DOKEZO Mfanyabiashara maarufu Arusha aibiwa Tsh. Milioni 100 kwenye akaunti ya Benki ya NMB

DOKEZO Mfanyabiashara maarufu Arusha aibiwa Tsh. Milioni 100 kwenye akaunti ya Benki ya NMB

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Benki za kibongo siziamini.

Mimi mwenyewe kuna rafiki yangu mpaka sasa anakimbizana na watu wa benki moja kubwa Bingo iliyopata tuzo hivi karibuni, kuna kama milioni 250 zake hazijulikani zilipo.

Maafisa wa usalama wa benki badala ya kuona aibu na kufanya kazi kuzirudisha, wanafanya uchunguzi mwezi wa 6 huu.

By comparison, more than 10 years ago, mimi nilishawahi kuibiwa $4,000 Citibank. Kuna jamaa walipata details zangu wakachonga kadi, wakatoa hela Dubai.

Citibank walikuwa so embarassed, niliwapigia simu Alhamisi, Jumatatu hela zikawa zimerudi tayari.

Walichofanya ni kuniuliza tu kuhakiki kama nimempa mtu kadi yangu na pin number. Nikasema sijampa. Wakaniuliza kama nimetoka nje ya Marekani wakati huo, nikasema sijatoka. Wakaangalia wenyewe wakaona mchezo umechezwa Dubai. Halafu wakajua kuwa kuna genge fulani linacheza ule mchezo. Wakanirudishia hela zangu mara moja.

Mpaka leo huniambii kitu kuhusu Citibank na Customer Service yao kwenye haya mambo ya kurudisha hela zinazoibiwa.

Bongo unaibiwa wewe halafu benki bado inakuzungusha haiogopi hata bad publicity!
Hongeraa brother wenzetu Huko wanajua maana ya kulinda brand na kutunza reputation Yao,bongo wanajua hakuna madhara yoyote Yale yatawakuta kisheria na hata kitaswira Yao
Nchi zetu hizi taabu tupu
 
Kuna kisa kimoja kilinipa maswali sana.

Kuna shangazi yangu mmoja Huwa yuko kijijini ana shughuli zake za kilimo. Sasa kuna kiwanja chake kilikuwa Morogoro maeneo ya ifakara, Binti yake akakiuza. Akamwambia binti yake Mil 1 amuwekee kwenye simu yake na laki 5 amuwekee bank. Sasa ile ya kwenye simu ilikaa zaidi ya mwaka hajaigusa.

Sasa siku ya siku ameenda 'center' kwa wakala kutoa laki 1, inagoma. Kumpa wakala anamuambia 'mama mbona hii line haijasajiliwa ....money?' Shangazi akamuonyesha message ya muamala wa kupokea Mil 1. Kuwapigia Call center, wanamuambia hajawahi jiunga 'air...money'. Ikabidi aende wilayani duka la huduma kwa wateja, nao wakawa na jibu hilo hilo. Alisumbukia week nzima; ulokole wake akaamua muachia Mungu tu.

Nimekuja learn hili tukio baada ya Mwezi, kuna jamaa yangu yukn kwenye mitandao, akaniambia hiyo issue imepigwa na watu juu wa mtandao huo.
Dhambi hizii jamani daahhhh
Walidhani kafa au vipi...
 
Ni kweli. Kuna kesi nyingi za warithi kudhulumiwa na kudanganywa kuhusu kiasi cha fedha kilichokuwa kwenye account ya marehemu.

Binafsi mzee wangu alikuwa anafanya shughuli zake na alikuwa anaweka fedha benki pia Alikuwa mstaafu so alikuwa analipwa Pension yake via NMB. Mwaka ambao mzee alifariki, alivuna mpunga na akauza gunia zaidi ya 500 ambazo alipeleka benki. Baada ya kufariki na tulikaa muda mrefu kupata utaratibu wa mirathi kwenda benki tunaambiwa mzee alikuwa na laki saba tu benki.
Na kama ni wilayani rahisi kuibiwa maana vifo vya watu km hao hujulikana na watu wengi hvyo wanawahi fastaaa tu
 
Bank ya NMB sio salama kabisa, matukio na malalamiko ya wizi ni mengi sana. Mimi mwenyewe ni muhanga wa kupigwa na hii Bank.

Serikali fanyeni uchunguzi kwenye hii Bank maana ni hatari sana, anzeni na pale Mbezi Beach Africana.

Ndomana matukio ya vifo vya wafanyakazi wa Bank ni vingi sababu ya haya mambo.

NMB nilihama muda sana.
Unachosema ni sahihi NMB haifai wizi na utapeli ni mwingi sana.
 
Hahahaha njaa itakuua sana dogo bahati mzuri nimewataja wahusika wote na humu wapo wengi watu wa mtwara tena wa sokoni na hivyo visa wanavijua vizuri sana...acha makasiriko sasa je nikikuletea kisa cha pedeshee kide baada ya kuipiga zaidi ya milion 150 za ambari kwa ujeuri wake akachukua karai lililo na mafuta ya moto ambayo wanakaangia chipsi akammwagia mtu pale mnarani na akampeleka yeye mwenyewe hospital na akawalipa ndugu zake mgonjwa Cash napo si utabisha?
Ndo shida ya wamakonde kibri na dharau saña wakipata unammwagia mtu mafuta kisa 150m...an evil acts,ndo maana tunadharaulika mnoo...from no where ummwagie mtu mafuta
Ndo Yale ya kuyapa talaka makopa kisa pesa za koroshoo
Alifanya ujinga sana
 
Ndo shida ya wamakonde kibri na dharau saña wakipata unammwagia mtu mafuta kisa 150m...an evil acts,ndo maana tunadharaulika mnoo...from no where ummwagie mtu mafuta
Ndo Yale ya kuyapa talaka makopa kisa pesa za koroshoo
Alifanya ujinga sana
Kumbe mkuu nawewe ni wahuku? ila mtwara ilikuwa na mzinguko mkubwa wa pesa ila alivyoingia magufuli kaharibu mzinguko wote kwasababu makampuni yote yalihama hapa mjini na pia machafuko ya msumbiji nayo ikachangia kuuondosha kabisa mzinguko wa pesa mjini kwasababu mipaka ilifungwa
 
Inakuwaje pesa zichomolewe asipewe taarifa kwa ujumbe mfupi? Au huyo jamaa alifanya yake zikitolewa asipate taarifa?
Kama aliweza kuchomoa hela, anaweza pia kumbadilishia namba kwenye profile. By the way, kama hujasajili mobile money, hupati ka meseji
 
Hao niwezi walishamwibia bab wawatu bosy wetu ml 250 tena zilikuja kwa dola na ilikuwa ya wateja wanakuja huku tanzania wa mwaka mzima palikuwa hapatoshi walituzungusha sana , benki zenye wizi wakuonekana ni hizi CRDB, NBC , BOA, NMB,STANBIC ,EXIM BANK NDIO WANATABIA ZA WIZI HAPA TANZANIA

Sasa hapa naona ni benki zote
 
Umenikumbusha mwaka fulani MKopo wangu wa kwanza nilichukua NBC. nikaambiwa mshahara wangu unaweza kupata milioni 10. Ila ajabu baada ya kupokea mkopo nikaanza kuona makato yanakuwa makubwa. Nikawaconsult. Kwa mshtuko mkubwa nikakuta makabrasha yanaonesha nimekopa 14m. Kumbe wale vijana wa mikopo walicheza mchezo. Sijui walimaliza vipi ila mi makato yangu yakawekwa sawa..
 
Ongezea hapo:

1. Kilimanjaro Cooperative bank iko huko Kilimanjaro( ombeni, Kingazi, makwebe) wapo magereza / wafungwe tu.

2. Akiba bank

3. Azania Bank ( kulikuwa na kijizi kimoja kinaitwa Swai, mtumishi wa Azania).

3. Saccos zote ni wezi wa mchana kweupe na wanashirikiana na mabank)
Kijizi nimecheka sana halafu ndio maana huwa riba nijuu sana
 
Ujinga wa kuiba pesa kwa kudonoa donoa mara nyingi huwa hazina cha maana unachofanyia. Ukute jamaa alikuwa anachukua Milioni moja moja na kwenda kulia bata, leo hii ukimwambia kapiga Mil. 100 ataona kama kaongezewa 00.

Mbongo mpe kichwa cha habari aandike story ndio ww
 
Back
Top Bottom