DOKEZO Mfanyabiashara maarufu Arusha aibiwa Tsh. Milioni 100 kwenye akaunti ya Benki ya NMB

DOKEZO Mfanyabiashara maarufu Arusha aibiwa Tsh. Milioni 100 kwenye akaunti ya Benki ya NMB

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Joseph ambaye hufanya biashara za bar na kusambaza vyakula kwenye kambi za jeshi anadaiwa kulundika kiasi hicho cha fedha kwa muda mrefu bila kutoa kiasi, na kwamba mfanyakazi huyo aliona huenda anayeimiliki alishakufa na kuanza kuchomoa kidogo kidogo na kufikia zaidi ya Tsh. Milioni 100.
Duh!...hii kali..
 
Mfanyabiashara maarufu katika mikoa ya Arusha, Dar na Dodoma Joseph Kalugendo mkazi wa Moshoni jijini Arusha, ameibiwa fedha zake zaidi ya milioni 100 katika benki ya NMB tawi la Clock Tower Arusha na mtumishi wa benki hiyo.

Taarifa ambazo zimethibitishwa na Mfanyabiashara huyo amedai kuwa siku za usoni alienda katika benki hiyo kwa ajili ya kuchukua fedha ndipo alipopigwa na butwaa kukuta kitita hicho hakipo.

Meneja wa benki hiyo Kanda ya Kaskazini Praygod Mphuru alipohojiwa alikiri kuwepo kwa tukio hilo akidai tayari wamemsimamisha kazi mfanyakazi wao Samweli na kwamba suala hilo linafanyiwa kazi na kuomba suala hilo lisitangazwe.

Pia vigogo wa benki hiyo kwa sasa wanahaha kutafuta mchawi aliyetoa taarifa hizo kwa waandishi wa habari na tayari baadhi ya wafanyakazi wameitwa na kuhojiwa juu ya taarifa hizo za ndani kufika kwa wanahabari

Joseph ambaye hufanya biashara za bar na kusambaza vyakula kwenye kambi za jeshi anadaiwa kulundika kiasi hicho cha fedha kwa muda mrefu bila kutoa kiasi, na kwamba mfanyakazi huyo aliona huenda anayeimiliki alishakufa na kuanza kuchomoa kidogo kidogo na kufikia zaidi ya Tsh. Milioni 100.

Hata hivyo baada ya taarifa hizo kubainika uongozi wa benki ulifanya kikao kizito na kubaini kwamba mfanyakazi wao aliyefahamika kwa jina moja la Samweli ndiye aliyehusika na wizi huo kwa kuchomoa fedha hizo kidogo kidogo hadi kufikia hicho cha fedha.

Uongozi wa benki hiyo tayari umemsimamisha kazi lakini suala hilo bado lipo kimya huku Mfanyabiashara huyo akilalamikia hatima ya fedha zake, maana benki hiyo kuwa kimya na haimpi jibu linaloeweka namna ya kurejeshewa.

Hiyo picha ni ya mfanyabiashara au ni ya tapeli? Benki ya kitapeli hiyo mnawekaje pesa nyie?!!
Nmb
 
hivi inakuwaje mtu achomoe pesa halafu usipate msg kwenye simu yako? au kuna namna huwa wanamute? na nini nifanye ili nisiibiwe, hapo hiyo bank wanatutisha sasa.
 
NMB na CRDB huwa nashangaa wanaozitumia. Ni benki za hovyo. KCB, Amana Bank, Azania, Exim, na ACB kwa uchache hazina shida.
binafsi NMB huwa hela ikiingia ni ya kutumia au kufanyia mambo ya biashara, au la, naichomoa naweka STANBIC hiyo ndio huwa naamini ni benki yenye macho makali walau.
 
FNB walishawahi mfanyia jamaa yangu hivyo hivyo kumchomolea pesa kibao kwenye account yake ya USD. Jamaa alikuwa kifungoni nje ya nchi. Alipotoka kaibuka kudai mpunga wake, mavi yaliwagonga chupi maana kipindi cha kifungo walimzungusha sana mkewe katika kufuatilia pesa.

Walimpa fidia ya 35% juu ya kile kiasi kilichopigwa kwa ombi kwamba asitangaze wala kwenda kwenye vyombo vya sheria. Baada muamala kusoma tu, jamaa akafunga na account yenyewe.
Daahh..kumbeeee....baasii Kuna watu wengi pesa zao zinachotwa haswaa ukifa bila nduguzo kujua kitu
 
Barclays pia kuna mwana aliikula milioni 300 alikuwa ameimaliza yote kwenye Bata alipokamatwa alikuwa hana hata hela ya mawakili.Tulimsaidia tulikuwa hatujui mwenzetu hela anapata wapi. Yaani tulishangaa hela yote huo hana hata kiwanja hata shamba.
Hiyo banki ndio imetoa Bwana Koroso wa Helmi@#$** kwani alipiga 1B. Watu wanapiga sana huko mabenki.
 
Siwezi kukudanganya kama wapo watu wa mtwara humu ndani watakuwa wanamfahamu mzee haule bambo ana fremu zake kama 10 pale sokoni karibu na shule ya chikongola na huyo kinyozi ni saidi mkwango ana saluni yake kule bima na pale kwenye jengo la mother house anayo saluni nyingine na hiyo kluger anayoendesha kapewa bure na huyo mzee bambo,na tukija kwa huyo kichaa aliekakopesha pesa ni rama lupanda maarufu daresalama ndogo na huyo aliekampa ni mbalawazi ambae siku hizi ana kiwanda cha kufyatua matofali hapo magomeni kwenye makutano ya barabara
Mipa nammya nnume uyooo
 
Hao niwezi walishamwibia bab wawatu bosy wetu ml 250 tena zilikuja kwa dola na ilikuwa ya wateja wanakuja huku tanzania wa mwaka mzima palikuwa hapatoshi walituzungusha sana , benki zenye wizi wakuonekana ni hizi CRDB, NBC , BOA, NMB,STANBIC ,EXIM BANK NDIO WANATABIA ZA WIZI HAPA TANZANIA
Duhhhh...kumbee
 
Back
Top Bottom