KERO Mfumo wa Ajira unawakataa waliosoma kozi ya Development Finance & Investment Planning

KERO Mfumo wa Ajira unawakataa waliosoma kozi ya Development Finance & Investment Planning

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Wadau,

Nimeona ni vyema kutoa mrejesho baada ya mjadala wetu hapa kuhusu mfumo wa ajira kukataa waombaji wa kozi ya Development Finance and Investment Planning kwenye nafasi ya Planning Officer II – TPA.

Kwa sasa mfumo tayari unaruhusu kutuma maombi kwa waliomaliza kozi hiyo kama ilivyoainishwa kwenye sifa.

Nashukuru kwa kila aliyetoa mawazo na pia kwa mamlaka husika kwa kulifanyia kazi kwa haraka.

Naamini ni hatua nzuri ya kuelekea kwenye mfumo jumuishi na unaozingatia sifa halisi za waombaji.

Tuwe tunatoa mrejesho pale mabadiliko chanya yanapotokea.

Ahsanteni sana.
 
Sema izi course zingine mnazo soma duh si Bora ungesoma uchumi pure au finance (accounts) pure
Mimi nimesoma uchumi pure na kwenye category watu wa uchumi wametuweka pia lkn kila nikijaribu ku-apply hiyo Planning Officer II (TPA) inanitema
 
Hizi ajira TPA zimekua kusanga sana, mimi mwenyewe nimesoma Uchumi na watu wa uchumi kwenye category za Planning Officer II tupo lkn kila nikiomba mfumo unanigomea
 
Hizi ajira TPA zimekua kusanga sana, mimi mwenyewe nimesoma Uchumi na watu wa uchumi kwenye category za Planning Officer II tupo lkn kila nikiomba mfumo unanigomea
Hii ni changamoto labda ya mfumo
 
Ulitumia njia gani kufanikiwa, uliwapigia direct? Au ulibadili category? Msaada please kwa maslahi ya wengi
Kuwapigia direct simu hazipokelewi , lakni pia nadhani watu walifanya mawasiliano na viongiozi wa chuo kuwajulisha juu ya changamotob yetu chuo wakafanya mawasiliano na wahusika nadhani hii itakuwa imesaidia pia
 
Okay poa nilidhani wewe ndio ulieshughulikia.
 
Ukiona kozi jina lake linaunganishwa na neno "and" hiyo si kozi, umepigwa. Ingekuwa eidha umesoma "Investment Planning" au ungesoma "Development Finance" hapo ingependeza Wala usingepata shida
 
Ukiona kozi jina lake linaunganishwa na neno "and" hiyo si kozi, umepigwa. Ingekuwa eidha umesoma "Investment Planning" au ungesoma "Development Finance" hapo ingependeza Wala usingepata shida
Acha ujuaji hauoni kuwa wametoa mrejesho kuwa tatizo Lao lipo solved
 
Sawa Ila tumia akili kuelezea jambo

Kwa akili yako ndogo ulidhani ajira portal ni Mungu sio

Eti kozi ikiwa na neno and haikubali

Sasa umeona wenzako walivyotoa mrejesho kuwa tatizo lao lipo solved from now.
We komaa na majibu yanayokufurahisha, haya mengine achana nayo mkuu, nzuri ukisomea jambo moja ...achana na mambo ya kusomea x and y kwa wakati mmoja😄. Ningekushauri mapema ila ukiendelea mbele zaidi stiki na kimoja mzee. Labda kama unampango wa kujiajiri na kuajiri wengine sawa
 
Ukiona kozi jina lake linaunganishwa na neno "and" hiyo si kozi, umepigwa. Ingekuwa eidha umesoma "Investment Planning" au ungesoma "Development Finance" hapo ingependeza Wala usingepata shida
Hakuna kitu kama hicho mkuu, kozi yeyote inayotolewa na chuo kilichosajiliwa na serikali ni kozi halali. Kinachokea ajira portal sometimes huwa ni changamoto za kimfumo, mfano mimi nimesoma uchumi pure no and walala nini lkn mfumo bado ulikua unanikataa, ingawa sasa hivi tayari imeshakubali nime-submitt
 
We komaa na majibu yanayokufurahisha, haya mengine achana nayo mkuu, nzuri ukisomea jambo moja ...achana na mambo ya kusomea x and y kwa wakati mmoja😄. Ningekushauri mapema ila ukiendelea mbele zaidi stiki na kimoja mzee. Labda kama unampango wa kujiajiri na kuajiri wengine sawa
Vijana wa JF mna mambo hata sisi wazee ambao tupo na 50+ mnatuambia mambo ya Ajira portal 😁 mnakariri mambo sio
 
Ukiona kozi jina lake linaunganishwa na neno "and" hiyo si kozi, umepigwa. Ingekuwa eidha umesoma "Investment Planning" au ungesoma "Development Finance" hapo ingependeza Wala usingepata shidat

Ukiona kozi jina lake linaunganishwa na neno "and" hiyo si kozi, umepigwa. Ingekuwa eidha umesoma "Investment Planning" au ungesoma "Development Finance" hapo ingependeza Wala usingepata shida
Shida hakuwa kozi mkuu , nadhani ilikuwa changamoto tu ya mfumo , pia wapo watu wamesoma economics mfumo mwanzo ukiwakataa lakni wametoa mrejesho sasa wanaweza kuomba
 
Back
Top Bottom