.5
 
Mtanzania haaminiki kwenye mambo ya fedha. Narudia tena: mtanzania haaminiki kwenye mambo ya fedha. Najua duniani kote binadamu kwenye fedha ni kitu kingine lakini kwa Tanzania ni zaidi. Benki nyingi tu (labda ondoa zile za kimataifa) wafanyakazi wake hawaaminiki. Bongo ukiwa na fedha benki inatakiwa kila uchwao uwe unaangalia balance. Na wakati wa kutoa kama unatoa fedha nyingi uwe makini sana kwani unaweza kuwekewa majambazi.
Polisi wanadeal na waandamanaji kiliko wahalifu kama hao
 
Back
Top Bottom