Mfanyakazi wa ndani auawa Uarabuni na mwili wake kutupwa chini ya gari

Mfanyakazi wa ndani auawa Uarabuni na mwili wake kutupwa chini ya gari

Riski ni kubwa mno.....
Uko sahihi, lakini hatari hizo zimekuwa zikielezwa na matukio kushuhudiwa miaka nenda rudi. Ila watu hawaachi kwenda kwa sababu ya uwezekano wa kutoka huko.

Kila kazi ina hatari zake, ingawa zatofautiana. Kuanzia shughuli za uchimbaji madini, mchanga, udereva, unesi, uvuvi n.k

Hata kuwa na pesa hapa Bongo ni hatari, majambazi watakuwa wanakumendea mendea. Lakini kila mmoja anapenda awe nazo.

Wenyewe wanasema ni bora ufe watafuta pesa kuliko kufa kwa umasikini na njaa.
 
Jiulize waarabu waliwachukua wafrika wengi sana kwenye utumwa kama vijakazi lakini hakuna waarabu weusi uko kwao kwann mbona marekani wapo ulaya wapo south america wapo na wamejichanganya vizuri tu..

Sent using Jamii Forums mobile app
Ficha umbumbumbu wako. Jaribu hata kugoogle hao waarabu weusi kabla yakuongea vitu usivyovijua. Tatizo lako kubwa ni kutotoka nje ya mipaka ya Tanzania.

Hawa wanaongelewa hapa kuwepo Iraq, Saudia, Jordan na Palestina ni wazungu au wachina?

Utakuta nawe eti nawe wazazi wako walikusomesha pengine mpaka kiwango cha digrii lakini washindwa ng'amua vitu vidogo kama hivi.

2020-03-25 16.04.16.jpg
 
Uko sahihi, lakini hatari hizo zimekuwa zikielezwa na matukio kushuhudiwa miaka nenda rudi. Ila watu hawaachi kwenda kwa sababu ya uwezekano wa kutoka huko.

Kila kazi ina hatari zake, ingawa zatofautiana. Kuanzia shughuli za uchimbaji madini, mchanga, udereva, unesi, uvuvi n.k

Hata kuwa na pesa hapa Bongo ni hatari, majambazi watakuwa wanakumendea mendea. Lakini kila mmoja anapenda awe nazo.

Wenyewe wanasema ni bora ufe watafuta pesa kuliko kufa kwa umasikini na njaa.

Mkuu hawa wanaolongalonga na kupayuka wivu tu unasumbua,,,mishahara wanayolipwa haifiki hata robo wanayopewa housegirl kule uarabuni.

Housegirl anapewa 600,000 mpaka 900,000 per month ,,,wakati bongo mfanyakazi wa benki,, secondary, msingi au hata serikalini sidhan ata laki4 wanapewa.

Housegirl mshahara mdogo na kunyanyaswa juu.
 
Wewe nae walewale tu....hujui ila unakisia tu...mimi nina ushuhuda kutoka kwa watu mbalimbali waliokuwa huko...tena kheri uwe muislamu ukiwa mkristo ndo utapata ugumu zaidi....najua unawatetea kisa dini moja ila ujue ni ujinga tu unatetea.
Na kuna waislamu wengi tu wapo against na haya mambo.

Na wewe ukaamini ulichoambiwa kwa hao mashuhuda bila kwenda mwenyewe kuhakiki,,,,yawezekana ulikuwa na plan ya kwenda kutafuta life kule ila ukakutana na mahasidi yasiopenda ufanikishe,,,,co binadamu wote tunapendana au kutakiana kheri katika mafanikio ye2,,wengine wapo kukukatisha tamaa.
 
Unakwama wapi mkuu..?
Mimi nimetoa maoni yangu kulingana na uelewa wangu,.hebu na wewe toa maon yako kulingana na uelewa wako,na usi criticize watu...
Ifike mahala mtu akitoa hoja,mjibu kwa hoja na si kumkhebehi
Huo umaskini unaousema una sababu zake za msingi,na chanzo chake,na theory zake.zipo kisomi si kwa maneno wewe unayoyasema..

Usitake nilete critical facts hapa..jkija kwa hoja pia nitakujibu kwa hoja,ila ukija unajibu kwa kebehi ina maana huna unachoelewa zaid una piga kelele.

Haya lete hizo facts zako
 
Na wewe ukaamini ulichoambiwa kwa hao mashuhuda bila kwenda mwenyewe kuhakiki,,,,yawezekana ulikuwa na plan ya kwenda kutafuta life kule ila ukakutana na mahasidi yasiopenda ufanikishe,,,,co binadamu wote tunapendana au kutakiana kheri katika mafanikio ye2,,wengine wapo kukukatisha tamaa.

Umeanza mabango sasa....Ila Uhalisia ndo huo...hata kama ukikaza sidhani kama utaubadilisha.
 
Mnanyanyaswa halafu mnang'ang'ania kuishi huko,hamna makwenu??
 
Mwenye akili zake hawezi kuamini huu utumbo uliou2ma,,,icpokua wajinga ndio huamini. Nackitika sana kuona weuc wenzangu wakipotoshwa na mabeberu 😁😁

Hivyo vikatuni vyako ningeomba uwawapelekee nyumbani kwenu au gengeni ndio utawakamata,, tunaojielewa hu2pati. kwanza kipindi icho hakukua na camera wala vidcamera,,,,

Arabs towards Africans was also a catalyst. The famous Arab historian of the 14th century, Ibn-Khaldum, wrote: “The only people who accept slavery are the Negroes, because of an inferior degree of humanity, their place being closer to the level of animals.” The question then was: how to see to it that these “animals” did not reproduce in Arab-Muslim
 
........................Nimefungua hiyo link aisee hawa jamaa siyo watu,wana roho mbaya sana hawa umbwa!

Mungu amrehemu huyu binti

Sent from my Redmi Note 5 using Tapatalk
 
Mfanyakazi wa ndani mwenye asili ya Kiafrika Faustina Tay aliyekuwa akifanya kazi nchini Lebanon amekutwa amefariki baada ya kutuma ujumbe kuwa alikuwa akinyanyaswa

Mfanyakazi huyo raia wa miaka 18 kutoka Ghana kabla ya kifo chake alituma ujumbemfupi kwa wanaharakati wa kutetea wafanyakazi wa ndani, na masaa 18 baadae mwili wake ukakutwa chini ya Gari, uchunguzi unaonyesha kuwa alisukumwa juu ya ghorofa na kubamiza kichwa

Nchi ya Lebanon ina wafanyakazi wa ndani wapatao 250,000 na inakadiriwa wafanyakazi wawili hufa kila wiki lakini Serikali haifuatilii mauaji hayo

Chanzo: Al Jazeera
The desperate final days of a domestic worker in LebanonView attachment 1398705
Faustina Tay akielezea mateso yake kwa njia ya video

View attachment 1398704
Faustina Tay siku aliyowasili Lebanon akitokea Ghana
Mabalozi wa kiafrika na serikali zao huwa hawajali matukio kama hili.
 
Back
Top Bottom